Uzi maalumu wa kupeana connection mbalimbali za biashara

Uzi maalumu wa kupeana connection mbalimbali za biashara

Wakuu naomba msaada wa connection au kujua bei za vitu vifuatavyo. (Nimetumwa kuuliza)

1. Mashine ya kupukuchua mahindi inayotumia mafuta.
2. Mashine ya kupiga mpunga inayotumia mafuta.
3. Mashine ya kupiga mtama,uwele,ulezi na alizeti inayotumia mafuta.
4. Bei ya ng'ombe wa Boran saizi zote (dume kubwa, jike na ndama)
5. Bei ya kukodi Fuso Tandam au scania ya tani26 toka Songea au Rukwa kuja Dar.
6. Bei ya mashine ya kukoboa mpunga ili uwe mchele za aina zote pia za kugrade mchele.
Upo wapi kiongozi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kama bado hujapata mkuu karibu mufindi bei ni kama ifuatavyo 2×2=500 2×4=2800 2×6=3800 1×8=5000 1×10=7000 hizi ndizo zenye uhitaji sana huko dar,dom,mwanza,maswa,bariadi nk
Nachukia sana haya matangazo yanayokosa maelezo ya kutosha lkn kibaya zaidi hakuna mawasiliano utadhan Tanzania nzima ni yeye tu ndo anauza mbao. Biashara ni ushindani tujitahidi kuweka kila maelezo yatakayo mfanya mteja mtarajiwa apige simu kuuliza vitu vichache sana au kumaliza biashara yenyewe.
Sasa leo nilikua na kazi ya dharura ya mbao ujazo wa semi, nikaikumbuka hii post na fasta nikaingia humu ndani kucheki hakuna mawasiliano SO NIMEKOSA KAZI NA WEWE UMEKOSA KAZI imeenda kwa wengine. Mnatufanya wateja tuwe na kazi ya ziada eti na mawasiliano nayo tuyatafute!!! Binafsi tangazo likikosa chochote kati ya maelezo kuhusiana na bidhaa yenyewe, picha(INATEGEMEA), bei elekezi, na mawasiliano uwanalipitia mbali KABISA sina sababu ya kupoteza muda kuvitafuta vitu au taarifa muhimu ambazo lazima ziwepo na kimsingi hizo ndo siraha katika biashara ya KUUZIANA NA KUNUNULIANA (By Mzee wetu ALI HASSAN MWINYI).
Kama wewe ni mfanya biashara, unatangaza bidhaa zako lengo unataka tukujue ili tununue kwahiyo lazima mawasiliano yawepo, kwanini usiweke/ufiche?
Kutokuweka mawasiliano katika biashara yako ni dalili za kutojihamini, au ukiamini unachokiuza na inawezekana umesahahu bahati mbaya!!!! Teh, bahati mbaya!!
Nakushauri rekebisha tangazo lako kwa kuongeza hizo taarifa muhimu-MAWASILIANO
 
Chia seed inatumika vp?
Hutumika kama tiba lishe ya magonjwa mengi kama kisukari, presha, amoeba, typhod sugu, na magonjwa mengineyo mengi pia inaongeza kinga ya mwili, ina balance uzito wa mwili... Ninauza 1kg kwa tsh 7,000 tu kwa jumla, pia rejareja nauza 6,000 tu. Mwenye uhitaji nicheki PM, zinapatikana Mwanza.
 
Katika zurura zurura nilipita kijiji kimoja kinaitwa kalando kama sijakosea kijiji hiki kipo sumbawanga kama unaenda mpanda unaingia kushoto , kipo pembeni ya ziwa Tanganyika .

Huku kuna fursa lukuki ikiwemo mchele samaki na mbao , mizigo ni mingi sana ya kuja mjini ila magari ni yakusua sua . njia ni vumbi japo inapitika . mbali na usafiri huku kuna fursa saaaana kwa biashara tajwa hapo juu

Sent using Jamii Forums mobile app
Kuna magari pale shinyanga mjini ya kwenda huko?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Inategemea na kipindi bei inakuwa ndogo kipindi cha mavuno na kupanda paka kipind ni adimu mwez wa 5/6 mavuno yanachanganya bei huwa 750/800 unapanda miez ya 10 Ila haizid 1200 hiyo ilikuwa 2015 kuna mzee wangu namfahamu anastoo na mashine hapo hyo bei ni kwa kg mchele swaf
Mkuu samahani naweza kupata mawasiliano ya huyo mzee mwenye stoo na mashine ya mchele nimcheki tufanye biashara.
 
Naam bila shaka, funguka zaidi kuhusu hapo mpakani ili watu tuchangamkie fursa.
Chief niliwakilisha kama swali kwa wajuvi wa mambo kwani nami nina kiu kujua nini ambacho kinahitajika kwa wakati huu niichangamkie fursa , kama ushawahi kutembelea mipakani kuna wazee wa bodaboda wanapita njia za panya biashara inafanyika kama kawaida , wewe inakupasa tu kujua nn cha kupeleka na wakati gan
 
Back
Top Bottom