Uzi maalumu wa kupeana connection mbalimbali za biashara

Mkuu uko serious?? Mbona kama mchezo wa kuigiza huu?...kwamba asafirishe kuku toka mlimba huko aliko aje!! Utapata faida gan? Mbona magari mengi tu huko yanapita masemi??...kuku ukodi truck??..
Ulikuja ukayaona hayo masemi? Afu hakuna anayefanya biashara isiyo na faida sijaanza Leo hii shughuli na lengo langu sio kubeba kuku pekeyake acha ujuaji
 
Jmn kama kuna mtu anahitaji kusafirisha dagaa kutoka mwanza kwenda mikoa ya kanda ya Kaskazini na Dar es salaam naomba anichek mzigo natuma kwa bei poa. Yan tunaongea na nakuuzia bei kama hapa mwanza tu.

Mimi ni bingwa wa kutuma mizigo unaupokea ndani ya saa 48 toka utumapo pesa ya mzigo
 
Katika zurura zurura nilipita kijiji kimoja kinaitwa kalando kama sijakosea kijiji hiki kipo sumbawanga kama unaenda mpanda unaingia kushoto , kipo pembeni ya ziwa Tanganyika .

Huku kuna fursa lukuki ikiwemo mchele samaki na mbao , mizigo ni mingi sana ya kuja mjini ila magari ni yakusua sua . njia ni vumbi japo inapitika . mbali na usafiri huku kuna fursa saaaana kwa biashara tajwa hapo juu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nauza shamba Kiagei bwawani Morogoro lina ukubwa wa hekari tano (5) linafaa sana kwa kilimo. Hekari moja sh. 750,000/= kwa biashara zaidi nicheki PM.
 
Debe moja unauza kiasi gani kwa bei ya jumla na debe moja lina jumla ya kilogram ngapi.???
Mkuu mi ninachoelewa n kuwa debe lina sado ngapi. Make nauza kwa debe na sado sijawahi kupima kwa kili mkuu
 
Asante mkuu ngoja nifuatiliee, Nina mwenyeji Kule

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni kweli unayoyasema. Moja ya tatizo kifika mlimba ni barabara hasa kipindi cha masika huwaga ni utata ila treni inasaidia sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…