Uzi maalumu wa kupeana connection mbalimbali za biashara

Uzi maalumu wa kupeana connection mbalimbali za biashara

Kwa mahitaji ya mashamba(Kisarawe) na viwanja vya bei nafuu kabisa kwa Dar (Chanika) karibuni.
 
Kama kichwa cha habari kinavyo someka ningependa uzi huu uwe maalum kwa kupeana connection mbalimbali za biashara. Biashara bila connection unaweza fanya bila mafanikio, hivyo basi ni vizuri tupeane connection mbalimbali za biashara.

Uzi huu utumike kuwakutanisha watu mbalimbali katika biashara tofauti tofauti na mwisho wa siku kupeana connection za biashara kutokana na ombi la muhusika. Wapo watu mbalimbali katika dunia hii, wana mitaji mizuri tu lakini kutokana na kutokuwa na connection wametulia na mitaji yao. Hivyo basi uzi huu uwe msaada kwao.

Elezea unahitaji connection ipi katika biashara kisha subiri kupewa connection na wahusika katika biashara hiyo. Lengo ni kusaidiana na si vinginevyo. Tuweke roho mbaya pembeni kisha tuungane pamoja katika gurudumu la maendeleo.

Wadau karibuni katika uzi huu tupeane connection za biashara.
Natafuta connection ya biashara za nguo za mitumba za watoto
 
Nawapa connection ya kuuza wazo la biashara kupitia APP inatwa "BANGO". Pakua na post wazo lako la biashara upige bingo chaap.
 
Natafuta tenda ya ku supply mchele kwenye mashule na taasisi zingine mkoa wa Pwani na Dar es Salaam. Nina mpunga wa kutosha kukoboa na ku supply bila kufeli.

10% kwa mleta dili bei ikiwa nzuri hawezi kosa!
Hukopeshi mkuu mchele
 
Ninapenda nipewe connection ya biashara ya mazao ya chakula baada ya muda muafaka nije niyauze.
Natanguliza shukrani.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hongera sana kwa wazo zuri. Biashara ya nafaka au mazao ya vyakula visivyo haribika haraka ni biashara nzuri na ni mara chache kupata hasara kama utakuwa makini kufatilia masoko mbalimbali nje na ndani ya nchi.

Mimi nina uzoefu na biashara hiyo kuanzia inakopatikana hadi soko.

Mimi nipo dar es slaam tanzania.0652529926
 
Natafuta mtu anaeuza maziwa mtindi ya kienyeji kwa bei nzuri angalau shillingi 500-600 kwa lita moja. awe mkoa wowote ule ambao una mabasi ya kuja Dar.
contact 0687886600
Bei iko chini sana ukiweza kufika 2000/ltr tuwasiliane nipo Moshi
 
Back
Top Bottom