Uzi maalum wa wana Mzizima aka Dar es Salaam

Uzi maalum wa wana Mzizima aka Dar es Salaam

SWAHILIYA

Member
Joined
May 13, 2017
Posts
55
Reaction score
116
Jiji la Dar es Salaam lilianza kama Kijiji kidogo cha wavuvi kilichojulikana kama
Mzizima. Kijiji hiki kilianzishwa na Wabalawa ambao walichanganyika na Wazaramo kuelekea kwenye maeneo ya Bara la Afrika Mashariki na ambazo zilijulikana kama ‘Caravan Routes’. Ujenzi wa Makao ya Sultani pamoja na bandari ulianza rasmi mwaka 1865 katika eneo la kijiji cha Mzizima. Ujenzi huo ulikamilika mwaka 1866 na Sultani Majid bin Said kuhamia Dar es Salaam mwaka huo.


Mara baada ya Sultani Majid bin Said kuhamia Dar es Salaam mji ulianza kupanuka na
uchumi wake kukua kwa kasi kubwa japo kwa kipindi kifupi ambapo Sultani Majid
bin Said alifariki mwaka 1870. Kifo cha Sultani huyo kilisababisha kudidimia kwa
maendeleo ya mji wa Dar es Salaam.

Hali hiyo ilianza tena kubadilika mwaka 1884 kufuatia kuanzishwa kwa koloni la Wajerumani la Afrika Mashariki. Mwaka 1891 Serikali ya kikoloni ya Kijerumani iliamua kuhamisha makao makuu ya utawala wake katika Afrika Mashariki kutoka Bagamoyo na kuyaweka Dar es Salaam. Hata hivyo, baada ya Wajerumani kushindwa na Waingereza katika Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia mwaka 1916, Mji wa Dar es Salaam uliendelea kuwa makao makuu ya utawala wa koloni la Waingereza nchini Tanganyika hadi ilipojipatia uhuru wake mwaka 1961.

Dar es Salaam iliendelea kuwa makao makuu ya Tanganyika huru na hatimaye kuwa
makao makuu ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hadi mwaka 1972
wakati Serikali ilipoamua kuhamishia makao yake makuu mjini Dodoma. Jiji la Dar es
Salaam liliendelea kubaki kuwa maarufu kwa kuwa Jiji kuu na kitovu cha biashara
nchini Tanzania.

Hadhi ya Mji, Manispaa na Jiji

Mji wa Dar es Salaam ulitangazwa kuwa Mji wenye Serikali yake ya Mitaa mwaka
1920. Hadhi ya Mji wa Dar es Salaam ilipandishwa kuwa ya Manispaa mwaka 1949 na
baadaye kutunukiwa hadhi ya Jiji na Malkia wa Himaya ya Uingereza tarehe 10
Desemba 1961 mara baada ya Tanganyika kupata uhuru wake. Kuanzia kipindi hicho,
Jiji la Dar es Salaam lilikuwa likiongozwa na Halmashauri ya Jiji hadi mwaka 1972
wakati ambapo Serikali ilivunja Serikali zote za Mitaa nchini ili kutekeleza mfumo wa
madaraka Mikoni. Mamlaka za Miji zilirejeshewa madaraka mwaka 1978 ambapo
Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam lilianza kufanya kazi tena.

Serikali za Mitaa


Kabla ya Ukoloni walitawala Machifu na Wazee wa mila. Wakati wa Utawala wa
Wajerumani (1884-1917) utawala wa kikoloni ulikuwa wa moja kwa moja zaidi maeneo
ya mijini “Direct rule”. Katika kipindi cha utawala wa Waingereza (1917-1961) katika
mwaka 1926 kulikuwa na utawala wa kikabila. Sheria ya Serikali za Mitaa zilianza
mwaka 1953 na Sheria ya Miji mwaka 1946.


Baada ya mwaka 1961 uliondolewa Utawala wa Machifu na kuanza Mfumo wa pamoja
wa Serikali za Mitaa. Mwaka 1972 Serikali za Mitaa ziliondolewa na kuanza Utawala
Mijini na mwaka 1982 Sheria ya Serikali za Mitaa zilirejeshwa tena. Mwaka 1984
ulirejeshwa mfumo wa Serikali za Mitaa na kudumu hadi mwaka 1995. Mpango wa
uboreshaji wa Serikali za Mitaa kuzifanya ziwe na uwezo wa utendaji, uwazi na
uwajibikaji ulianzishwa mwaka 1996 uliojulikana kama “Local Government Reform
Programme”.


Mkoa wa Dar es Salaam wenye eneo na km za mraba 1,800 ulianzishwa kutoka Mkoa
wa Pwani mwaka 1973 ukiwa na Wilaya 3 za Ilala, Kinondoni na Temeke. Mamlaka za
Serikali za Mitaa za Mkoa wa Dar es Salaam zilizopo sasa zilianzishwa mwaka 2000
baada ya kuvunjwa kwa Tume ya Jiji iliyokuwepo kufuatia kuvunjwa kwa Serikali za
Mitaa mwaka 1996 kulikoendelea hadi mwishoni mwa mwaka 1999.


Huu uzi nitakuwa nawaletea updates za watu wa Dar es salaam. waliopita na waliopo na maeneo mbali mbali na pia nitakuwa nawapatia updates ya kinachoendelea socially, economically na politically.

Nitaambatanisha picha mbali mbali

Library ni kubwa mno kwa kweli...

17192223_1690644737901309_2334581465764016624_o.jpg


maulid ya vijana wa sikukuu kkoo. Wa kwanza kushoto ni mbunge wetu wa ilala Mh. Zungu. Katibu wa Saigon Boi Juma Risasi na Mweka hazina wa Saigon Alhaj Mussa Shagow

16707288_1681401058825677_6611630087830377499_o.jpg


18359319_1715699535395829_4424223930534305624_o.jpg




15235559_1647094798922970_1267257799279501110_o.jpg


Hawa ni wadau wa soka wa mkoa wa Dar es Salaam enzi hizo . Mwaka 1986 walichangia kuweka madarakani IDFA. Kutoka kushoto ni Margaret Bwana. Luke luhui. Afisa utamaduni wilaya ilala. Marehem Malik Chanzi. Amin Bakhressa. Chando. Hamisi Kissiwa. Abdallah Kisungura.Mstari wa pili viongozi walikuwa Saidi Kizega. Mussa Shagow. Abdallah Katungunya. Wadau wengine. Gerald Sewe Jaluo. (R.ip) Shabani Kinana(r.i.p)Shaaban Zembwela(r.i.p) Muharami Mkamba na wengineo
 
Swahiliya nakupa.hongera kwa kazi hii. Nami In Shaa Allah nitakuwa nachangia "anecdotes" yaani nyepesi nyepesi za watu ninaowafamu ili kulichangamsha barza lisisinzie. Mtu kama marehemu Kinana, Hamisi Kisiwa, Mussa Shagow ni watu tukifahamiana miaka na kwa ajili hii mikasa ya kutuchekesha haikosi.
 
Swahiliya nakupa.hongera kwa kazi hii. Nami In Shaa Allah nitakuwa nachangia "anecdotes" yaani nyepesi nyepesi za watu ninaowafamu ili kulichangamsha barza lisisinzie. Mtu kama marehemu Kinana, Hamisi Kisiwa, Mussa Shagow ni watu tukifahamiana miaka na kwa ajili hii mikasa ya kutuchekesha haikosi.
Naam mzee wangu nakuona picha ya tatu umeshika camera, au sio wewe?,tunategenea muingie maktaba zenu mtuletee vitu adimu hapa jamvini
 
Kumbe Rage downtown kitambo?
Huu uzi nitakuwa nawaletea updates za watu wa Dar es salaam. waliopita na waliopo na maeneo mbali mbali na pia nitakuwa nawapatia updates ya kinachoendelea socially, economically na politically. Hb

Nitaambatanisha picha mbali mbali

Library ni kubwa mno kwa kweli...

17192223_1690644737901309_2334581465764016624_o.jpg


maulid ya vijana wa sikukuu kkoo. Wa kwanza kushoto ni mbunge wetu wa ilala Mh. Zungu. Katibu wa Saigon Boi Juma Risasi na Mweka hazina wa Saigon Alhaj Mussa Shagow

16707288_1681401058825677_6611630087830377499_o.jpg


18359319_1715699535395829_4424223930534305624_o.jpg




15235559_1647094798922970_1267257799279501110_o.jpg


Hawa ni wadau wa soka wa mkoa wa Dar es Salaam enzi hizo . Mwaka 1986 walichangia kuweka madarakani IDFA. Kutoka kushoto ni Margaret Bwana. Luke luhui. Afisa utamaduni wilaya ilala. Marehem Malik Chanzi. Amin Bakhressa. Chando. Hamisi Kissiwa. Abdallah Kisungura.Mstari wa pili viongozi walikuwa Saidi Kizega. Mussa Shagow. Abdallah Katungunya. Wadau wengine. Gerald Sewe Jaluo. (R.ip) Shabani Kinana(r.i.p)Shaaban Zembwela(r.i.p) Muharami Mkamba na wengineo
 
Naam mzee wangu nakuona picha ya tatu umeshika camera, au sio wewe?,tunategenea muingie maktaba zenu mtuletee vitu adimu hapa jamvini
Msaga...
Ndiye mimi mwenye camera.

Ngoja nikuwekee kitu hpo chini na maelezo kidogo ya Dar es Salaam
ambayo mimi nimekulia katika miaka ya 1950/60.

Hii picha nimeipiga nikiwa MOI nkitazama Jangwani upande wa pili wa Morogoro Road:

22852968_142902479790472_8481386550822511968_n.jpg


Miaka 1960 mimi nikipita hapo kwa miguu nikienda Kinondoni kwa bibi yangu nikitokea Kariakoo. Nikiwa kwa bibi mie na wenzangu tukija sehemu hiyo kufua na tukioga na maji yalikuwa masafi. Tulikuwa na kilima cha kupanda kuingia Moscow basi hicho tukiserereka na makota ya mnazi kama tunaendesha baiskeli. Siku nyingine tukivua dagaa kwa kutumia khanga. Tunakwenda up stream tunawawafukuza nao wanakimbia down stream ambako tumeshika khanga. Ilikuwa raha sana. Masika inakuja hili eneo linapitika wala sikumbuki watu kushindwa kupita kwa maji kujaa.
 
22730058_1782012852097830_3797822435271813123_n.jpg



Kwenye makaburi ya kisutu tar 25/10/2017 siku aliyozikwa mzee wetu Hussein Alibhai maarufu Thethethe.
Alikuwa mwanachama wa klabu ya Saigon na Pan Africa.
Kutoka kulia. Mkweche. Boi Risasi. Nyuma yake Sunday Manara. Carlos Mwinyimkuu. Mussa Shagow. Seif Bwanga. Harudiki Kabunju. Adolph Rishard. . nyuma yake lule. . Wakili Mbwezeleni.aliyevaa suti. Salum Chaurembo . Ali .S. Mwenda. Na mwisho ni Sunday Kayuni. Mzee Hussein alikuwa kipenzi cha watu. Mungu ampe kauli thabit
 
20840801_1757344521231330_6335138247600615273_n.jpg



King KIBADENI MPUTA na Hassan Afif walifanikiwa kurudisha kombe la klabu bingwa Afrika mashariki na kati mwaka 1991 baada kupotea tangu 1975 . Napenda kumpa hongera kaka yangu king Kibaden kwa kukumbukwa na klabu ya simba kupata tuzo ambayo ulikuwa unastahili kutokana na mengi ya kihistoria uliyoyafanya
 
19780430_1741489739483475_3014788082784021770_o.jpg



Kwenye makaburi ya kisutu kumzika Mwanamziki mkongwe Shaaban Dede .
Kutoka kushoto Muhidin Issa Michuzi. Dr. Mwakasole. Carlos Mwinyimkuu. Muddy pizaro. Mussa Mtulya na Alhaj Mussa Shagow . Wote kwa pamoja walikuwa watu wa karibu na marehemu enzi za ujana. Mungu ampe kauli thabit
 
18921158_1728424404123342_7598876508613574153_o.jpg


Kwenye msiba wa Balozi ABDUL KARIM CISCO MTIRO alikuwepo Balozi Mohamed Maharage aliyevaa kanzu nyeusi yeye alikuwa classmate wa akina Mussa Shagow Mnazi Mmoja Primary School miaka ya 60 kushoto katibu wa Saigon Boi Risasi na kulia ni mwana historia Mohammed Saidi.

wote hawa wamekuwa pamoja toka utotoni hadi uzeeni

Allah azidi kuwapa umeri na afya na hikma
 
18403826_1716882295277553_8013531625288090448_o.jpg



Hiki ni kikosi cha Sunderland mwishoni mwa miaka ya 60 na mwanzoni mwa 70.

Balozi tunaomba line up tafadhali...
 
1075494_562892577089792_2007765021_o.jpg


SHEIKH ALI BIN HEMED AL-BUHRY.

KINDAKINDAKI WA "UMWAMWANDE".

Sheikh Ali bin Hemed bin Abdallah bin Said bin Abdallah bin Mas’uud bin Khelef bin Ali bin Said bin Nassor bin Suleiman Al-Buhriy Al-Hinai amezaliwa katika Kijiji cha Saadani, Tanga tarehe 29 August 1889 (sawa na Muharram 1307).

Sheikh Ali bin Hemed alilelewa na wazazi wake hapo Saadani na baadae wazazi wake wakahamia Kijiji cha Darigube (Wanga) kilichopo katika vijiji vya Maere na Kiwavu, Umwamwande, Tanga.

SILSILA YAKE

Sheikh Hemed bin Abdallah bin Said bin Abdallah bin Mas’uud bin Khelef bin Ali bin Said bin Nassor bin Suleiman Al-Buhriy Al-Hinaiy - Maarufu Mwalimu "KIBAO" ndiye baba wa Sheikh Ali Bin Hemed.

Shughuli kubwa ya Baba yake ilikuwa Utabibu na Uandishi. Baadhi ya tenzi maarufu alizotunga Baba yake Sheikh Ali bin Hemed ni kama "Utenzi wa Abdirrahmani na Sufiyani", "Utenzi wa Kadhi Kassim bin Jaafar", "Utenzi wa Seyyidna Huseni bin Ali" na "Utenzi wa VITA VYA WADACHI KUTAMALAKI MRIMA".

Pia aliandika vitabu vingi kama kitabu cha sharia za NIKAH na vinginevyo. Tenzi hizi nyingi zilichukuliwa na J.W.T Allen na kuzitafsiri kwa Kiingereza ambaye alipewa na Sheikh Muhammad bin Hemed, mwanawe Sheikh Hemed bin Abdallah.

Tenzi hizi za familia ya Sheikh Hemed bin Abadallah sasa zimewekwa kwenye Maktaba za Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na mahali kwengineko kwenye tovuti tofauti tofauti za vyuo na za tafiti za Kiswahili.

Mama yake Sheikh Ali Bin Hemed Al-Buhry ni Bibie Maasimbu binti Mwinyimkuu bin Mwinyiamiri.

MASOMO YAKE

Alianza masomo ya Qur'ani hapo kijijini Saadani akisomeshwa na Mwalimu Kadhi Mwinchande. Masomo ya awali ya ilimu ya dini alianza akusomeshwa na baba yake Mzee Hemed bin Abdallah. Pia alihudhuria masomo ya shule, Tanga School, na kusitisha masomo ya shule akiwa darasa la pili ili aendelee na masomo ya dini.

Aliendelea na masomo yake ya dini kwa Sheikh Faqih (kutoka Magunyani na kuishi Mafere, Muheza - Tanga). Alisomeshwa na Sheikh huyu Rubu'ul Ibadah.

Alisoma ilimu ya Faraidh (Mirathi) kwa Sheikh Khamis bin Salim Riyamy wa Tanga. Sheikh Khamis alikuwa Kadhi wa Tanga.

Vilevile alisoma tena ilimu ya Faraidh na ilimu ya Nahau kwa Sheikh Umar bin Stambuli bin Abubakar As-Saady wa Tanga. Sheikh Umar alikuwa Kadhi wa Tanga.

Kisha akaenda Unguja kuzidi kuongeza ilimu yake. Akasoma hapo Unguja kwa Kadhi Sayid bin Abubakar bin Sumeyt. Vile vile akasoma kwa Sheikh Abdallah bin Muhammad Bakathir.

Akazidi kuongeza ilimu yake ya Faraidh kwa kusomeshwa na Sheikh Salim bin Said bin Seif Ash-Sheheyby ambae alikuwa ndiye mjuzi wa ilimu ya Urithi zama hizo kuliko mwanachuoni yeyote mwengine wa pande hizi.

Vile vile hapo Unguja alisoma ilimu ya Balagha na Mantiq kwa Sheikh Abubakar bin Abdallah Bakathir (Huyu ni mtoto wa Sheikh Sheikh Abdallah Bakathir).

Lakini mwanachuoni, kama tajiri, hakinai kwa alichopata, hutaka kila siku kuongeza. Kwa hiyo alikwenda Mombasa kwa Sheikh Al-Amin bin Ali Mazrui akachukuwa aliyoyachukuwa. Ilimu ya Miqaat aliisomea huko.

KIFO CHAKE.

Ilikuwa Jumaapili tarehe 4 August 1957 siku ambayo aliendesha shughuli zake za kusomesha darsa zake kama kawaida mchana kutwa bila ya dalili zozote za dhahiri kwamba lipo tatizo la afya yake na kwamba mchana ule ndio ungekuwa mchana wake wa mwisho wa uhai wake duniani.

Ilipofika usiku majira ya saa nne hivi aliingia ndani kulala. Na huo siku hiyo ukawa mwisho wa umri wake duniani. Alifariki.

Alizikwa mchana wa Jumatatu tarehe 5 August 1957 katika kijiji kile kile alipozaliwa, yaani Saadani.
 
14224888_319214328469923_6686100934972008390_n.jpg

Simba Sports wakiwa mazoezini pamoja na viongozi wao! Taja majina yao!Hapo yupo mwanachama maarufu Baba wa mtangazaji mmoja wa kituo maarufu cha Redio na TV.

 
13450097_262909754100381_4241248873936167130_n.jpg


Mchezaji wa zamani wa timu ya Young Africans na Timu ya Taifa (Taifa Stars)Marehem Mzee Abdulrahman Lukongo. Katika picha hii iliyopigwa Ikulu ya Dsm 1965 wakiwa na Mwl.Nyerere baada kutwa kombe la Gossage(Challenge cup) Marehemu Lukongo anaonekana mstari wa nyuma wa tatu kutoka kulia baada ya Rashid Seif.Hamisi Fikirini(wote marehemu)wa tatu Lukongo anaecheka sana.
 
Back
Top Bottom