Uzi maalumu wa Mimea Tiba inayotuzunguka majumbani

Uzi maalumu wa Mimea Tiba inayotuzunguka majumbani

FAHAMU KUHUSU FAIDA ZA MTI WA MUINGE AU MUEGEA KATIKA TIBA ZA ASILI

MTI huu una majina mengi wengine huita muegea, muinge mlemela na majina mengine. Mti hutumika sana kukuzia maumbile ila kuna utaalam maalum hutumika ila nitawapa faida kiafya

KWA AFYA KWA UJUMLA

Unatibu Tumbo Kujaa Gesi Kujisaidia Milendalenda Vidonda Vya Tumbo Kunawirisha Mwili Kwa Wale Wenye Afya Mgogoro ukurutu na magonjwa mengine ya ngozi.

Jinsi ya kutumia Kupata faida hizo kwa kutumia mizizi ya mti huo, chukua mizizi au magome yake na uyakaushe kivulini (sio juani), baada ya kukauka, saga magome hayo ili upate unga. Chota unga huo kiasi cha gramu 700 (karibu na robo tatu kilo), changanya na maji kiasi cha lita 6. Mwenye tatizo anatakiwa kunywa mchanganyiko huo kwa kiasi cha robo lita kila siku

Hifadhi kwenye fliji ili isiharibike ukhtaj kutumia waipasha moto kidogo.

kukausha vidonda chukua unga huo hunyunyuziwa katika nguo au kitambaa na kisha nguo au kitambaa hicho hufungwa katika kidonda au jereha na baada ya siku kadhaa jeraha hilo hukauka.

KWA MARADHI YA WATOTO WADOGO

kupata tiba ya nimonia na matatizo ya tumbo ikiwa ni pamoja na minyoo kwa watoto, magome ya mvunge huchukuliwa na kulowekwa kwenye maji kisha mtoto mwenye tatizo la tumbo hunywesha maji hayo. Aidha, unaweza kutumia mizizi kama mbadala wa magome kutibu nimonia.

KWA WANAWAKE KUONDOA MAJI NA KUONGEZA JOTO NA HAMU YA TENDO LA NDOA

tafuta maua ya mti huo, huchemshwa au kukaushwa na kusagwa kisha huchanganywa na maji. Baada ya kupata dawa hiyo, muhusika anaweza kuitumia kwa kunywa kwa kipimo cha robo lita na nyingine kujisafishia sehemu za siri ndani ya ck saba mfululizo

pia mti huu hutumika kukuza maumbile kwa kuchanjia km inavyoelezwa na wengine wengi na pia kwa kupakaa baada ya kuandaliwa kwa kuchukua mti huu na kuchanganywa na miti na mafuta mengine.....
hii miti pwani siioni kbsa ila upande wa nyumban mwanza ipo mingi tu
 
Bitter melon majani
Hutumika kufukiza majini
Tumia kumuogeshea mtoto asipatwe na nguvu za Giza
Yaweke kwenye maji..pigia deki kwenye nyumba au eneo la biashara kuondoa Giza lolote lile.
Tumia kuongea kusafisha mwili wako
Unaweza weka majani Kona za nyumba kuepusha ubaya wa nguvu za Giza
Weka Jani chini ya mto kukomesha wanga na majini wanaoattack usiku.

Matunda yake husaidia kueka level ya sukari kua sawa


1200px-Momordica_charantia_001.JPG
 
Ila mambo ni mengi unaambiwa wanyamwezi wanayodawa ukiwapa watoto wafupi wanakuwa warefu badae .pia waha wana majani wakilisha mbuzi au binadamu lazima azae mapacha
 
Jamani msaada wenu.

Ninasumbuliwa na kitu kooni ni kama kohozi limekwama hivi, ukimeza halimezeki, ukijikoholesha litoke halitoki hata ukijitapisha halitoki, yanatoka mate mazito kidogo ivi ila bado tu naskia bado lipo.

Kuna muda(mwezi au miezi) hua linapotea kabisa kuna muda linarudi.

Dawa nilizowahi kutumia:-

Amplicox
Metronidazole + Amoxilin + Omeprazole
Predinisolene (kama sijakosea spelling)
Vitamin B



Je nifanyeje?
 
Back
Top Bottom