Uzi maalumu wa kupeana connection mbalimbali za biashara

Mwenye connection na biashara ya mafuta ya alizeti (ambayo hayaja chakachuliwa ) toka Dodoma , mi nipo Iringa mjini kwasasa . kama ataweza kutuma madumu ya mafuta toka Dodoma mbaka Iringa basi itakuwa poa zaidi .
 
Kwa Wakazi wa Dodoma Jiji, ni maeneo gani wanauza miche ya matunda mbalimbali? Hasa ile ya kisasa!
 
Kama kuna fundi sim humu anajua kucheza na software vzr naomba tuwasiliane make nataka kubali sim version kutoka 4.0.0 kwenda 6.0.1 sim ni Samsung Galaxy S3. Hilo faili la kubadilishia linaitwa CM13

Kama upo njoo tuyajenga nipo Mwanza lkn
 
Madini sana hizi fursa kwa freelancer
 
Mwenye connection na biashara ya mafuta ya alizeti (ambayo hayaja chakachuliwa ) toka Dodoma , mi nipo Iringa mjini kwasasa . kama ataweza kutuma madumu ya mafuta toka Dodoma mbaka Iringa basi itakuwa poa zaidi .

Unahitaji kiasi gani, kwa Dodoma (hasa Chemba na Kondoa) huu ndio msimu wa mavuno ya Alizeti, na kwasasa gunia ni 35,000/- mpaka 40,000/-. Gunia kwa kadirio la chini inatoa Lita 20 ukikoboa na kuchuja.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…