Napenda sana vijana kama nyinyi wenye uthubutu ngoja nikushauri mawili matatu
Kwanini scan document app ikawa ni moja ya feature ya sharepal
Mfano let me give you an idea app yako iwe ni let's say tuiite Spacedrop iwe na mifumo ya
1) scan documents
2) file sharing
3) file store
4) file uploading
Ili kutengeneza value nashauri tengeneza prototype then tafuta co-founders wawili wazungu kutoka Marekani mmoja awe ni mwenye capability ya programing ya hali ya juu na pili awe ni mtaalamu wa cybersecurity
Ili aweze kutengeneza kitu kilicho bora
Kabla ya hapo wekeza kwanza kwenye Design UI na UX unaweza nunua Designs kutoka dribbble.com
Ukishanunua design ile inakuwa ni prototype yako sasa unatafuta programmer ambaye ni Experienced programmer akaitengeneza na mtaalamu wa cybersecurity akaifanyia integration na security
Tafuta pia watengenezaji wa website nzuri wakatengeneza website yako
Ingia clutch.co utaona kampuni kibao za Website design
Ofisi anza na kulipia virtual office na kampuni ya Regus ili uwe na business address
Kwa kuwa ni cloud mtapata hela kwenye kutoa space mfano mtu anaweza kutumia free space up to 100 GB then from 500 GB kwa makampuni iwe ni let's say $199 then from 1TB iwe ni $499
Sasa basi ili kutengeza value ni kwamba platform yenu iwe ni end to end encrypted file sharing hapo yule jamaa wa cybersecurity ana appear
Ukiwahakikishia kuwa files za watu zitakuwa stored kwa kutumia technology Ni rahisi kupata funds
Mkipata Active users 10,000 wa kwanza mnaanza ku rise finds up to $2M
Hapo valuation yenu inakuwa
Bongo utachelewa anza kufuatilia kusajili kampuni Marekani kupitia Delaware company
Ukishafanya hivyo denver Colorado ni very suitable kwa biashara yako ingia website ya
Denver, Boulder Startups & Tech Companies | Built In Colorado utapata mawili matatu kuhusu Denver
Kwakuwa watu wanatakiwa walipie kwa kutumia credit card ni vyema ukatumia Stripe katika kufanya malipo na Yes ili na uwe na stripe kwa kampuni ya Tanzania lazima utumie stripe atlas na lazima uwe na kampuni USA so ukitumia Delaware registration
Utapata vitu hivyo
So kwa kuanza anza kufanya yafuatayo
1) angalia mfumo wa sasa wa file sharing hasa kwa kampuni kama Drobbox, google drive ect na wewe angalia biashara ambayo itakuwa ni file solution kwanzia uploading, storage na sharing kwa kuwa mpinzani wa hizo kampuni
Usiogope kuhusu majina ya hayo makampuni Wawekezaji ndio watakuwa interested kujua una kipya kipi kuwapiku dropbox na google na hapo ndio chance yako
2) Fikiria Jina sahihi na lenye kuakisi mfano unaweza ita Vaultspace, Heaven space, etc
3) Tafuta Logo designer mzuri mcheck jamaa mmoja tweeter anaitwa Richstar @richstartz hayuko vibaya kwenye utengenezaji wa Logo
Logo iwe simple ambayo inaweza kutumika as icon kwenye app na ikajieleza
4) Andika vitu unavyotaka tafuta mtu akutengenezee UX/UI
5) Tafuta watu sasa wawili ambao ni wazungu from denver Colorado jisajili LinkedIn, tengeneza profile yako vizuri usifollow kila watu follows tu watu wanatakiwa kufanya nao kazi
6) Fanya videoconferencing na watu unaohisi mtakuwa ni owners ect waambie kuwa mtakuwa share holders
7) anza kufanya taratibu za registration USA kule ni usd 500 tu unapata registration
8)Lipa Virtual Regus Office denver Colorado Corona imesaidia sana watu wana work remotely popote duniani now so virtual office kwa kuanza inafaa
9) Anza kuitengeneza the platform
10) tafuta website designer kupitia clutch.co aifanyie design vizuri kwamba website itatoa taarifa kuwa nyinyi ni akina nani na link ya app kwa PC, Mobile na iOS
11) mtafute Gilsant Mlaseko akushauri namna bora ya kui push kwa soko la Marekani kupitia social media na maswala ya SEO
12) Angalia MVP inaendaje watu wangapi wanapakua platform, early customer feedback ikoje
13) Andaa business plan ya kuwaandikia Us based investor kuhusu wao kuwekeza kwenye biashara yenu kiwango cha chini
14) strength yenu iwe kwenye security ya sharing
Sikushauri ulenge soko la Tanzania na Africa so ni bora kwa kuanza na soko la USA na Ulaya
Ni bonge moja la Idea ila unatakiwa ukae chini kupiga bonge moja la plan