Uzi maalum wa wana Mzizima aka Dar es Salaam

Hii nina uhakika ni "economically" na kama mwana Mzizima naomba kuwajulisha...

Wanachama na Wana hisa wa Vitendo SACCOS wanategemea kuzindua na kuanza kazi miradi yao mitatu mipya hivi karibuni.

Miradi hiyo mitatu yote iliyo nje ya Vitendo SACCOS lakini imebuniwa na Wana VTS na itaendeshwa kwa njia ya kuchangiana mitaji na kugawana faida kwa muda maalum.

Miradi inayotarajiwa kuzinduliwa hivi karibuni ni, mradi wa ukumbi wa sinema na mikutano, unaoweza kukaa watu 100, unatambulika kama mradi wa Vitendo Cinema Hall. Huu ni mradi wa muda mfupi kwa waliowekeza. Inatarajiwa kuwa mara tu utakapoanza hivi karibuni, wote waliowekeza kwenye mradi huu kuanza kupata mafao yao na faida ndani ya miezi sita.

Mradi mwingi unaotarajiwa kuzinduliwa hivi karibuni unaojulikana kwa jina la Vitendo Bricks, mradi huu ni wa muda wa kati. Mradi huu utajumuisha utengenezaji wa matofali ya aina tofauti tofauti na pia kwa siku za mwanzoni unatarajiwa kuwa na bidhaa tofauti zinazotokana na mchanga, kokoto na simenti.

Mradi huo pia unatarajiwa kuwa na uwezo wa kutengeneza bidhaa zote za ujenzi zinazotokana na simenti, kokoto na michanga.

Mradi mwengine kuanza hivi karibuni ni mradi wa kijiko (excavator) ya kuchimba na kupakilia mchanga. Mradi huu upo kwenye matayarisho ya mwisho na unategemewa kuanza hivi karibuni. Huu ni mradi unaotarajiwa kuanza kulipa mafao ya wawekezaji na kukamilika ndani ya siku 365 za kazi.

Tunawakaribisha nyote kujiunga na Vitendo SACCOS Ltd. Kwa faida ya wengi.

Vitendo SACCOS imedhamiria kufanya mabadiliko ya uwekezaji Tanzania. Na sasa unaweza kuanza kuwekeza na VTS kwa kuanzia Shillingi 10,000 tu.

Kwa maelezo zaidi, wasiliana nasi kwa simu au whatsapp namba 0625249605.

Ahsanteni sana.
 
17021796_447433318981356_6688860930682555036_n.jpg

The Revolutions hao! Unamuona Wazir wa Njenje aliechuchumaa! Dula wa Tatunane(wa pili kulia) Wadau wa zamani malizieni wakiobaki!
Huyu wa kati aliepozi ki Kung fu atakuwa Teddy Mbarak bassist wa Tatunane pia.
 
1075494_562892577089792_2007765021_o.jpg

SHEIKH ALI BIN HEMED AL-BUHRY.

KINDAKINDAKI WA "UMWAMWANDE".

Sheikh Ali bin Hemed bin Abdallah bin Said bin Abdallah bin Mas’uud bin Khelef bin Ali bin Said bin Nassor bin Suleiman Al-Buhriy Al-Hinai amezaliwa katika Kijiji cha Saadani, Tanga tarehe 29 August 1889 (sawa na Muharram 1307).

Sheikh Ali bin Hemed alilelewa na wazazi wake hapo Saadani na baadae wazazi wake wakahamia Kijiji cha Darigube (Wanga) kilichopo katika vijiji vya Maere na Kiwavu, Umwamwande, Tanga.

SILSILA YAKE

Sheikh Hemed bin Abdallah bin Said bin Abdallah bin Mas’uud bin Khelef bin Ali bin Said bin Nassor bin Suleiman Al-Buhriy Al-Hinaiy - Maarufu Mwalimu "KIBAO" ndiye baba wa Sheikh Ali Bin Hemed.

Shughuli kubwa ya Baba yake ilikuwa Utabibu na Uandishi. Baadhi ya tenzi maarufu alizotunga Baba yake Sheikh Ali bin Hemed ni kama "Utenzi wa Abdirrahmani na Sufiyani", "Utenzi wa Kadhi Kassim bin Jaafar", "Utenzi wa Seyyidna Huseni bin Ali" na "Utenzi wa VITA VYA WADACHI KUTAMALAKI MRIMA".

Pia aliandika vitabu vingi kama kitabu cha sharia za NIKAH na vinginevyo. Tenzi hizi nyingi zilichukuliwa na J.W.T Allen na kuzitafsiri kwa Kiingereza ambaye alipewa na Sheikh Muhammad bin Hemed, mwanawe Sheikh Hemed bin Abdallah.

Tenzi hizi za familia ya Sheikh Hemed bin Abadallah sasa zimewekwa kwenye Maktaba za Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na mahali kwengineko kwenye tovuti tofauti tofauti za vyuo na za tafiti za Kiswahili.

Mama yake Sheikh Ali Bin Hemed Al-Buhry ni Bibie Maasimbu binti Mwinyimkuu bin Mwinyiamiri.

MASOMO YAKE

Alianza masomo ya Qur'ani hapo kijijini Saadani akisomeshwa na Mwalimu Kadhi Mwinchande. Masomo ya awali ya ilimu ya dini alianza akusomeshwa na baba yake Mzee Hemed bin Abdallah. Pia alihudhuria masomo ya shule, Tanga School, na kusitisha masomo ya shule akiwa darasa la pili ili aendelee na masomo ya dini.

Aliendelea na masomo yake ya dini kwa Sheikh Faqih (kutoka Magunyani na kuishi Mafere, Muheza - Tanga). Alisomeshwa na Sheikh huyu Rubu'ul Ibadah.

Alisoma ilimu ya Faraidh (Mirathi) kwa Sheikh Khamis bin Salim Riyamy wa Tanga. Sheikh Khamis alikuwa Kadhi wa Tanga.

Vilevile alisoma tena ilimu ya Faraidh na ilimu ya Nahau kwa Sheikh Umar bin Stambuli bin Abubakar As-Saady wa Tanga. Sheikh Umar alikuwa Kadhi wa Tanga.

Kisha akaenda Unguja kuzidi kuongeza ilimu yake. Akasoma hapo Unguja kwa Kadhi Sayid bin Abubakar bin Sumeyt. Vile vile akasoma kwa Sheikh Abdallah bin Muhammad Bakathir.

Akazidi kuongeza ilimu yake ya Faraidh kwa kusomeshwa na Sheikh Salim bin Said bin Seif Ash-Sheheyby ambae alikuwa ndiye mjuzi wa ilimu ya Urithi zama hizo kuliko mwanachuoni yeyote mwengine wa pande hizi.

Vile vile hapo Unguja alisoma ilimu ya Balagha na Mantiq kwa Sheikh Abubakar bin Abdallah Bakathir (Huyu ni mtoto wa Sheikh Sheikh Abdallah Bakathir).

Lakini mwanachuoni, kama tajiri, hakinai kwa alichopata, hutaka kila siku kuongeza. Kwa hiyo alikwenda Mombasa kwa Sheikh Al-Amin bin Ali Mazrui akachukuwa aliyoyachukuwa. Ilimu ya Miqaat aliisomea huko.

KIFO CHAKE.

Ilikuwa Jumaapili tarehe 4 August 1957 siku ambayo aliendesha shughuli zake za kusomesha darsa zake kama kawaida mchana kutwa bila ya dalili zozote za dhahiri kwamba lipo tatizo la afya yake na kwamba mchana ule ndio ungekuwa mchana wake wa mwisho wa uhai wake duniani.

Ilipofika usiku majira ya saa nne hivi aliingia ndani kulala. Na huo siku hiyo ukawa mwisho wa umri wake duniani. Alifariki.

Alizikwa mchana wa Jumatatu tarehe 5 August 1957 katika kijiji kile kile alipozaliwa, yaani Saadani.
Ahsante sana kwa hidaya hii,
Sikuomba ruksa lakini kwa thamani ya hii makala nimeiweka katika
blog yangu: www.mohammedsaid.com.

Mohamed Said: SHEIKH ALI BIN HEMED AL-BUHRY KINDAKINDAKI WA "UMWAMWANDE"

Naomba jina la mwandishi wa makali haya.
 
17021796_447433318981356_6688860930682555036_n.jpg

The Revolutions hao! Unamuona Wazir wa Njenje aliechuchumaa! Dula wa Tatunane(wa pili kulia) Wadau wa zamani malizieni wakiobaki!

Ndugu zangu ngojeni niheme kwanza.

Haya yote yanaakisi maisha yangu katika miaka ya 1960s katikati hadi 1970s
katika pia.

In Shaa Allah kuna mambo nitaeleza lakini kwa sasa bado kila ikipatikana
nafasi hujikumbusha siku nyingi zilizopita:

22894496_144602246287162_8051809906815459629_n.jpg

Hapa ni nyumbani kwa Dr. Harith Ghassany Muscat 2015 kwenye piano hii 1999 akiwa hatufahamiani
nilimpigia nyimbo hii: ''Crying in the Chapel,'' yeye na mkewe wakinisikiliza na walishangaa sana kwani
picha waliyokuwanayo yangu kuwa mimi ni ''sheikh.'' Dr. Ghassany aliniuliza nimejifunza wapi kupiga
piano?

22814337_144603072953746_8969097268614014041_n.jpg

Hapa ni Humburg 2011 nyumbani kwa Abdillatif Abdalla mwanae Muyaka
alikuwa na guitar anajifunza nilimuonyesha ''chords,'' kidogo na kumpigia,
''The House of the Rising Sun,'' Eric Bardon na Animals...

Abdilatif kama alivyokuwa Dr. Ghassany na yeye alipigwa na butwaa pia...
 
13450097_262909754100381_4241248873936167130_n.jpg

Mchezaji wa zamani wa timu ya Young Africans na Timu ya Taifa (Taifa Stars)Marehem Mzee Abdulrahman Lukongo. Katika picha hii iliyopigwa Ikulu ya Dsm 1965 wakiwa na Mwl.Nyerere baada kutwa kombe la Gossage(Challenge cup) Marehemu Lukongo anaonekana mstari wa nyuma wa tatu kutoka kulia baada ya Rashid Seif.Hamisi Fikirini(wote marehemu)wa tatu Lukongo anaecheka sana.
Abduahman Lukongo yupi tena huyo Maana nilisoma na mtu wa Jina Hilo miaka ya mwishoni 80s ''Kitobo Ndimu'' wa Kariakoo karibu na Jangwani! au ni Babu yake huyo pichani?
 
Mwenye Picha ya Mwalimu wangu Mkuu Chalila aiweke maana nishamsahau
 
1075494_562892577089792_2007765021_o.jpg

SHEIKH ALI BIN HEMED AL-BUHRY.

KINDAKINDAKI WA "UMWAMWANDE".

Sheikh Ali bin Hemed bin Abdallah bin Said bin Abdallah bin Mas’uud bin Khelef bin Ali bin Said bin Nassor bin Suleiman Al-Buhriy Al-Hinai amezaliwa katika Kijiji cha Saadani, Tanga tarehe 29 August 1889 (sawa na Muharram 1307).

Sheikh Ali bin Hemed alilelewa na wazazi wake hapo Saadani na baadae wazazi wake wakahamia Kijiji cha Darigube (Wanga) kilichopo katika vijiji vya Maere na Kiwavu, Umwamwande, Tanga.

SILSILA YAKE

Sheikh Hemed bin Abdallah bin Said bin Abdallah bin Mas’uud bin Khelef bin Ali bin Said bin Nassor bin Suleiman Al-Buhriy Al-Hinaiy - Maarufu Mwalimu "KIBAO" ndiye baba wa Sheikh Ali Bin Hemed.

Shughuli kubwa ya Baba yake ilikuwa Utabibu na Uandishi. Baadhi ya tenzi maarufu alizotunga Baba yake Sheikh Ali bin Hemed ni kama "Utenzi wa Abdirrahmani na Sufiyani", "Utenzi wa Kadhi Kassim bin Jaafar", "Utenzi wa Seyyidna Huseni bin Ali" na "Utenzi wa VITA VYA WADACHI KUTAMALAKI MRIMA".

Pia aliandika vitabu vingi kama kitabu cha sharia za NIKAH na vinginevyo. Tenzi hizi nyingi zilichukuliwa na J.W.T Allen na kuzitafsiri kwa Kiingereza ambaye alipewa na Sheikh Muhammad bin Hemed, mwanawe Sheikh Hemed bin Abdallah.

Tenzi hizi za familia ya Sheikh Hemed bin Abadallah sasa zimewekwa kwenye Maktaba za Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na mahali kwengineko kwenye tovuti tofauti tofauti za vyuo na za tafiti za Kiswahili.

Mama yake Sheikh Ali Bin Hemed Al-Buhry ni Bibie Maasimbu binti Mwinyimkuu bin Mwinyiamiri.

MASOMO YAKE

Alianza masomo ya Qur'ani hapo kijijini Saadani akisomeshwa na Mwalimu Kadhi Mwinchande. Masomo ya awali ya ilimu ya dini alianza akusomeshwa na baba yake Mzee Hemed bin Abdallah. Pia alihudhuria masomo ya shule, Tanga School, na kusitisha masomo ya shule akiwa darasa la pili ili aendelee na masomo ya dini.

Aliendelea na masomo yake ya dini kwa Sheikh Faqih (kutoka Magunyani na kuishi Mafere, Muheza - Tanga). Alisomeshwa na Sheikh huyu Rubu'ul Ibadah.

Alisoma ilimu ya Faraidh (Mirathi) kwa Sheikh Khamis bin Salim Riyamy wa Tanga. Sheikh Khamis alikuwa Kadhi wa Tanga.

Vilevile alisoma tena ilimu ya Faraidh na ilimu ya Nahau kwa Sheikh Umar bin Stambuli bin Abubakar As-Saady wa Tanga. Sheikh Umar alikuwa Kadhi wa Tanga.

Kisha akaenda Unguja kuzidi kuongeza ilimu yake. Akasoma hapo Unguja kwa Kadhi Sayid bin Abubakar bin Sumeyt. Vile vile akasoma kwa Sheikh Abdallah bin Muhammad Bakathir.

Akazidi kuongeza ilimu yake ya Faraidh kwa kusomeshwa na Sheikh Salim bin Said bin Seif Ash-Sheheyby ambae alikuwa ndiye mjuzi wa ilimu ya Urithi zama hizo kuliko mwanachuoni yeyote mwengine wa pande hizi.

Vile vile hapo Unguja alisoma ilimu ya Balagha na Mantiq kwa Sheikh Abubakar bin Abdallah Bakathir (Huyu ni mtoto wa Sheikh Sheikh Abdallah Bakathir).

Lakini mwanachuoni, kama tajiri, hakinai kwa alichopata, hutaka kila siku kuongeza. Kwa hiyo alikwenda Mombasa kwa Sheikh Al-Amin bin Ali Mazrui akachukuwa aliyoyachukuwa. Ilimu ya Miqaat aliisomea huko.

KIFO CHAKE.

Ilikuwa Jumaapili tarehe 4 August 1957 siku ambayo aliendesha shughuli zake za kusomesha darsa zake kama kawaida mchana kutwa bila ya dalili zozote za dhahiri kwamba lipo tatizo la afya yake na kwamba mchana ule ndio ungekuwa mchana wake wa mwisho wa uhai wake duniani.

Ilipofika usiku majira ya saa nne hivi aliingia ndani kulala. Na huo siku hiyo ukawa mwisho wa umri wake duniani. Alifariki.

Alizikwa mchana wa Jumatatu tarehe 5 August 1957 katika kijiji kile kile alipozaliwa, yaani Saadani.
Hii nayo ni ya Dsm (Mzizima) ? au ndio kuharibu Thread yako Mwenyewe? naona kama imekaa kidini zaidi najuta hata kuisoma!
 
Mod bora wahamishie hii thread Jukwaa la Dini
nimekumbuka mbali sana hasa ukiona picha za watu ambao asilimia zaidi ya 90 unawakumbuka na kuwaona i miss mission quarter
 
Mod bora wahamishie hii thread Jukwaa la Dini
Mlaleo,
Nielewavyo mie hili ni jukwaa linaitwa Swahiliya na ikiwa Mswahiliyetu
moja ya tamaduni zetu ni Maulid.

Tunasoma maulid katika harusi.
Tunasoma maulid tukipata mtoto.

Sasa sijui tatizo liko wapi kwa huyo Mswahili kuweka picha ya maulid.

Lakini kubwa hicho chuo cha Abbasiyya kina historia kubwa ya watu
wa Dar es Salaam.

Kwa sisi watoto tuliozaliwa Dar es Salaam ya 1950s ilikuwa lazima mama
akupeleke kwa Sheikh Ramadhani Abbas ukapewe, ''kinga.''

Hii ni historia yetu.

o5Xf2ipjEKW7wHVswEYqhI5TdvNkQYcwoZtxC-hr8Mweue2BT-w_vQTwnS6G10Yr9njrUgK2SzEQHMqUY3VrshLzTYCOzIIdT6Mq5hON-g27zi_8GcPVcfSlZhMo3fZldIBjHUByB95hMPxKjbaH6rhVIBiscO8QtEOZmQ3uEhdXIhI6bi3tYdxunDXaRlNSjqgsqUYsxz1vgKxBj8SJPtuxSy9xl9UDune2-7LVKUofvALllzJ-r9qFWeMXXcxiFKvkCE9MwgzeLrz7P8XDW8huy3laAnfGubQFki1MPWhhORCSErXrmr4ZErOn8WJ7hK7mXqWTofUVX6hB92tf9MiaDOwMIUd0F3CXM-QuulahCrvYYNA8veBVGjxtgn006yogNzR7MCZXM-2o3KgWrzOw8Txnq7NfVJ6sHKgJam85v7oU3rcJRuec7JgoO4qnnwrfErNZM6icfiXsrvy__wYfqciy5-j8rqe30sZfhwiD0w9_ISlM4_pqDQZAcAt5l3h8B51OmngUoKHCllX0iQhHmBWsmnRg5uajWGF7nuL23afMMwGuGyX5uOgQbNOnGwohpxcxjKtlU3q-Oc50ansS7R6G4CuC46scfmf2Sv4=w839-h629-no

Sheikh Abbas Ramadhani Abbas kabla ya zafa Maulid ya Mfungo Sita. Hilo juba huwa karithi kwa baba
yake Sheikh Ramadhani Abbas na huwa halivai hadi siku ya hadhara kama hil. Kila mwaka mie huenda
katika zafa kupiga picha na kuziweka katika blog yangu na watu wengi dunia nzima hufatilia kutaka kujua
maulid ya mwaka huu Abbassiya yalikuwaje.
 
Hii nayo ni ya Dsm (Mzizima) ? au ndio kuharibu Thread yako Mwenyewe? naona kama imekaa kidini zaidi najuta hata kuisoma!
Mlaleo,
Hiyo ni Dar es Salaam ondoa hofu.
Huyo kushoto ni Mufti Sheikh Hassan bin Amir.

Mmoja katika wanafunzi wake alikuwa Sheikh Ramadhani Abbas muasisi
wa Abbasiyya.

Historia ya Sheikh Hassan bin Amir si tu inakwenda na mji wa Dar es Salaam
bali inakwenda na historia ya TANU na kudai uhuru wa Tanganyika na kumjenga
Baba wa Taifa akubalike katika Dar es Salaam ya 1950 na kujenga umoja wa
wananchi.

Ukikerwa na historia hii kwa kuwa unawaona Waislam utakosa na kupitwa na mengi.
Kwetu sisi hawa ni wazee wetu hatuwezi kuacha kuwarehemu.
 
Hapo kwenye red ungeandika tu Shirki! yaani mnatoka nje ya Dini... Uganga na ulozi kinga kwani mkienda kusali hupati?
 
Mlaleo,
Hiyo ni Dar es Salaam ondoa hofu.
Huyo kushoto ni Mufti Sheikh Hassan bin Amir.

Mmoja katika wanafunzi wake alikuwa Sheikh Ramadhani Abbas muasisi
wa Abbasiyya.

Historia ya Sheikh Hassan bin Amir si tu inakwenda na mji wa Dar es Salaam
bali inakwenda na historia ya TANU na kudai uhuru wa Tanganyika na kumjenga
Baba wa Taifa akubalike katika Dar es Salaam ya 1950 na kujenga umoja wa
wananchi.

Ukikerwa na historia hii kwa kuwa unawaona Waislam utakosa na kupitwa na mengi.
Kwetu sisi hawa ni wazee wetu hatuwezi kuacha kuwarehemu.
Hivi wewe mzee huwa unaelewa vichwa vya mada husika au ndio kupost post tu vitu hovyo tu hata sehemu zisizo husika... Thead mtu kaanzisha kuhusu DSM Mzizima and then anapost mambo ya Tanga,Mara shughuri za Ibada wapi na wapi? au na nyie mkiwa mnaswali kuna time mnaacha na mnaanza zungumzia Diamond katoa wimbo gani au leo Njenje au Sikinde wanapiga wapi? lazima ueshimu uhalisia wa jambo lihusulo. kuchanganya changanya mwishowe wasomaji tunashangazwa tunajikuta tupo jukwaa la Dini au la mkoa husika!

Najua povu litakutoka kisa umepost picha za vinanda news isiyo na kichwa wala miguu ndio maana kama facebook vile, nasema kuna vitu vingine tunasoma hadi tunajuta why tumesoma comments.

Unaposema ati nakerwa na Waislam??? are Mental Man? how come unajenga kichwani mwako thought kama hiyo? are you Ok? unahitajika ukapimwe Mkojo Mzee maana kama ushambenga wewe umepitiliza... Sijawahi kerwa zaidi ya kucrash sifa za kijinga tu mtu aletazo.

Nyerere alikuwa na Akili zake na sio hao wazee uwasemao nadhani hujui Siasa ndio maana unatatizwa sana na uwepo wa watazamaji au wasindikizaji katika Siasa ukidhani wao ndio wasababishaji haswa... Siasa ni Kipaji hata kama hukuwa na maneno matamu kama Kawawa ukiwa na Nyota ya uongozi utafanikiwa tu sasa hao wazee walishindwa hadi wakaona wakomae na mwenye akili. siasa zilikuwepo na Waingereza hawakuwa wakoloni bali walitushikia tu Uongozi hadi tutakapokuja weza jiongoza wenyewe. blah blah za Tanu na kadharika ni sehemu ya Matokeo tu.
 
2be8f925db017dda5b64c08ae8c40740.jpg
hapo nipo mzee wngu Haridiki Kabunju ndio wenye mzizima yao...
 
Una ushahidi gani? Kwanini Watanzania huwa mnaleta habari zisizo jitosheleza? Unknown person can claim something with no evidence!.

Mzizima kuna watu Walimiliki Bustani za Mnazi Mmoja na kuzigawa bure kina Rupia,Karimjee kuna watu kama Agakhan na community yake walitisha,Azizi Ally kiasi Mkuu tupe Hostoria za aina hiyo... Sio Kukaa kijiweni na kunywa Kahawa kama Mzee Mo Saidi hihihihi
 
Una ushahidi gani? Kwanini Watanzania huwa mnaleta habari zisizo jitosheleza? Unknown person can claim something with no evidence!
Mie nafikiria siwezi kuongelea watu kwenu uko chato au monduli maana siwajui jambo la busara ni kukaa kmy kwa kitu usichokujiua sio kila kitu lazima uchangie tatizo wenzetu mnapenda sna ujuaji ndio maana mwenzenu anawanjoosha...
 
Umevamia Uzi wenye Mada ya Mkoa wa DSM Mzizima so unapochangia uwe kama mtu mwenye kuitambua vizuri au Mzee wako ni almaarufu n.k sio kuleta mada za Chato ambapo hupajui kama usivyoifahamu Mzizima. Tumia akili kwanza na sio kingine Nguvu hasitakusaidia kuhamisha Mada husika. Hivi hapo ulipochangia unahisi Mwanao akisoma atasema nataka niwe na akili kama za Baba?
 
Umevamia Uzi wenye Mada ya Mkoa wa DSM Mzizima so unapochangia uwe kama mtu mwenye kuitambua vizuri au Mzee wako ni almaarufu n.k sio kuleta mada za Chato ambapo hupajui kama usivyoifahamu Mzizima. Tumia akili kwanza na sio kingine Nguvu hasitakusaidia kuhamisha Mada husika.
Watu wa mzizima tunajua ww mie binafsi Hamid Rubawa doe na livingstone ww nani km sio chato wacheni kujitia kwenye miji ya watu kwani hamna makwenu...
 
62f379f7ba14eafb7fc45eb97c65a418.jpg
wenye mzizima yetu hapo kwenye mazishi ya mzee wngu lukongo...
 
Back
Top Bottom