Uzi maalum: Wapenda mazoezi ya viungo tukutane hapa kwa maoni, ushauri, aina za mazoezi, faida zake n.k

Uzi maalum: Wapenda mazoezi ya viungo tukutane hapa kwa maoni, ushauri, aina za mazoezi, faida zake n.k

GAZETI

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2011
Posts
5,286
Reaction score
6,736
Wakuu binafsi nafanya mazoezi mengi sana, lakini sijui faida zake nafanya tu kwa kuwa mwili unachangamka na muda mwingi nakuwa mtu mwenye furaha tofauti na kipindi ninachoacha mazoezi. Faida nyingine ninayoiona ni kumbukumbu,
kipindi ninachofanya mazoezi ninakuwa na uwezo mzuri sana wa kuhifadhi vitu kichwani.

Heshima nyumbani. Hapo sitaki niseme sana.

Tuwe tunakutana hapa kukumbushana na kupeana moyo kwani mazoezi yataka moyo sana yaani uyafanye kama IBADA hapo tutafanikiwa.

Pia, tunaweza kushauriana ni vyakula gani vizuri kula baada ya mazoezi, binafsi kuanzia leo nimebadili aina ya mlo. Asubuhi nimekula wali, mchicha usioiva vizuri, chai na korosho robo kilo. Mchana natarajia kula ugali na mchicha, embe dodo 2, nanasi na maji.

Karibuni wakuu.
 
Kuna uzi humu ukielezea changamoto za mazoezi.

Aliyeuleta ule uzi anadai kuwa sio kwamba mazoezi ni magumu ila utekelezaji wake ndio mgumu.

Ukosefu wa vifaa vya mazoezi.

Watu walitiririka mno kwenye ule na walifurahisha sana jinsi walivyoelezea walipoanza mazoezi na kuyaacha
 
Zoezi bana mkiwa timu linanoga sana na likichangaya linakuaga na alosto

Hapa brother hapa mchizi, kushoto niko mimi aisee tulikua tunakiamsha kinoma

Saizi tuko mbali mbali kwaiyo ile hamasa imepungua naishia kupiga pushups tu
 
Wadau mimi naulizia vifaa vya kufanyia mazoezi kama vya kwenye gym vinapatikana wapi! Hata vya mtumba, suala la kufanya mazoezi ni muhimu sana.
 
Wadau mimi naulizia vifaa vya kufanyia mazoezi kama vya kwenye gym vinapatikana wapi! Hata vya mtumba, suala la kufanya mazoezi ni muhimu sana.
Ngoja wajuvi watakujuza, mimi kwa sasa mazoezi yangu ni kutembea kwa mwendo kasi/haraka(japo hiyo ni nature yangu).

Na mazoezi mengine ni kule 6x6 nikiwa na ubavu wangu[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Hongera kwa kula korosho robo kilo, je itakuwa menyu yako kila asubuhi?
 
Asubuhi supu ya mbuzi na chapati 2

Mchana maziwa mgando robo lita na karanga za kukaanga pakti 2 za sh. mia mia.

Jioni natafuna tango 1 na usiku mboga za majani. Kipato hakikizi mahitaji ila naufurahia mlo na afya ipo safi kabisa.

Mazoezi nafanyia kwenye 6×6 japo ninavifaa vingi vya mzoezi.
 
Mimi napenda sana zoezi la kukimbia asubuhi.
Faida nyingi sana za kiafya nimezipata tangu nilivyoanza mpaka sasa kulinganisha na nilivyokuwa hapo kabla.
Pia huwa nafanya push ups angalau 100 kwa siku na kulift chuma kdg kujenga misuli ya mwili.
Changamoto kubwa ninayokumbana nayo ni kukiacha kitanda alfajiri na kwenda kufanya mazoezi...dah inataka moyo sana!!
Screenshot_2019-10-24-14-25-26.jpeg
Screenshot_2019-10-24-14-25-57.jpeg
Screenshot_2019-10-24-14-26-44.jpeg
Screenshot_2019-11-04-13-43-34.jpeg
Screenshot_2019-12-13-17-32-35.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mazoezi huleta furaha, tiba, huzuia magonjwa. Wataalam wanasema kipimo cha kawaida cha mazoezi ni Dak 30 hapo mwili uwe umetoa jasho la kutosha na kama mfano ulikuwa unakimbia mtu akikusemesha ushindwe kumjibu kwa ufasaha, kutokana na kitendo cha mapigo ya moyo na kuvuta hewa kuwa juu.
 
Back
Top Bottom