La sensor ndilo lilikuwa swali lake. Lililotangulia nalo hukulijibu. Nadhani hujalielewa. Unakimbilia kuzungumzia uimara wa mashine zenu zenye finishing ya hovyo kabisa. Hilo nawe pia umekiri. Esthetics sifuri. Hamko serious! Ni jambo linalowezekana kwa watu makini. Linachangia kufukuza baadhi ya wateja watarajiwa!
Swali ambalo hukuelewa hili hapa. Ni muda mrefu sasa hizi mashine za kukoboa na kusaga zimebaki vilevile. Hakuna mabadiliko licha ya kukua kwa teknolojia. Tulianza na mashine za kusaga tu. Kuna jambo la hatari likatokea. Kulikabili ukaja mfumo wa kukoboa. Lengo si kupata unga mweupe. Wanaorudia dona kirahisi ni tatizo la nusu elimu. Leo sio mada yangu kwa Kijana Mpole.
Kwako ni hivi. Baada ya kukoboa unakuwa na mahindi ya makande/yaliyokobolewa na pumba. Tatizo ni kwamba kwenye pumba kuna mapepe, vumbi na kiini. Pumba haifai kwa chakula cha binadamu. Linganisha na kumenya yai ukatupa ganda na kiini cha yai. Unabaki na ile sehemu nyeupe tu. Sembe hiyo!
Licha ya kukua kwa teknolojia tumebaki na mashine zinazotoa sembe na pumba yenye kiini. Wapenzi wa dona wanarudia kiini. Hatari hawaioni na hawaijui. Kijana Mpole waokoe wasile na pumba. Kwenye pumba kuna hatari iliyokimbiwa kwa kukoboa. Wameirudia wajinga hao. Waokoe kwa kukoboa na kubakiza mahindi ya makande na kiini chake. Kuwepo tu ugomvi kati yako na wafuga mbuzi katoliki!