SEHEMU YA KWANZA: MAHITAJI(TOOLS) YA KUWEZA KUFANIKISHA UUNDWAJI WA ANDROID APPS
Kuna programu kadhaa ambazo zinahitajika ili kuweza kuunda hizi apps, programu hizo ni kama zifuatazo.
1. kompyuta inapaswa iwe na JAVA Development kit (JDK),
Apps za android kwa asilimia kubwa huundwa kwa kutumia java hivyo ni vizuri ukapata SDK ya javaa ambayo ni latest kabisa, unaweza kuipata kwa kutumia link ifuatayo,
Java SE Development Kit 8 - Downloads
2. Android SDK ambayo imeambatanishwa na Android Studio IDE
Hizi tooks zipo kwa ajili ya platform(OS) tofauti tofauti, kwangu mimi nitakuwa natumia windows na si linux lakini ukitaka kwa upande wa linux pia zipo.
Android Studio ndio ambayo tutaitumia katika kuandika codes, hii ni IDE rasmi ya android kwani zamani Eclipse IDE ndio iliyokuwa inatumika.
links.
kwa ajili ya windows,
Download Android Studio and SDK Tools | Android Studio