Uzi maalumu; Machine zinazotengenezwa hapa nchini

Ahsante sana kwa kujibu. Umejitahidi sana. Naona uko mechanical mno. Kwani huwezi kuwa na mashine imara na ikawa na finishing nzuri? Zipo za kijerumani. Jaribuni kutafuta finishing.
Nimefurahi kusikia kuna parazo. Hilo ni jambo jema sana. Watu siku hizi wanafanya fasheni kula dona. Ni hatari. Kuna sumu kuvu(aflatoxin)! Nasikia kuna unga wa sembe na dona tu. Sijasikia unga unaotokana na parazo. Unaitwaje? Huo ndio utakuwa unga sahihi na salama. Sembe ni ya hovyo kama ilivyo dona. Hiyo mashine ya parazo ifanyie marketing. Utaokoa sana wala ugali.
Una maana gani unaposema: sasa hilo ni hitaji la kila mtu! Sio kwamba labda lugha inakupiga chenga?
 
Mashine ya kukausha vitu mbalimbali kama dagaa mboga mboga
 
Vipi mashine za kuprocess gogo kuwa mbao? Zinazotumia petrol Mnaweza tengeneza, na gharama yake ipoje? Mashine iwe mobile ya kuvuta kama trailer ama caravan.
 
Mashine hii kwa wale wanaohitaji kusaga cocoa tunaitengeneza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…