Uzi maalumu: Uchaguzi mkuu wa Kenya mwaka 2017

Kwani uhuru ameingia mwaka gani? Au uchafuzi uliopita ulifanyika mwaka gani?

Sent using Jamii Forums mobile app
Kulingana na Katiba,uchaguzi unafaa kufanyika baada ya miaka 5. Uchaguzi uliopita ulifaa kufanyika August 2012 Lakini mahakama ikaisongeza kwa miezi sita hadi March2013. Nimesahau sababu ya mahakama kufanya hivyo.Hii ni kumaanisha Uhuru Kenyatta amekaa uongozini kwa miaka minne na nusu.
 
Hakika Msando ameuliwa kwa sababu ya msimamo wake thabiti wa kutopindua matokeo kwa namna yoyote ile. Uhuru na Ruto wanahusika kwa 101%.
Je na kama the deadly Jimmy Wanjigi amehusika pengine wakihitaji wapate hizo codes ili ma hackers wapate access ya IEBC servers....hiki kifo kinaweza kua ni Nasa au Jubilee...
 
Kituo cha Kuhesabia Kura cha Upinzani Kenya (NASA) Chavamiwa

Ikiwa ni siku chache kabla ya uchaguzi mkuu kufanyika nchini Kenya, Muungano wa Upinzani (NASA) umeishutumu serikali kuwa imevamia moja ya vituo vyake vya kuhesabia kura kilichopo eneo la Westlands jijini Nairobi.

Msemaji wa NASA ameeleza kuwa wanaume waliokuwa wamefunika nyuso zao walivamia ofisi hiyo wakafanya uharibifu na kubeba kompyuta, simu za mkononi na vitabu.

Kwa upande wake, serikali ya nchi hiyo imesisitiza kuwa hakuna uvamizi uliofanyika, . Mgombea wa upinzani Raila Odinga amesema kuwa atakubali tu kushindwa ikiwa uchaguzi utakuwa wa haki.

Hivi karibuni, Rais wa Uhuru Kenyatta alikaririwa akisema ataheshimu matokeo ya uchaguzi huo wa siku ya Jumanne licha ya kila mmoja kusisitiza kuwa ataibuka mshindi.

Uchaguzi wa Kenya mara nyingi umekua ukikumbwa na ghasia. Zaidi ya watu 1000 waliuawa wakati wa ghasia za baada ya uchaguzi wa mwaka 2007.

Uchaguzi wa kenya ni miaka 5, sema uliopita ulisogezwa mbele sababu ya hiyo tallying yao ya kielectronic ilikuwa haijawa sawa na hata hivyo ilizimika tena kwenye kura zao. Ila uchaguzi ujao utakua 2022
 
Wakati Tanganyika ikiadhimisha sikukuu ya wakulima mnamo tarehe 08/08/2017, wakenya watakuwa wakipigana vikumbo kwenye mistari mirefu wakimchagua rais wao atakayewaongoza kwa kipindi kingine cha miaka 5 ijayo. Wagombea wawili wanaotarajia kuchuana vikali kwenye uchaguzi huu ni Rais anayemaliza muhura wake wa kwanza, Uhuru Kenyatta na mgombea wa muungano wa NASA, Agwambo Raila Amolo Odinga (mjaluo), ambaye safari hii anaungwa mkono na wakenya katika Kenya nzima bila kuzingatia ukabila. Wakati Uhuru (mkikuyu) na mgombea mwenza wake, Ruto (mkalenjin) wakijikita kwenye siasa za ukabila, Odinga ameazimia kuwaunganisha wakenya wote na kuachana na siasa za kikabila.

Uchaguzi uliopita ulishuhudia viongozi wakichaguliwa kwa misingi ya kikabila hivyo kupelekea mgawanyiko mkubwa miongoni mwa wakenya. Hii ilipelekea Uhuru ambaye anatoka kwenye kabila la wakikuyu katikati mwa Kenya akitumia kete ya kabila lake (Kikuyu is the largest single tribe in Kenya) na Ruto akitumia kete ya ukalenjini, kuibuka washindi na kuchaguliwa kuingia madarakani. Wakelenjini ni mkusanyiko wa makabila mengi ambayo yanakaa katika jimbo la Rift Valley, ambalo ni kubwa kuliko majimbo yote nchini Kenya).

Safari hii Raila na kundi lake wameacha siasa za ukabila na badala yake wamejikita kuwaunganisha wakenya wote bila kujali ukabila wao. Kura za maoni zilizopigwa hivi majuzi zimeonesha kwamba Odinga anaongoza kwa asilimia kubwa dhidi ya Kenyatta na kundi lake la kikabila.

Katika uchaguzi huu mimi natupia kete yangu kwa Agwambo Raila Amolo Odinga. Hii ni kwa sababu serikali ya Kenya chini ya Uhuru Kenyatta imeingia katika kashfa ya kihistoria kwa kumuua CHRIS MUSANDO , Mkurugenzi wa IT wa tume ya uchaguzi ya Kenya (IEBC). Wananchi wamechukizwa sana na kitendo hiki na wameapa kutowarudisha madarakani wauaji hawa. Je, wewe kete yako unaitupia kwa nani na kwa nini? Toa maonai yako hapa.
Agwambo huwa ndio mshindi mara zote lakini hufanyiwa zengwe na Wakikuyu,Wakikuyu wanahofia biashara zao na kupoteza nguvu za kiuchumi,pia Wakikuyu ndio wameshika sehemu nyeti za ulinzi na usalama,mimi naamini kama uchaguzi utakuwa wa haki(sitegemei) Agwambo atashinda lakini kwa hawa jamaa waliopo madarakani hivi sasa sidhani kama wataruhusu Agwambo ashinde,nadhani umeona kilichompata marehemu Msando,alidai kwamba safari hii hakuna kuvuruga system labda wakate kiganja chake,na jamaa kweli wamekata kiganja chake,na pia wamevamia na kuharibu kituo cha kuhesabia kura cha mlengo wa NASA,Amolo ni raisi wa Kenya ambaye hakai Ikulu.Ukimuuliza Mkikuyu kwanini hawezi kumchagua Amolo pamoja na UhuRuto kuonyesha kutowajali masikini pia kuongezeka kwa ufisadi ,utawasikia ah hatuwezi tu kumchagua Raila kisa ni Mjaluo.Kenya ukabila ni kama laana waliyolaaniwa nayo kizazi kwa kizazi
 
Hakika Msando ameuliwa kwa sababu ya msimamo wake thabiti wa kutopindua matokeo kwa namna yoyote ile. Uhuru na Ruto wanahusika kwa 101%.
Kama waliweza kuwazima mashahidi wa ICC na kushinda kesi kwa kukosa ushahidi sembuse Musando,kosa la Musando ni kujipiga kifua mbele ya halaiki ,lakini pia nadhani alijua kuwa atauawawa na ndio maana akaona atoe dukuduku lake kwani alikuwa ametishwa mara nyingi na hata alipotoa taarifa polisi,polisi hawakuchukua hatua zozote nadhani ndio maana jamaa akaamua kumwaga mboga hadharani
 
Mwenye kuanzisha mada ameleta kasumba fulani na kuegemea propaganda to reach his flawed and skewed conclusions.Uvumi huwezi kubadilika kuwa facts na giza haliwezi kushinda mwangaza jameni.
 
Agwambo huwa ndio mshindi mara zote lakini hufanyiwa zengwe na Wakikuyu,Wakikuyu wanahofia biashara zao na kupoteza nguvu za kiuchumi,pia Wakikuyu ndio wameshika sehemu nyeti za ulinzi na usalama,mimi naamini kama uchaguzi utakuwa wa haki(sitegemei) Agwambo atashinda lakini kwa hawa jamaa waliopo madarakani hivi sasa sidhani kama wataruhusu Agwambo ashinde,nadhani umeona kilichompata marehemu Msando,alidai kwamba safari hii hakuna kuvuruga system labda wakate kiganja chake,na jamaa kweli wamekata kiganja chake,na pia wamevamia na kuharibu kituo cha kuhesabia kura cha mlengo wa NASA,Amolo ni raisi wa Kenya ambaye hakai Ikulu.Ukimuuliza Mkikuyu kwanini hawezi kumchagua Amolo pamoja na UhuRuto kuonyesha kutowajali masikini pia kuongezeka kwa ufisadi ,utawasikia ah hatuwezi tu kumchagua Raila kisa ni Mjaluo.Kenya ukabila ni kama laana waliyolaaniwa nayo kizazi kwa kizazi
Kosa alilofanya mzee Odinga (marehemu) ni kumwachia mzee kenyata kushika urais wa nchi kisa alikua gerezani,ikumbukwe kuwa wakoloni walimkabidhi mzee Odinga nchi na yeye kamkabidhi nyang'au,hii dhambi itawatesa waluo daima.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wakati Tanganyika ikiadhimisha sikukuu ya wakulima mnamo tarehe 08/08/2017, wakenya watakuwa wakipigana vikumbo kwenye mistari mirefu wakimchagua rais wao atakayewaongoza kwa kipindi kingine cha miaka 5 ijayo. Wagombea wawili wanaotarajia kuchuana vikali kwenye uchaguzi huu ni Rais anayemaliza muhura wake wa kwanza, Uhuru Kenyatta na mgombea wa muungano wa NASA, Agwambo Raila Amolo Odinga (mjaluo), ambaye safari hii anaungwa mkono na wakenya katika Kenya nzima bila kuzingatia ukabila. Wakati Uhuru (mkikuyu) na mgombea mwenza wake, Ruto (mkalenjin) wakijikita kwenye siasa za ukabila, Odinga ameazimia kuwaunganisha wakenya wote na kuachana na siasa za kikabila.

Uchaguzi uliopita ulishuhudia viongozi wakichaguliwa kwa misingi ya kikabila hivyo kupelekea mgawanyiko mkubwa miongoni mwa wakenya. Hii ilipelekea Uhuru ambaye anatoka kwenye kabila la wakikuyu katikati mwa Kenya akitumia kete ya kabila lake (Kikuyu is the largest single tribe in Kenya) na Ruto akitumia kete ya ukalenjini, kuibuka washindi na kuchaguliwa kuingia madarakani. Wakelenjini ni mkusanyiko wa makabila mengi ambayo yanakaa katika jimbo la Rift Valley, ambalo ni kubwa kuliko majimbo yote nchini Kenya).

Safari hii Raila na kundi lake wameacha siasa za ukabila na badala yake wamejikita kuwaunganisha wakenya wote bila kujali ukabila wao. Kura za maoni zilizopigwa hivi majuzi zimeonesha kwamba Odinga anaongoza kwa asilimia kubwa dhidi ya Kenyatta na kundi lake la kikabila.

Katika uchaguzi huu mimi natupia kete yangu kwa Agwambo Raila Amolo Odinga. Hii ni kwa sababu serikali ya Kenya chini ya Uhuru Kenyatta imeingia katika kashfa ya kihistoria kwa kumuua CHRIS MUSANDO , Mkurugenzi wa IT wa tume ya uchaguzi ya Kenya (IEBC). Wananchi wamechukizwa sana na kitendo hiki na wameapa kutowarudisha madarakani wauaji hawa. Je, wewe kete yako unaitupia kwa nani na kwa nini? Toa maonai yako hapa.

Hapana, umeegemea tu upande mmoja kwenye huu uandishi wako.

Raila na chama chake pia ni mkusanyiko wa makabila kadhaa kama tu ya Uhuru ambayo pia ni mkusanyiko ya makabila kadhaa zaidi ya wakikuyu na wakalenjin.

Isitoshe, wote wamezidi kuwarai wapiga kura kutoka kila eneo mwa Kenya, hata kwenye yale maeneo ambapo kuna dhana haungwi mkono, mfano Raila amefanya kampeni kwwnye maeneo ya Uhuru na Uhuru kwenye maeneo ya Raila.

Kwahivo ndugu, ungejaribu kuwa balanced tu katika analysis yako badala ya kusemekana kuegemea upande moja katika uzi huu umeweka spesheli ati ni ya kuhusu uchaguzi mkuu wa Kenya.

Hii thread basi haifai kabisa.
 
Watz waombe sana Raila asishinde uchaguzi huu, urafiki wao na magful hautawai kuwa wa faida. Nawahakikishia kabla ya miaka tano ya RAO kuisha watakuwa wamekosana na itabidi sisi raia tukosane pia. Uhuru huwa hana ubaya na utashangaa akisharudi mambo ya NASA na tz atayasahau na uhusiano kati ya Kenya na Tz utarudi kuwa kama kawaida!
 
Back
Top Bottom