Uzi maalumu wa kujua gharama za ujenzi wa majengo mbalimbali

Englishman

New Member
Joined
Jul 13, 2018
Posts
2
Reaction score
2
Habari wadau,

Naomba msaada wa gharama za ujenzi wa nyumba ya vyumba 2(self), sitting room & kitchen.

maeneo ya Mwanza Busweru.

 
Habari wadau,

Naomba msaada wa gharama za ujenzi wa nyumba ya vyumba 2(self), sitting room & kitchen.

maeneo ya Mwanza Busweru.
Tuwasiliane PM nikupatie fundi mzuri ambaye hamtoshindwana
 
Habari wadau,

Naomba msaada wa gharama za ujenzi wa nyumba ya vyumba 2(self), sitting room & kitchen.

maeneo ya Mwanza Busweru.
Nicheki nikupe namba ya fundi yupo mwanza pia atakufanyia kwa bei nzuri
 
Wakuu naomba ushauri wenu au uchambuzi wenu wa kujua (roughly estimates) gharama za ujenzi wa nyumba ya vyumba vitatu yenye ifuatavyo (ukubwa wa 17 kwa 12)
1.master 1 na self 2
2.sitting room
3.dining room
4.jiko na store na public toilet
Gharama ya kwa ujumla (material +ufundi) kuanzia msingi,boma, kupaua, blundering hadi kuezeka bati la royal romantile la alaf, mashimo yachimbwe kabisa na grill ziwekwe. Kabla ya plasta na jamvi. Kwa ujumla itagharimu kama kiasi gani... Naomba msaada wenu kwa ujuzi wenu.. Yaani usiwe na upungufu wa kiasi gani??
 
Uko mkoa gani? ama wilaya gani? sikia nkuambie tukikupa estimates unaweza ukajiona hujengi, Anza na fundi wako na uanze kidogo kidogo!

kiuhalisia nyumba unayotaka angalau anza na 5m, Ila kufika mpaka uliposemea angalau 45m.
 
Uko mkoa gani? ama wilaya gani? sikia nkuambie tukikupa estimates unaweza ukajiona hujengi, Anza na fundi wako na uanze kidogo kidogo!

kiuhalisia nyumba unayotaka angalau anza na 5m, Ila kufika mpaka uliposemea angalau 45m.
Nipo dar-Goba, nataka nijue ili nisipigwe sana yaani nijue nachezea wapi.. Nimeamua kujenga ila nataka niwe na idea kidogo kuwa nitasimama wapi hadi wapi
 
Umejiminya Sana 30 million , bila stress 40-45 millions ,mziki upo kwenye finishing , unaweza itoroka nyumba Kwa mda
 
Habari Mkuu, nina fundi mzuri sana anajenga mpaka finishing zote anafanya. Kama ukimhitaji karibu nikuunganishe naye.
 
Naomba kujua gharama za ujenzi mpaka lenta.

Urefu 18m upana 14mita
vyumba vitatu, kimoja masta, seble choo public na stoo pemben ndogo, Dar es Salaam.
 
Ili tujue lazima tu:
1. Tuone mchoro
2. Unajenga wapi
3. Kiwanja tambalale au slope
4. Udongo mfinyanzi au kichanga nk.
 
mkuu kwa upande wangu hii nyumba ni kubwa sana ungeweza hata kutoa vyumba vinne vya kulala,bila shaka vyumba ni vikubwa na seble ni kubwa,sasa ngoja nikushauri , kama unapenda nyumba kubwa ni sawa endelea na hio ramani,ila kama sio mpenzi wa nyumba kubwa hakikisha wakati wa kuseti msingi unapunguza vipimo,kwa makadirio hapo andaa kama 15m kufikia lenta(inaweza kuzidi) ,kupaua kama utatumia bati kigae andaa 15 m ,ya kawaida migongo mipana inaweza kucheza 12m - 13m,All the best.
 
35 hadi 45M.

Nimeona site moja hadi sasa wanapaua na shimo la choo limefunikwa, tayari imegota 20M.

Kwa hiyo kuna kazi kibao hazijafanyika.
 
Kwa wale ambao Wana uzoefu wa ujenzi au kama ni mafundi

Naomba msaada wa kujua gharama za fundi kwenye msingi, kupandisha pagale na mwisho finishing, Kwa kila stage nijue gharama.

Nyumba ni yenye vyumba vinne.

Shukrani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…