Nilipokuwa mahabusu Butimba mwaka 2018 niliugua Sana mapele hasa matakoni maana sikuwa na mtu yeyote wa kuniletea nguo gerezani, na nilipofungwa 28/6/2018 niliumia Sana pale hakimu amenihukumu miaka3 au faini ya Laki5 halafu nafika gerezani nataka kulipa faini ili niachiwe huru maaaskari magereza wakaniambia hati ya kifungo Haina faini, nililalamika Sanaa, maaaskari Butimba gereza wakachukia Sana wakaamua kunihamishia Gereza la Kilimo kitengule_kyaka, Kagera manamo tar 10/01/2019, hapo Kitengule nilitolewa kafara ya wafungwa majambazi kwani Maaaskari wa kikosi maalum Cha Magereza(K.M) walikuwa wananitembezea kipigo kisicho Cha kawaida kipindi nimefika. Fimbo za kumwaga mgongoni, kupigwa kichwani na kuumuka kichwa, kulazwa kwenye matope na kulala nayo ndani ya sell bila kuoga . Yote haya yalikuwa yanafanyika kwa mfungwa mmoja tu ambaye nimimi. Tena nikizihakiwa kwa jina la TICHA. Kitengule ukisema TICHA utaambiwa mateso yote niliyoyapata.
Maaaskari wengine walikashifu eti kanajiona kana degree lakini tumelichakaza li degree kwenye matope na TICHA kadharaulika gereza zima. Maneno ya fedheha yalinichoma Sana. Nawashukuru Maafisa was gereza wenye kuanzia Nyota moja na kuendelea waliamua kuniokoa akiwemo Dr. Andrew aliyeniweka Zahanati kufanya matibabu kàma ODEL akishirikiana na Mvungi ili kuninusuru vipigo vya Kila siku. Lakini pia Sttaff Sajenti Julius na Sajenti Sebastian wote wa Admission office, walinipa sapoti kubwa Sana ya kujifua kisheria ikiwemo kuandika Rufaa za wafungwa, maombi na viapo n.k na baadae nikipewa nafasi ya Unyampara hewa.ambayo kimsingi niliutumia Unyampara kuwaelimisha zaidi wafungwa na mahabusu maswala mbalimbali ya kimaisha na kijamii japonilipandikiziwa chili kwa manyampara wenzangu na hawakutaka kunisapoti zaidi waliogopa kupigwa au kutumbuliwa.