Je ukihesabu ukapata 11 tafsiri yake inakuaje au unazijumlisha tena..?!Leo tunaendelea na majina ya namba zilizobaki tuone zikiwa kwenye mahusiano zinakuwaje. Majina ya watu Yana nguvu kubwa Sana katika mahusiano ya mtu na mtu, hivyo yanaweza yakapelekea watu wakawa kwenye mahusiano ya aina Fulani kulingana na namba za majina yao. Tunaangalia namba za majina kwa kutumia alfabeti za kiingereza A mpaka Z.
A, j na s Ni namba 1
B, k na t Ni namba 2
C, l na u Ni namba 3
D, m na v Ni namba 4
E, n na w Ni namba 5
F, o na x Ni namba 6
G, p na y Ni namba 7
H, q na z Ni namba 8
I na R ni namba 9
Mfano tunachukua jina la John na Fatuma tuone wakiwa kwenye mahusiano wataishi maisha gani.
J. O. H. N
1 +6 +8 +5=20
20=2+0=2
Jina la John Lina namba 2.
F. A. T. U. M. A
6+1+2+3+4 +1=17
17=1+7=8
Jina la Fatuma Lina namba 8.
Baada ya kupata namba za majina ya John na Fatuma, tunajumlisha namba zao 2+8=10, 10=1+0=1. Hivyo basi, mahusiano ya John na Fatuma yatakuwa Chini ya namba 1.
Sifa ya namba 1 Ni kujiongoza yenyewe, namba 1 Ni namba yenye ubinafsi. Hivyo basi, mahusiano ya John na Fatuma yatakuwa na ubinafsi ndani yake, kila mmoja atakuwa anaangalia upande wake. Lakini pia, kutakuwa na mabishano katika mahusiano yao, kwa sababu kila mmoja hatopenda kupelekeshwa na mwenzake. Mahusiano yao yatakuwa na majivunia ndani yake, kila mmoja atajiona Bora kwa mwenzake.
Ingekuwa namba 4, mahusiano yao yangekuwa kwenye wakati mgumu Sana. Namba 4 Ni namba ya upinzani. Hivyo kila mmoja angekuwa mpinzani kwa mwenzake, vurugu na kupigana ingekuwa Ni Jambo la kawaida. Lakini pia, katika mahusiano yao wangekuwa Wana panda na kushuka kwenye kipato chao.
Ingekuwa namba 5, mahusiano yao yangekuwa rahisi kuachana na kutengana. Mahusiano ya namba 5 yanaenda kwa kutumia akili nyingi. Jambo la kuachana na kurudiana Ni Jambo la kawaida kwenye mahusiano ya namba tano. Namba 5 inataka tuishi nao kwa akili, sio kuangalia hisia ya mtu. Uzuri wa namba 5 upo kwenye mahusiano ya kibiashara, Ni rahisi kufanikiwa, kwa sababu namba 5 Ni namba ya biashara.
Ingekuwa namba 7, mahusiano yao yangekuwa ya Siri au mmoja wapo angekuwa msiri kwa mwenzake. Siri zipo nyingi, inawezekana ikawa mmoja wapo anamficha mwenzake Kama ana biashara, nyumba, pesa au ana mwanamke au mwanaume wa pembeni. Angalizo, usije ukamuhesabia mume wa mtu au mke wa mtu alafu ikaja namba 7, utajiingiza kwenye matatizo, maana Cha mtu sumu.
Ingekuwa namba 8, John au Fatuma, mmoja wapo angechelewa kumpenda mwenzake. Hapa ingechukuwa muda mrefu mmoja wapo kumkubalia mwenzake kuingia kwenye mahusiano. Ila mahusiano yakianza kunakuwa na heshima kubwa Sana kwenye mahusiano, kila mmoja anamuheshimu mwenzake.
Namba zingine nilishazielezea huko nyuma, hivyo leo nilikuwa namalizia namba 1, 4, 5, 7 na namba 8. Watu wengi wametaka nizielezee namba zote, Nami nikaona Ni Bora nizimalizie.
By magical powerView attachment 2898420
Mbona darasa limejieleza vyema mkuuJe ukihesabu ukapata 11 tafsiri yake inakuaje au unazijumlisha tena..?!
Tafuta majani yanaitwa Murda yakaushe kisha yaweke kwenye karatasi fanya Kama unavuta sigara Moshi wake hii usaidia wavutaji wa aina zote na waleviWataalamu ninaomba formula au dawa ya mtu kuacha pombe .Nia yangu nikijua niitengeneze niwasaidie vijana wanaoumiza sana familia zao kwa ulevi.naambiwa ipo mitishamba ambayo mtu anaacha kabisa pombe.Tatizo hawa vijana ni hohe hahe hawana hela za kuona waganga wakubwa wapone .
Na dozi ikoje avute mara ngapTafuta majani yanaitwa Murda yakaushe kisha yaweke kwenye karatasi fanya Kama unavuta sigara Moshi wake hii usaidia wavutaji wa aina zote na walevi
Shukran sana mkuu. Na vipi kama umenenepa sana na unataka kupunguza mwili....Kama kuna mtu ana afya ya kusuasua, mwili uliokondeana, chukua matunda ya muegeya yakaushe kisha saga na tumie kama lishe kila siku kijiko kimoja cha chakula kwenye uji halafu njoo na majibu yetu hapa mkuu.
Ni kweli kabisa.Matunda ya mmea huu yana uwezo mkubwa sana wa kuongeza kinga ya mwili,ina maana automatically ni lazima uimarishe afya ya mtu aliyenyong'onyea.Kama kuna mtu ana afya ya kusuasua, mwili uliokondeana, chukua matunda ya muegeya yakaushe kisha saga na tumie kama lishe kila siku kijiko kimoja cha chakula kwenye uji halafu njoo na majibu yetu hapa mkuu.
Na kuhusu marijuana maelezo yake kidogoMti hii kwauku kwetu twauita kitodzo unakifanyaje,Aya mapenz haya hapa, Najina lengine mashona nguo au gusa unase au kiboko yamahabba wewe mwenye mumeo au mkeo unataka atulie asisikilize yoyote bila Rai yako au asimfikirie yoyote mwenza wako Zaid yako wewe chafunya chukua hivyo vimimba vinavyokamata nguo hivyo vikaange au viponde Kisha uo unga wake changanya na asali mbichi kidogo bakaaa kwenye dhakar wakat watendo lkn paka kwaumakini asikuone tumia mbinu zako mwenyewe nawewe dada nawe utapakaa kwenye uke wako vizur bc hiyo ndokiboko yalimbwata mkishafanya ilo tendo akili zake kuanzia siku hiyo atakuwa nakuwazatu wwe Nakama nimsichana au Unatabia zakutembea nawake zawatu usitumie hiyo dawa au watembea namwanaume zawatu usitumie kabisaa dawa hiyo nakuomba Sana ndugu yang nihatar Sanaa maana Kama mtu anamkewe atamuacha kwajili yako nakama mtu anamumewe nawewe umemfanyia hivyo ataachika,Chukua changanya na Asali mbichi kidogo pakaa kwandani kwenye uke wako Aya ingia kwenye tendo,Maana kunawatu wanaachika kilasiku limbwata Hilo hapo misinaga maficho sifichi kitu.
By magical power.View attachment 2901031
Unafuta Mara mbili kwa sikuNa dozi ikoje avute mara ngap
dawa ya kuacha pombe,sigara na madawaKwa wale wanaotumia sigara,bangi na madawa ya kulevya na wanahitaji KUACHA hii ndyo dawa mujarabu kwaNa dozi ikoje avute mara ngap
Hapa umefafanua vizuri umesaidia wengi.tunaomba umalizie na picha ya mmea huodawa ya kuacha pombe,sigara na madawaKwa wale wanaotumia sigara,bangi na madawa ya kulevya na wanahitaji KUACHA hii ndyo dawa mujarabu kwa
⚡wanywaji wa pombe
⚡Bhangi, sigara
⚡Mirungi , ugoro
⚡Na madawa mengine ya kulevya ukitaka KUACHA
🌹 Chukua dawa inayoitwa MURDA , chukua majani yake uyaanike yakauke
🌹Kisha chukua majani hayo na uyasokote kama sigara kisha vuta msokoto huo nusu asubui na nusu yake jioni , yaani kutwa mara mbili
🌹Dawa hiyo utayumia kwa siku tano tuu. Hakika hutotamani walakutimia tena vilevi vyako
🌹 Na dawa hii ilivyo mujarabu ukivuta mara ya kwanza tu hapo hapo jaribu kuvuta bhangi au sigara au kunywa Hakika utaona inakukera sanaa na ni mbaya