Uzi maalumu wa kuweka tetesi na Taarifa za usajili Ligi Kuu ya NBC kwa msimu ujao 2022/2023

Uzi maalumu wa kuweka tetesi na Taarifa za usajili Ligi Kuu ya NBC kwa msimu ujao 2022/2023

Beki katili Nathan Fasika Idumba kwenye rada za Simba

View attachment 2251820

INAELEZWA kuwa, Rais wa Heshima wa Simba, ambaye pia ni mwekezaji wa klabu hiyo, Mohamed Dewji ‘Mo’, ameingilia usajili wa beki wa kati wa Cape Town City ya Afrika Kusini, Nathan Fasika Idumba.

Idumba raia wa DR Congo mwenye umri wa miaka 23, alijiunga na Cape Town City FC Julai 16, 2021, akitokea FC Saint Eloi ya kwao DR Congo.

Beki huyo anatajwa kuja kuwa pacha wa Henock Inonga Baka katika eneo la ulinzi la Simba msimu ujao ambapo tayari wachezaji hao wameshawahi kucheza pamoja.

Chanzo chetu kutoka ndani ya Bodi ya Wakurugenzi ya Simba, kimeweka bayana kwamba: “Ukisikia msimu ujao tumejipanga kufanya usajili wa kutisha basi ni vema tukaelewana hivyo, maana tayari Mo, kashika usukani wa usajili na hapa ninapoongea tayari ameiita menejimenti ya mchezaji wa Cape Town City, Nathan Fasika Idumba ili kukamilisha dili.

“Kimsingi Mo ameamua kufanya mazungumzo na uongozi wa Bro Soccer Management, ambao unamsimamia Idumba, hii ni baada ya kukamilisha mazungumzo ya awali na uongozi wa Cape Town City.

“Bodi yetu imeweka mkazo zaidi kwa Idumba kwa kuwa ni moja ya mabeki bora kwa sasa, kama akitua hatakuwa na kazi kubwa ya kuzoeana na Inonga ambaye tayari alishawahi kucheza naye, wanajuana vizuri,” kilisema chanzo hicho

Chanzo : Globalpublishers
The 23-year-old DR Congo international has reportedly attracted interest from a number of European clubs

The agent of Cape Town City defender Nathan Idumba Fasika says the door has not been entirely shut for Mamelodi Sundowns to bid for the centre-back’s signature.

There have been reports of growing interest in the 23-year-old from Europe as his agent Faustino Mukandila thinks the chances of switching to a Premier Soccer League club are very slim.

While Mukandila says City chairman John Comitis might not be interested in listening to PSL clubs, the possibility of entertaining Sundowns has not been entirely ruled out, provided the Brazilians flex their financial muscles.

“I don’t think John would ever consider the PSL market now,” Mukandila told iDiski Times.

“Why would he improve other teams when now Cape Town City could be the second-best in the league this season, so I don’t think so. Unless Mamelodi Sundowns make a huge offer to John, it’s business at the end of the day but I don’t think it interests the club or Nathan.”

Sundowns are reportedly in the market for a centre-back following some inconsistent performances by their defenders this season as well as injuries.

With Fasika’s City contract having six more seasons left before it expires, it might be difficult to prize him away from the Citizens.

If Sundowns make a move, they might have to compete with Swiss giants FC Zurich as well as Russian side FC Akhmat Grozny who are said to be keeping tabs on the player although the move to Russia is highly unlikely due to their ongoing invasion of Ukraine.

“There’s a team in Portugal, Russia, Switzerland, Israel and Denmark. They are all serious since scouting the player,” added Mukandila.

“They know the chairman’s number but now it all depends on the money the club will ask. But I know John will never block a player from leaving, he sold Benni McCarthy, he sold Pienaar, he knows what he’s doing, he knows his job.”

Idumba’s profile has risen and he has become a regular in the DR Congo national team in their recent games.

He made 23 league appearances for City this season, starting 20 of them

source : Goal.com
 
Ili wachezaji wanaosajiliwa Simba nafasi za ushambuliaji wafanye vizuri, timu ihakikishe Bocco, Kagere, Chama na Chris wote wanaachwa.
Tofauti na hapo hakuna atakayetoboa maana misumari ya hao jamaa acha kabisa.
Hata hawa akina Mpole mtawakataa endapo hao akina Viboko wataendelea kusalia kikosini.
 
Ila mashabiki na viongozi wa yanga huwa washamba sana sijui shida nini.
Shida hii hapa
FB_IMG_1655579378566.jpg
 
Pamoja na timu kufanya sajili mbali mbali eti uzi hauna updates!!

Mleta amekimbia uzi
 
Uzi umetelekezwa.!!
1656915004146.png


BEKI wa Yanga ambao ni mabingwa wa Ligi Kuu Bara na Kombe la Shirikisho msimu wa 2021/22 ametua ndani ya kikosi cha Singida Big Stars.Yanga jana Julai 2 iliweza kukamilisha msimu kwa kutwaa Kombe la Shirikisho kwenye mchezo wa fainali dhidi ya Coastal Union kwa ushindi wa penalti 4-1 baada ya dk 120 kukamilika kwa kufungana mabao 3-3,Uwanja wa Sheikh Amri Abeid. Taarifa kutoka Singida Big Stars imeweka wazi kuwa:”

Tumefanikiwa kuinasa saini ya beki no 2 kutoka kwa mabingwa wa kihistoria nchini Tanzania Yanga. Godfrey amesaini mkataba wa miaka 2 kuitumikia timu yetu,”.Nyota huyo kwa msimu wa 2021/22 hakuwa chaguo la kwanza la Kocha Mkuu, Nasreddine Nai kutokana na uwepo wa Djuma Shaban ambaye alikuwa chaguo la kwanza
 
1656915121322.png


Azam wamuaga Kigonya

Tumefikia makubaliano ya pande mbili ya kuachana na aliyekuwa kipa wetu, Mathias Kigonya.

Mara baada ya kumalizika kwa msimu huu, Kigonya alikuwa amebakiza miezi sita kwenye mkataba wake na akatuomba anataka kuondoka kutafuta changamoto sehemu nyingine na tukafikia makubaliano ya kuachana.

Tunapenda kumshukuru Kigonya, kwa mchango wake alioutoa kwenye klabu yetu kwa kipindi chote tokea alipojiunga nasi Januari mwaka jana, akitokea Forest Rangers ya Zambia.
 
1656915204303.png


🚨 D O N E D E A L 🚨

Tumefanikiwa kunasa saini ya kiungo mshambuliaji, Cleophace Mkandala, kwa mkataba wa mwaka mmoja akitokea Dodoma Jiji.

Kiungo huyo aliyefanya vizuri msimu uliopita, amesaini mkataba mbele ya mmiliki wa timu, Yusuf Bakhresa na Ofisa Mtendaji Mkuu, Abdulkarim Amin ‘Popat’.

Mkandala, 21, ni mmoja wachezaji vijana wanaochipukia vizuri, amesaini mkataba huo wenye kipengele cha kuongeza ndani ya miezi sita na hiyo itatokana na kiwango atakachokionyesha.

Aidha mbali na kuicheza Dodoma Jiji, Mkandala pia amewahi kucheza kwa misimu mitatu ndani ya kikosi cha maafande wa Tanzania Prisons, 2018-2019 hadi 2020-2021.

Huo unakuwa usajili wetu wa kwanza kwa wachezaji wa ndani kuelekea msimu ujao, tukiwa tumewashawatangaza watatu wa kigeni, viungo washambuliaji, Kipre Junior na Tape Edinho, wanaotokea Ivory Coast.

Katika kuimarisha eneo la ulinzi, pia tumemnasa kiungo mkabaji kutoka Nigeria, Isah Ndala.
 
1656915371302.png


🚨 D O N E D E A L 🚨

Tumefanikiwa kunasa saini ya kiungo mkabaji kutoka Nigeria, Isah Ndala, tukiingia naye mkataba wa miaka miwili.

Ndala aliyekuwa akichezea Plateau ya Nigeria, amesaini mkataba mbele ya mmiliki wa timu, Yusuf Bakhresa na Afisa Mtendaji Mkuu, Abdulkarim Amin.

Kiungo huyo, mwenye umbo kubwa, sifa ya ukabaji na kupiga pasi, anakuja kuimarisha eneo la kiungo, ambapo Septemba mwaka huu atakuwa anatimiza umri wa miaka 20.

Aidha mbali na kucheza Plateau, Ndalla amepita pia katika timu ya Sevan ya Armenia na Nasarawa United ya Nigeria.

Huo unakuwa ni usajili wetu wa tatu kuelekea msimu ujao, baada ya jana kuwatangaza nyota wawili kutoka Ivory Coast, Kipre Junior na Tape Edinho.
 
1656915495346.png


🚨 D O N E D E A L 🚨

Tunayo furaha kuwataaarifu kuwa tumeinasa saini ya kiungo mshambuliaji kutoka Ivory Coast, Tape Edinho, kwa mkataba wa miaka mitatu.

Edinho tumemnunua kutoka timu ya ES Bafing ya kwao, ambapo mkataba huo utamfanya kuhudumu ndani ya viunga vya Azam Complex hadi mwaka 2025.
Nyota huyo mwenye uwezo mkubwa, amesaini mkataba huo mbele ya mmiliki wa timu hii, Yusuf Bakhresa na Afisa Mtendaji Mkuu, Abdulkarim Amin 'Popat'.

Mkali huyo amechaguliwa kwenye kikosi bora cha Ligi Kuu ya Ivory Coast (Ligue 1) msimu huu, kutokana na ubora wake wa kuhenyesha wachezaji wa timu pinzani.

Msimu uliomalizika, amefanikiwa kufunga jumla ya mabao matano na kuchangia pasi tisa zilizozaa mabao.
 
1656915720312.png


Augustine Okrah (28) signs two-year contract with Simbasctanzania 🇹🇿 and is expected in Dar es Salaam next week to complete the other details.

Ghana Premier League - 32 games, 14 goals, 4 assists

FA Cup - 5 games, 3 goals, 1 assist
 
Back
Top Bottom