round kick
JF-Expert Member
- Feb 3, 2025
- 345
- 1,145
Nimeona sio jambo baya Kama tukawa na Uzi maalum kwa ajili ya viwanja vya starehe, Tukutane hapa
Tusisahau kutupiamo vimbwanga na vituko tulivyoahi kukutana navyo tukiwa viwanjani
1. TABIA AMBAZO HUTAKIWI KUZIONYESHA, UTAONEKANA MSHAMBA, KUKU MWENYE KAMBA MGUUNI
2. UKISIKIA MANENO HAYA JUA WANAKUKWEPA (acha kuomba omba, acha kuleta stori za matatizo, n.k)
3. VIWANJA VINAVYOJAA WAZUNGU, WACHINA, WATALII, n.k.
- Kupeana updates za viwanja
- ubora wa huduma zitolewazo kwenye viwanja
- viwanja vya kukwepa
- Tahadhari tuwapo viwanjani
- Elimu kwa wageni wasichekwe wakitembelea viwanja 🤣
Tusisahau kutupiamo vimbwanga na vituko tulivyoahi kukutana navyo tukiwa viwanjani
1. TABIA AMBAZO HUTAKIWI KUZIONYESHA, UTAONEKANA MSHAMBA, KUKU MWENYE KAMBA MGUUNI
- Kushangaa shanga watu - unatolea macho mashoga ukiwakazia macho utatongozwa 😂, wakijua unawashangaa wanaweza kukumwagiwa bia
- Vibe likikolea usianze habari za kuwaambia wenzako kurudi nyumban eti muda umeenda sana, kwani upo boarding ?
- acha kuuliza time kila muda, kwa wazoefu nyimbo flani ikipigwa wanajua kabsa sa hivi muda flani
- Bill ya Lak 2 unaanza kulalamika mbona bill ni kubwa ivyo wakati ni kiwanja kikali
- kubambia anae cheza na mwingne, hii sio bush party
2. UKISIKIA MANENO HAYA JUA WANAKUKWEPA (acha kuomba omba, acha kuleta stori za matatizo, n.k)
- umetukuta ndio tulikuwa tunaondoka Muhudumu tunaomba Bill"
- Mbona meza nyingi, sio lazima tukae meza moja
- Vp huendi nyumbani
- Tunahama, hapa jau
- Nyumbani wanajua upo hapa
- Sisi tunaenda kuna emergency,
- subiri tutakupitia
- Leo kila mtu atumie pesa yake
- hivi job unaingiaga saa ngapi mkuu
3. VIWANJA VINAVYOJAA WAZUNGU, WACHINA, WATALII, n.k.
- Havoc, slipway, cliff, wavuvi camp - DSM
- The Hub, Zeze - Arusha
- Kendwa rocks - Zanzibar
- Ukienda chooni ukirudi nunua kinywaji kingine, usinywe ulichokiacha, kuna uhuni unaitwa spiking
- Vuta chako au cha mtu ambae mpo karibu, usigongee kwa watu usiowajua, wapo wanaomix madawa.
- NI vema kutuliza ugomvi kuliko kuukuza, hujui unaetaka kupigana nae ni nani, kaja na kina nani, n.k.
- No mara waaa, beba mpira, likitokea la kutokea tumia mpira, utasifiwa wewe ni rijali ila majuto kivyako.