Richard
JF-Expert Member
- Oct 23, 2006
- 15,692
- 23,038
Kwa wale wote ambao mko nje ya Tanzania hapa panawahusu
Kwanza tunataka kujua uzoefu changamoto zenu na mnayakabili vipi maisha ya huko
Hapa tupate kujua unapendelea safari na kampuni gani au shirika gani la.ndege ni lipi unalichukia na kwanini??
Mji gani umekaa, je umewahi kubaguliwa?
Unaishi na kina nani huko, masela, umepanga kwako, au unaishi na familia yako,
Mara ya kwanza kupanda pipa nani alikupa mchongo mpaka huko ulipo?
Umewahi pata changamoto yeyote na uliikabili vipi
Je ulisumbuka kupata kibali cha kuishi hapo??
Na wale wa boder za nchi kavu karibu
Kuna mengi sana ya kushare hapa
luambo makiadi Jon Stephano Kiranga Nyani Ngabu Witness ponela venchwa
Mimi nimeishi na kufanya kazi miji ya Toronto Canada, Tennessee USA, London UK na Talinn Estonia.
Nilianzai kusafiri nikiwa kijana mdogo wa skauti lakini nilipofika London nikatulia nikatafuta kazi (miaka ya mwanzo ya 90)
Nilianza kufanya kazi ya ulinzi kwenye hoteli maarufu iitwayo Strand iliyopo karibu kabisa na BBC Bush House London.
Hivyo mimi sasa hivi ni mtaalam wa CCTV, nafunga alarm systems na nipo level ya C yaani nimekuwa vetted kuingia maeneo nyeti na kupiga kazi bila kubughudhiwa.
Mwanzoni nimeishi na masela ya nchi mbalimbali Tanzania, Uganda, Kenya, Gambia, Ghana, Nigeria na Zimbabwe (UK twawaita wazimbabwe jina la "wazimzim")
Wasichana wa kizimbabwe na wakenya wanawapenda sana vijana wa Tanzania wanasema wanapenda kuwa nasi na upole wetu.
Mimi kabla ya kuoa nilikuwa na msichana mmoja aitwae Busiliwe namkumbuka sana huyu binti alivyokuwa akisonga ugali wa kizimbabwe uitwao Saza. Baadae alirudi kwao Zimbabwe na mpaka sasa huwa tunatupiana Hi.
Lakini mwanzoni mwa 2015 nilirudi Tanzania na nikaamua kuwa low profile na sasa ni mjasiriamali na nafanya shughuli zangu mwenyewe lakini nina familia kwenye moja ya nchi hizo tajwa hapo juu.
Nilipoishi na kufanya kazi UK ubaguzi upo lakini unapotea endapo unaonyesha kuwa unazo "skiils" na wazungu wanazihitaji.
Ubaguzi upo lakini ni vigumu kuona kwa macho yako isipokuwa kwenye masuala yanahowahusu wazungu wenyewe kama Brexit ya sasa ndo twaona wanzungumzia uwingi wa wageni na kwamba wageni wasiruhusiwe waingie tena UK.
Pipa ninalolipendelea ni la Emirates na hiyo ni kwasababu ya entertainment.
Nnapenda hilo pipa kwa sababu mimi ni mpenzi wa shopping hivyo nikiwa Dubai basi ntahakikisha nanunua vitu kadhaa kwa ajili ya familia khasa ya nyumbani Tanga ambayo ndo ndogo.
Changamoto kubwa nilizopata khasa kupata vibali vya kuishi kwenye nchi zote hizo moja ni fedha za kulipia ili kuongeza muda wa viza.
Kwa mfano katika nchi za USA na Estonia niliingia kama skauti hivyo wakawa na kumbukumbu yangu na wakawa wamenipatia viza ya ILE yaani Indefinite Leave to Enter ya miaka 5 na baadae nikapata kibali cha kudumu.
Hata hivyo USA nimefanya kazi kidogo kule FEDEX (makao makuu Tennessee) na hiyo kazi ilinisaidia sana kufahamu barabara za huko.
Canada nilikuwa naenda kumtembelea rafiki yangu wa siku nyingi ambae baadae akanisaidia akaunti yangu ya benki iwe inatuna kila ninapoongeza muda.
Mwisho baada ya kukaa miaka mitatu wakanipa viza ya kudumu ambayo niliitumia kufanya kazi kwenye maduka kama lile alilokuwa kufanya Dr Slaa alipokuwa huko.
Baada ya mwaka 2007 kila nchi imebadilisha sheria zake za uhamiaji si USA, wala UK wala Canada na baadhi ya nchi za Scandinavian.
Hivyo ni kutokana na uwingi wa wageni kutoka nchi za Afrika, zile zenye migogoro kama Syria na wageni wengine magaidi.
Jambo kubwa na la msingi kabisa unapokuwa unakwenda kwenye hizo nchi ni kuhakikisha una fedha mkononi za kutosha.
Kumbuka penye udhia ni lazima upenyeze rupia.
Lakini pia yote hayo hutegemea na bahati ya mtu na afisa uhamiaji utakaemkuta siku waingizana irport ya kigeni.