Tukiwa tunaelekea Ukingoni mwa Ligi kuu Tanzania Bara, Dirisha La Usajiri linatagemea Kufungulia Mwezi Juni Kuanzia Tarehe 14. Dirisha la Usajiri litaenda Hadi Msimu wa Ligi kuu Utakapo Tarajia Kuanza.
Club Tayari zimeanza kuachana na Wachezaji pamoja na Makocha Wao…. Hatua Inayo toa Mwanga kwa Wachezaji kuanza kutafuta Timu na Makocha kuanza kutafuta Timu za Kufundisha.
Tayari Simba Imeachana na Pablo Franco Martin kocha wao mkuu na sasa timu ipo chini ya Kocha Msaidizi.
Yanga wamesha Achana na Mchezaji wao Saido Ntibanzokiza na sasa yupo huru.
Tuwe kwenye huu Uzi kwa Tetesi na Taarifa kamili za Usajiri wa Timu za Ligi kuu Tanzania Bara. Kuweza kupeana Taarifa Zilizo na Zisizo Rasmi.
NB: Huu Uzi ni Kwaajiri ya Timu za Tanzania, wachezaji wanaondoka Tanzania Na Kujiunga pia na Timu za Tanzania Zitakazo shiriki Ligi Kuu Msimu Ujao.