Serikali ya Awamu ya Sita chini ya
Rais Samia Suluhu Hassan imeendelea kufanya uwekezaji na mageuzi makubwa katika sekta ya afya tangu alipoingia madarakani tarehe 19 Machi, 2021.
Uboreshaji huu umefanyika katika maeneo ya miradi ya maendeleo ikiwemo uboreshaji wa miundombinu ya kutolea huduma za afya , ujenzi na ukarabati wa Hospitali mpya za kanda, Hospitali za Rufaa za Mikoa, upatikanaji wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi, kuimarisha huduma za uchunguzi, kuimarisha huduma za mama na mtoto, kuendeleza na kuanzisha huduma za kibingwa na bobezi kama ifuatavyo;
1. Kuimarisha Miundombinu ya kutoa huduma za Afya
2. Kuimarisha huduma za Tiba za Dharura (EMDs), Wagonjwa Mahtuti na Wanaohitaji Uangalizi Maalumu (ICU)
3. Kuimarisha upatikanaji wa Dawa, VifaaTiba na Vitendanishi
4. Kuimarisha Huduma za Uchunguzi wa Magonjwa na Huduma za Uchunguzi wa Mionzi (Radiolojia)
5. Kuimarisha huduma za Afya ya Uzazi, Mama na Mtoto
6. Kuimarisha huduma za KIbingwa na Bobezi- kuanzisha huduma mpya za matibabu ya kibingwa
7. Kuimarisha Rasilimali Watu katika Afya- kusomesha Wataalam katika fani za Ubingwa
Mwelekeo wa Sekta
Kwa kuzingatia Dira ya Taifa ya Maendeleo, Mpango Mkakati wa Sekta ya Afya, Ilani ya Uchaguzi ya CCM, Serikali ya Awamu ya 6 itaendelea kufanya uwekezaji mkubwa kwenye sekta ya Afya kwa lengo la kuimarisha ubora wa huduma ili kufikia lengo la Afya kwa wote. Mwelekeo mkubwa utakuwa ni kuimarisha UBORA WA HUDUMA NA SIO BORA HUDUMA.