tpaul
JF-Expert Member
- Feb 3, 2008
- 24,225
- 22,632
Wakati Tanganyika ikiadhimisha sikukuu ya wakulima mnamo tarehe 08/08/2017, wakenya watakuwa wakipigana vikumbo kwenye mistari mirefu wakimchagua rais wao atakayewaongoza kwa kipindi kingine cha miaka 5 ijayo. Wagombea wawili wanaotarajia kuchuana vikali kwenye uchaguzi huu ni Rais anayemaliza muhura wake wa kwanza, Uhuru Kenyatta na mgombea wa muungano wa NASA, Agwambo Raila Amolo Odinga (mjaluo), ambaye safari hii anaungwa mkono na wakenya katika Kenya nzima bila kuzingatia ukabila. Wakati Uhuru (mkikuyu) na mgombea mwenza wake, Ruto (mkalenjin) wakijikita kwenye siasa za ukabila, Odinga ameazimia kuwaunganisha wakenya wote na kuachana na siasa za kikabila.
Uchaguzi uliopita ulishuhudia viongozi wakichaguliwa kwa misingi ya kikabila hivyo kupelekea mgawanyiko mkubwa miongoni mwa wakenya. Hii ilipelekea Uhuru ambaye anatoka kwenye kabila la wakikuyu katikati mwa Kenya akitumia kete ya kabila lake (Kikuyu is the largest single tribe in Kenya) na Ruto akitumia kete ya ukalenjini, kuibuka washindi na kuchaguliwa kuingia madarakani. Wakelenjini ni mkusanyiko wa makabila mengi ambayo yanakaa katika jimbo la Rift Valley, ambalo ni kubwa kuliko majimbo yote nchini Kenya).
Safari hii Raila na kundi lake wameacha siasa za ukabila na badala yake wamejikita kuwaunganisha wakenya wote bila kujali ukabila wao. Kura za maoni zilizopigwa hivi majuzi zimeonesha kwamba Odinga anaongoza kwa asilimia kubwa dhidi ya Kenyatta na kundi lake la kikabila.
Katika uchaguzi huu mimi natupia kete yangu kwa Agwambo Raila Amolo Odinga. Hii ni kwa sababu serikali ya Kenya chini ya Uhuru Kenyatta imeingia katika kashfa ya kihistoria kwa kumuua CHRIS MUSANDO , Mkurugenzi wa IT wa tume ya uchaguzi ya Kenya (IEBC). Wananchi wamechukizwa sana na kitendo hiki na wameapa kutowarudisha madarakani wauaji hawa. Je, wewe kete yako unaitupia kwa nani na kwa nini? Toa maonai yako hapa.