Mimi ni mtaalam siyo kama unavyofikri.Ninayo taaluma ya dawa za mimea kwa level ya chuo kikuu na nimesajiliwa na baraza la dawa la tiba asili na tiba mbadala linalosimamiwa na wizara ya afya.Kwa hiyo ninafahamu namna na majira ya uvunaji wa dawa,uandaaji wake na mpaka uhifadhi wake ili mmea uliovunwa uendelee kuhifadhi dawa iliyoko ndani yake.Si kila mmea tiba unaweza kuwa ni dawa,inategemeana na uandaaji wake maana unaweza kuharibu dawa wakati wa uandaaji wake.Mfano unaweza kutumia mlonge na usipate matokeo katika shida yako,kumbe unatumia makapi bila kujua nguvu yake ilishaisha kwa kukosea kanuni zake za uvunaji na uandaaji wake.
Kwa hiyo ndugu nilichoandika ninakijua!