Uzi maalumu wa kupeana connection mbalimbali za biashara

Uzi maalumu wa kupeana connection mbalimbali za biashara

Nachukia sana haya matangazo yanayokosa maelezo ya kutosha lkn kibaya zaidi hakuna mawasiliano utadhan Tanzania nzima ni yeye tu ndo anauza mbao. Biashara ni ushindani tujitahidi kuweka kila maelezo yatakayo mfanya mteja mtarajiwa apige simu kuuliza vitu vichache sana au kumaliza biashara yenyewe.
Sasa leo nilikua na kazi ya dharura ya mbao ujazo wa semi, nikaikumbuka hii post na fasta nikaingia humu ndani kucheki hakuna mawasiliano SO NIMEKOSA KAZI NA WEWE UMEKOSA KAZI imeenda kwa wengine. Mnatufanya wateja tuwe na kazi ya ziada eti na mawasiliano nayo tuyatafute!!! Binafsi tangazo likikosa chochote kati ya maelezo kuhusiana na bidhaa yenyewe, picha(INATEGEMEA), bei elekezi, na mawasiliano uwanalipitia mbali KABISA sina sababu ya kupoteza muda kuvitafuta vitu au taarifa muhimu ambazo lazima ziwepo na kimsingi hizo ndo siraha katika biashara ya KUUZIANA NA KUNUNULIANA (By Mzee wetu ALI HASSAN MWINYI).
Kama wewe ni mfanya biashara, unatangaza bidhaa zako lengo unataka tukujue ili tununue kwahiyo lazima mawasiliano yawepo, kwanini usiweke/ufiche?
Kutokuweka mawasiliano katika biashara yako ni dalili za kutojihamini, au ukiamini unachokiuza na inawezekana umesahahu bahati mbaya!!!! Teh, bahati mbaya!!
Nakushauri rekebisha tangazo lako kwa kuongeza hizo taarifa muhimu-MAWASILIANO
Umeongea kwa uchungu kweli,pole !

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jeki ya gari na drill yake ya kufungulia Tyres inatumia umeme wa gari mpya bei 250000
IMG-20200512-WA0030.jpg
IMG-20200512-WA0029.jpg
IMG-20200512-WA0027.jpg
IMG-20200512-WA0028.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyo ni dalali kama mimi hapa,hauna haja ya kibishana naye.
Madalali tunanunua kuku mikoani ukitaka. tunakuuzia 15,000/= mpaka 20,000/= hizo ndio kazi zetu boss.
Nawewe unazingua hakuna kuku wa kienyeji mkubwa kwa bei ya 5000/- hapa Dar, iwe reja reja au jumla.
Hata ukitaka kuku 1000 kwa siku hupati kwa hiyo bei. Labda kama unataka bado wadogo (siyo vifaranga) wa kwenda kufuga
Heshimuni biashara za watu.

Na yule mdau naye bei zake ni za reja reja hazifanani na bei ya jumla.
Kama vipi msichafue uzi mzuri kwa post zenu za bei zisizo na uhalisia.
 
Mashine ya kupukuchua mahindiView attachment 1391300

Sent using Jamii Forums mobile app
I smell something fishy!
Tangazo limetag hadi marehemu na wasnii maarufu au ndiyo mbinu za kupata waonaji wengi?

Pili habari za mzigo kufikia zanzibar zinatia walakini flani, kuna watu wametapeliwa kwa stori za mzigo toka nje kuja Dar unashukia zanzibar, tena na hiyo habari ya advance labda uoneshe certificate za TRA za ku-clear tax na usajiri wa BRELA wa kampuni ya hao wauzaji.

Sorry sina nia ya kuharibu tangazo ila tunasaidiana tu hapa kusitokee vilio vya watu kulizwa na walaghai.
 
Mimi nmepata ideas, nme note down nategea siku Mungu akifungua milango akaleta baraka zake nijiingize rasmi ktk kujiajiri.. one day yes #TheMarathonContinues [emoji120][emoji469]
Huu uzi ni mzuri sana kwa sisi vijana tunaohangaika kila siku kutafuta fursa za maisha,sibanduki hapa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom