Mkuu uliwezaje kusoma litabu hili lenye kurasa 1000 ndani ya siku 3 ?1. Ni kizuri.
2. Kina kurasa nyingi. Lazima uwe umedhamiria ndiyo utaweza kukimaliza. Nakumbuka nilipokipata kwa mara ya kwanza (hard copy), niliahirisha karibia kila kitu isipokuwa kula nikakimaliza kukisoma ndani ya masaa 48.
Ni siku nyingi hata hivyo, 2009.Mkuu uliwezaje kusoma litabu hili lenye kurasa 1000 ndani ya siku 3 ?
Kwani hili ni jukwaa la Uchumi? wewe mwenyewe umefanya nini kuhusu kuporomoka kwa hiyo shillingi.Bonge moja la point ya Ki????? nge.Mkuu hii inasaidia vipi kuhusu kuporomoka kwa thamani ya shilingi yetu dhidi ya US dolar na sarafu nyingine za kigeni?
Mkuu natamani Sana kujua kingereza, lakini changamoto ni nyingi sana zinazo nirudisha nyuma, ikiwa changamoto kubwa ni mazingira ambayo naishi ni kiswahili tupu so hata ile language interaction haipo.Wilson Kaigarula alikuwa na column yake nafikiri Sunday News inaitwa "With A Light Touch".
Nilisema hiki Kiingereza piga ua galagaza ni lazima nikijue tu, hata kama nasoma kwa kuangalia kamusi pembeni, lakini sitaki anachoandika huyu bwana kinipite.
Nikakomaa naye mpaka nimekiweza kwa kiasi changu.
Ukiona Kiranga ana Kiingereza kigumu (kama wanavyosema wengine, ingawa ni cha kawaida sana)ujue safari ilianza muda mrefu tangu enzi za kusoma kina Wilson Kaigarula.
RIP.
Mambo mengi yapo online siku hizi, kuna Youtube channels nyingi za kujifunza lugha. Pia BBC wana podcasts za kujifunza Kiingereza, pia unaweza kuuliza British Council walikuwa na madarasa ya Kiingereza kama unataka interaction zaidi offline.Mkuu natamani Sana kujua kingereza, lakini changamoto ni nyingi sana zinazo nirudisha nyuma, ikiwa changamoto kubwa ni mazingira ambayo naishi ni kiswahili tupu so hata ile language interaction haipo.
Unaweza nisaidia Hits jinsi ya kufahamu hii lugha hata kusoma na Kuelewa!!
Natanguliza Shukurani 🙏