Uzi maalumu wa Mashujaa wa ziwa Tanganyika, Mashujaa FC

Uzi maalumu wa Mashujaa wa ziwa Tanganyika, Mashujaa FC

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2009
Posts
76,107
Reaction score
160,001
Hii ndio timu pekee inayoshiriki ligivkuu kutoka mkoani Kigoma.
Mashujaa FC ni timu inayomilikiwa na Jeshi la Wananchi Tanzania JWTZ, na msimu huu 2023/2024 wamepanda daraja baada ya kuifunga timu ya soka ya Mbeya City Fc kwenye mechi zote mbili.

Mpaka sasa Mashujaa FC IMECHEZA mechi tatu, imeshinda mbili na imetoa sare moja.

Imekalia usukani
IMG-20230918-WA0033.jpg
 
Naomba utaratibu wa kupata jezi kwa tulio mikoa mingine nje ya Kigoma.

Hili dude baada ya kukamilisha preseason yao chini ya Lake Tanganyika, hakika hakuna atakayetoka salama pale Uwanjani kwao, vinginevyo mechi ikachezewe Mwandiga kwa Mwami Zitto.
 
Naombeni matokeo kwa wanaofuatilia mechi yetu leo
 
DROO….MASHUJAA FC 0vs GEITA GOLD FC WAMEWEZA KUZUIA KASI YETU YA MAPIGO NA MWENDO

Leo tumetoka bila kufunga goli Ktk Uwanja wetu wa lake Tanganyika baada ya kutoka Droo bila magoli Geita Gold fc Nina wapongeza Geita Gold kwa kuweza kuzuia Mapigo na Mwendo kupata Droo lake Tanganyika ni bahati kwao……

Nina toa shukrani za dhati kutoka moyoni kwa Wachezaji wa MASHUJAA FC kwa Mchezo Mzuri, Bechi la Ufundi, Viongozi wa mashujaa fc, Chama cha soka mkoa wa kigoma(KFA) na kamati ya hamasa kwa kazi kubwa maandalizi ya mechi yetu tumecheza Mpira mzuri tumekosa bahati ya kushinda tumetemgeneza nafasi nyingi ninaamini kocha atafanyia kazi mapungufu.

Ninatoa shukrani kwa Wadau wa Mpira na Waandishi wa habari kwa kuitangaza timu yetu Morari ya mashabiki kushangilia Muda wote wakati mpira unachezwa Unaona rahaaa.

Nawatakiwa hamasa njema.


Hamasa mashujaa Fc.
21/08/2023
 
Wiki ijayo nitaweka makala maalumu ya historia ya kuanzishwa kwa timu ya mashujaa na kila kitu kuhusu timu yetu pendwa ya Mashujaa wa lake tanganyika

Nipo kwenye mchakato wa kuomba ruhusa hiyo kutoka kitengo husika
 
mechi ya jana imemalizima na alhamdulil laah tumepata point 1. si haba[emoji1317][emoji1317]
Focus yetu sasa ni kujiandaa kikamilifu kuelekea Game ya Ihefu ambayo sina shaka tutafanya vzr[emoji1317][emoji1317]
ukiachia mbali maswala ya timu na mchezo. Je ni changamoto zipi ambazo washabiki wetu mlikutana nazo ili tuweze kuzipresent zifanyiwe kazi mchezo ujao??

tunawapenda na kuwajali washabiki wetu hivyo kama kuna changamoto mlikutana nazo vema mtujuze. tunataka mechi ya Ihefu umati wa washabiki uwe mkubwa sana. point 3 zitatufanya tufikishe point 7 ambazo bado zitakuwa zimetuweka nafasi za juu
 
Back
Top Bottom