Uzi maalumu wa Mashujaa wa ziwa Tanganyika, Mashujaa FC

Ngoja niweke kambi hapa. Mashujaa tunaitaka CCL
 
Huu ni uzi wetu, maoni ya wadau Ni hazina yetu
 
Timu yetu inaongoza ligi kwa sasa, ikitokea ligi imesimama leo, kesho tutatangazwa mabingwa wapya 2023/24 😅😅
 
Hii ndio timu pekee inayoshiriki ligivkuu kutoka mkoani Kigoma.
Mashujaa FC ni timu inayomilikiwa na Jeshi la Wananchi Tanzania JWTZ, na msimu huu 2023/2024 wamepanda daraja baada ya kuifunga timu ya soka ya Mbeya City Fc kwenye mechi zote mbili.
Hongereni, mnaongoza ligi. Kazeni hapohapo
 
Mashujaa wa Lake Tanganyika Nyumbani.........nikiwa Buzebazeba Mtaa wa Sokoine Mechi tunaangalia kutokea juu ya miti inayozunguka Uwanja wa Lake T, hii huwa tunafanya kwenye mechi za wakuja Kama Simba na Yanga,Ila Chama la Wana Lake T....tunachangia getini.

Mashujaa wametuheshimisha Sana...tunazitaka timu za Kariakoo Sasa tuzioneshe rangi halisi ya wana Kigoma ndani ya Dimba la Lake T.
 
Timu ikiingia mtego wa Simba na Yanga umeisha hiyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…