GAZETI
JF-Expert Member
- Feb 24, 2011
- 5,286
- 6,736
Wakuu binafsi nafanya mazoezi mengi sana, lakini sijui faida zake nafanya tu kwa kuwa mwili unachangamka na muda mwingi nakuwa mtu mwenye furaha tofauti na kipindi ninachoacha mazoezi. Faida nyingine ninayoiona ni kumbukumbu,
kipindi ninachofanya mazoezi ninakuwa na uwezo mzuri sana wa kuhifadhi vitu kichwani.
Heshima nyumbani. Hapo sitaki niseme sana.
Tuwe tunakutana hapa kukumbushana na kupeana moyo kwani mazoezi yataka moyo sana yaani uyafanye kama IBADA hapo tutafanikiwa.
Pia, tunaweza kushauriana ni vyakula gani vizuri kula baada ya mazoezi, binafsi kuanzia leo nimebadili aina ya mlo. Asubuhi nimekula wali, mchicha usioiva vizuri, chai na korosho robo kilo. Mchana natarajia kula ugali na mchicha, embe dodo 2, nanasi na maji.
Karibuni wakuu.