Uzi maalumu kuwaenzi Waandishi wakongwe kwa njia ya kuweka misemo au nukuu maarufu kupitia vitabu vyao

Uzi maalumu kuwaenzi Waandishi wakongwe kwa njia ya kuweka misemo au nukuu maarufu kupitia vitabu vyao

1. Ni kizuri.
2. Kina kurasa nyingi. Lazima uwe umedhamiria ndiyo utaweza kukimaliza. Nakumbuka nilipokipata kwa mara ya kwanza (hard copy), niliahirisha karibia kila kitu isipokuwa kula nikakimaliza kukisoma ndani ya masaa 48.
Mkuu uliwezaje kusoma litabu hili lenye kurasa 1000 ndani ya siku 3 ?
 
Mkuu uliwezaje kusoma litabu hili lenye kurasa 1000 ndani ya siku 3 ?
Ni siku nyingi hata hivyo, 2009.

Nilisitisha shughuli zingine zote isipokuwa kula, tena kiasi kidogo tu kuepuka kuchoka. Nilikuwa na hamu nacho kwa sababu nilikitafuta muda mrefu. Nilikuwa nikishinda ndani nikisoma. Usingizi ulienda likizo kwa muda.

Hata hivyo, hard copy haikuwa na kurasa nyingi kama soft copy, hard copy ilikuwa na kurasa chini ya 1,000 lakini zaidi ya 500.
 
Mkuu hii inasaidia vipi kuhusu kuporomoka kwa thamani ya shilingi yetu dhidi ya US dolar na sarafu nyingine za kigeni?
Kwani hili ni jukwaa la Uchumi? wewe mwenyewe umefanya nini kuhusu kuporomoka kwa hiyo shillingi.Bonge moja la point ya Ki????? nge.
Kila kitu na mahali pake na maudhui yake.Mtoa mada yuko sahihi watu wote hatuwezi kujadili uchumi wakati sio taaluma yetu.
 
,, Dunia uwanja wa fujo.Kuna fujo za aina nyingi kisiasa na kiimani.YESU alikuja na fujo zake kutuletea neno la MUNGU tuongoke.Waasisi wa Mataifa duniani walikuja na fujo zao hadi nchi zao kupata uhuru''............
E Kezilahabi RIP Mzee wa kitabu kingine kiliitwa Kaptura la Max ambacho kilikukimbiza nchini maana kiligusa utawala wa mtu flani
 
Wilson Kaigarula alikuwa na column yake nafikiri Sunday News inaitwa "With A Light Touch".

Nilisema hiki Kiingereza piga ua galagaza ni lazima nikijue tu, hata kama nasoma kwa kuangalia kamusi pembeni, lakini sitaki anachoandika huyu bwana kinipite.

Nikakomaa naye mpaka nimekiweza kwa kiasi changu.

Ukiona Kiranga ana Kiingereza kigumu (kama wanavyosema wengine, ingawa ni cha kawaida sana)ujue safari ilianza muda mrefu tangu enzi za kusoma kina Wilson Kaigarula.

RIP.

Mkuu natamani Sana kujua kingereza, lakini changamoto ni nyingi sana zinazo nirudisha nyuma, ikiwa changamoto kubwa ni mazingira ambayo naishi ni kiswahili tupu so hata ile language interaction haipo.

Unaweza nisaidia Hits jinsi ya kufahamu hii lugha hata kusoma na Kuelewa!!
Natanguliza Shukurani 🙏
 
Mkuu natamani Sana kujua kingereza, lakini changamoto ni nyingi sana zinazo nirudisha nyuma, ikiwa changamoto kubwa ni mazingira ambayo naishi ni kiswahili tupu so hata ile language interaction haipo.

Unaweza nisaidia Hits jinsi ya kufahamu hii lugha hata kusoma na Kuelewa!!
Natanguliza Shukurani 🙏
Mambo mengi yapo online siku hizi, kuna Youtube channels nyingi za kujifunza lugha. Pia BBC wana podcasts za kujifunza Kiingereza, pia unaweza kuuliza British Council walikuwa na madarasa ya Kiingereza kama unataka interaction zaidi offline.

Ona hapa.

 
Wanawake warembo ni sumu kubwa na hatari kwa maisha ya wanaume.. Kuwa makini sana unapokuwa mbele ya Mwanamke mrembo ..

Aristabulus Elvis Musiba..
Hapo alikuwa akimzungumzia mrembo Tausi.. Jina la kitabu nimelisahau..
 
^Ni rahisi kufanya mambo yawe magumu; ni ngumu kufanya mambo yawe rahisi. Tofauti katika haya mawili ni tofauti baina ya akili ndogo na akili kubwa.^ ~Mark Deverson.
 
^Most people are other people. Their thoughts are someone else's opinions, their lives a mimicry, their passion a quotation.^ ~Oscar Wilde
 
^If you are ever tempted to look for outside approval, realize that you have compromised your integrity. If you need a witness, be your own.^ ~Epictetus
 
^A high degree of unguarded intellect tends to make a man unsocial.^ ~adapted from Arthur Schopenhauer
 
Back
Top Bottom