Uzi maalumu: Kijiwe cha Soga kwa waliowahi na wanaoendelea kukaa nje ya Tanzania


Mimi nimeishi na kufanya kazi miji ya Toronto Canada, Tennessee USA, London UK na Talinn Estonia.

Nilianzai kusafiri nikiwa kijana mdogo wa skauti lakini nilipofika London nikatulia nikatafuta kazi (miaka ya mwanzo ya 90)

Nilianza kufanya kazi ya ulinzi kwenye hoteli maarufu iitwayo Strand iliyopo karibu kabisa na BBC Bush House London.

Hivyo mimi sasa hivi ni mtaalam wa CCTV, nafunga alarm systems na nipo level ya C yaani nimekuwa vetted kuingia maeneo nyeti na kupiga kazi bila kubughudhiwa.

Mwanzoni nimeishi na masela ya nchi mbalimbali Tanzania, Uganda, Kenya, Gambia, Ghana, Nigeria na Zimbabwe (UK twawaita wazimbabwe jina la "wazimzim")

Wasichana wa kizimbabwe na wakenya wanawapenda sana vijana wa Tanzania wanasema wanapenda kuwa nasi na upole wetu.

Mimi kabla ya kuoa nilikuwa na msichana mmoja aitwae Busiliwe namkumbuka sana huyu binti alivyokuwa akisonga ugali wa kizimbabwe uitwao Saza. Baadae alirudi kwao Zimbabwe na mpaka sasa huwa tunatupiana Hi.

Lakini mwanzoni mwa 2015 nilirudi Tanzania na nikaamua kuwa low profile na sasa ni mjasiriamali na nafanya shughuli zangu mwenyewe lakini nina familia kwenye moja ya nchi hizo tajwa hapo juu.

Nilipoishi na kufanya kazi UK ubaguzi upo lakini unapotea endapo unaonyesha kuwa unazo "skiils" na wazungu wanazihitaji.

Ubaguzi upo lakini ni vigumu kuona kwa macho yako isipokuwa kwenye masuala yanahowahusu wazungu wenyewe kama Brexit ya sasa ndo twaona wanzungumzia uwingi wa wageni na kwamba wageni wasiruhusiwe waingie tena UK.

Pipa ninalolipendelea ni la Emirates na hiyo ni kwasababu ya entertainment.

Nnapenda hilo pipa kwa sababu mimi ni mpenzi wa shopping hivyo nikiwa Dubai basi ntahakikisha nanunua vitu kadhaa kwa ajili ya familia khasa ya nyumbani Tanga ambayo ndo ndogo.

Changamoto kubwa nilizopata khasa kupata vibali vya kuishi kwenye nchi zote hizo moja ni fedha za kulipia ili kuongeza muda wa viza.

Kwa mfano katika nchi za USA na Estonia niliingia kama skauti hivyo wakawa na kumbukumbu yangu na wakawa wamenipatia viza ya ILE yaani Indefinite Leave to Enter ya miaka 5 na baadae nikapata kibali cha kudumu.

Hata hivyo USA nimefanya kazi kidogo kule FEDEX (makao makuu Tennessee) na hiyo kazi ilinisaidia sana kufahamu barabara za huko.

Canada nilikuwa naenda kumtembelea rafiki yangu wa siku nyingi ambae baadae akanisaidia akaunti yangu ya benki iwe inatuna kila ninapoongeza muda.

Mwisho baada ya kukaa miaka mitatu wakanipa viza ya kudumu ambayo niliitumia kufanya kazi kwenye maduka kama lile alilokuwa kufanya Dr Slaa alipokuwa huko.

Baada ya mwaka 2007 kila nchi imebadilisha sheria zake za uhamiaji si USA, wala UK wala Canada na baadhi ya nchi za Scandinavian.

Hivyo ni kutokana na uwingi wa wageni kutoka nchi za Afrika, zile zenye migogoro kama Syria na wageni wengine magaidi.

Jambo kubwa na la msingi kabisa unapokuwa unakwenda kwenye hizo nchi ni kuhakikisha una fedha mkononi za kutosha.

Kumbuka penye udhia ni lazima upenyeze rupia.

Lakini pia yote hayo hutegemea na bahati ya mtu na afisa uhamiaji utakaemkuta siku waingizana irport ya kigeni.
 
Mkuu imetisha kumbe hata mambo ya sasa ya CCTV unayajua hee
 
Dah mkuu Ritchie this really interesting. Estonia nilishafika Tallin old city Rakvere na Tartu. Nilitokea stockholms na Silja line hadi helsinki Finlend then nikapanda linda line speed boat ila abiria flan Estonian Russian aliniambia waliipunguza speed iende taratibu ni kama zenji na Dar. Aliniambia speed ya kawaida ingekuwepo ingechukua nusu saa tu. Pia aliniambia kuna kipindi helikopta zilikuwa zinabeba watu ikapata ajali wakasitisha

Nilimfuata demu Tallin baada ya kukutana kwenye dating sites ni red head ila kashehen mzigo mzito nyuma. Alikuwa anaishi kwenye apartments flan karibu na Prisma supermarket high way ya kwenda Rakvere.
Ila tulishindwana. Naona sasa hivi yuko na niga mwengine na watoto wawili.

Pia nilifika hadi Riga. Nilipokuwa narudi nilikutana na msomali flani ana uraia finlend ila kiswahili kinapanda. Aliniambia alisoma Estonia miaka ya late 80s wakaamia Finlend early 90s na wasomali wengine ndio walikuwa wasomali wakwanzakwanza
 
Kumbe wewe chizi fresh lb7 una kadiploma hahhahahah kichwa maji kabisa
 
Ulikua Na miaka mingap? Pia eliku yako je?
 

Nillingia huko nikitokea Sweden nilikokuwa nimeenda na Tatu Nane original miaka hiyoo na nikaamua kukaa kidogo na rafiki yangu wa kike ambae kwa asili anatokea Finland.

NImeishi mji uitwao Pirita nje kidogo ya Talinn.

Ni nchi tulivu sana na raisi wao ni mwanamke na waziri mkuu mwanamme.

Raha ya nchi hii ni kwamba ukipata makazi ya kudumu basi huduma za matibabu ni bure na kwa raia wote, na elimu ni bure.

Ni nchi ya kwanza duniani kufanya uchaguzi kupitia internet na ni nchi ya kwanza duniani kwa kutoa kibali cha makazi kiitwacho e-residency kwa raia wa kigeni.

Hiyo e-residency unaoewa kadi maalum ambayo watumia kwa kila kitu, kulipia kodi kufungua kampuni na hata masuala ya kibenki mtandaoni.
 
juz hapa nilikuw Melbourne
kama nimefk Australia ni nchi gan nitashindwa,
Yap ukiwa na passport ya EU ama Norway Switzerlend lietchtestein kokote duniani unaingia bila visa. Australia unaweza ukafanya kazi na ikaishi two years nakuomba permanent residence.

Ila passport hizi bado zinautata za Romania Bulgaria na croatia lazima maswali mengi utaulizwa licha ya wa wao kuwa EU kuna procedure flan inabidi wafuate
 
Riga Latvia ushafika? Ila natamani sana tena kwa sana kufika kwa bibi has kutokea paris kupitia chini ya maji kwenye ile tunnel.
Natamani sana yani hadi skotlend kwenye yale macastle
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…