Uzi maalumu wa Mimea Tiba inayotuzunguka majumbani

Uzi maalumu wa Mimea Tiba inayotuzunguka majumbani

Hii ni kila siku au mara moja tu? Utakuwa unafanya?
Si kila siku, ukiweka ni hadi pale utapohisi yale maji yamechafuka kwa vumbi ndo unaweza badilisha. Inaweza chukua hata baada ya mwezi.

Ni vyema ukaweka kwenye kona ili yakae kwa siku nyingi zaidi.
 
Ukitaka kufukuza negative energy nyumbani kwako.

Chukua chombo kilicho transparent (glass) jaza maji safi pia weka na chumvi ya mawe changanya na white vinegar then kiweke pale sebuleni kwako utakuja kunishukuru.

Shukrani mkuu
Je mwilini?
 
Shukrani mkuu
Je mwilini?
Mmmh kwa upande wa mwili hiyo experience sina mkuu hivyo siwezi kushauri kitu ambacho sijaki experience hii knowledge niliipata kwa wenzetu huko ndo sayansi huwa wanaitumia majumbani kwao.

Ila Chumvi ya mawe pekee inatosha kabisaa kuogea mwilini na ikaleta matokeo chanya kwa asilimia 💯.

Ila cha msingi zaidi ni kuwa na imani, tena imani kwa mwenyezi Mungu kupitia hizo vitu ameviumba yeye.
 
Wakuu naomba msaada;mke wangu ni mjamzito wa miezi mitano ila amepatwa na hali ya kukosa usingizi,pia kuota ndoto mbaya kama anakabwa na nini na zingine mbaya mbaya,yaan kiufupi malue malue tu...pia tumbo huwa linamuuma mda mwingi...wakuu naombeni msaada maana nakosa amani
N.B hii mimba yake ya pili means tuna mtoto mmoja tayri.
Tumia ubani maka na zukra ponda ponda mwagia kitandan kabla hajalala hii itampa nafuu kubwa.
 
Mkuu ningependa kujua faida na madhara ya mmea huu tafadhali.
 

Attachments

  • 335A9AAC-9983-4F7A-971A-9E00F6C47033.jpeg
    335A9AAC-9983-4F7A-971A-9E00F6C47033.jpeg
    1.4 MB · Views: 80
Msaada kwa anaejua aina ya dawa za mimea inayotibu uke mkavu plz msaada
Bamia.

Kata vipande vya bamia (bamia 3) kisha loweka kwenye nusu lita ya maji(usiku), tumia kwa siku 14 mfululizo (kila siku asubuhi).

NB: Unachuja kisha unakunywa maji yake (yanakua kama mlenda). Usiku unaandaa mpya.

Inasaidia pia kisukari, nguvu za kiume na madonda ya tumbo ( ukitumia siku 30 mfululizo)
 
Mmmh kwa upande wa mwili hiyo experience sina mkuu hivyo siwezi kushauri kitu ambacho sijaki experience hii knowledge niliipata kwa wenzetu huko ndo sayansi huwa wanaitumia majumbani kwao.

Ila Chumvi ya mawe pekee inatosha kabisaa kuogea mwilini na ikaleta matokeo chanya kwa asilimia [emoji817].

Ila cha msingi zaidi ni kuwa na imani, tena imani kwa mwenyezi Mungu kupitia hizo vitu ameviumba yeye.

Ahsante mkuu
 
Tiba ya miti shamba ni nini?

Huu ni utaalamu wa matibabu ya binadamu kwa kutumia mimea asilia inayopatikana sehemu mbalimbali. Asilimia 25 ya dawa zinazotengenezwa viwandani hutokana na mimea asilia.

Nchi zilizoendelea wataalamu wa matibabu haya wanasomea kabisa vyuoni na kupata degree za matibabu haya tofauti na hapa kwetu ambapo mtu yeyote anaweza akaibuka tu na kujiita daktari wa mitishamba, kwa mfano china kusomea udaktari huu wa mitishamba ni miaka mitano na mtu anayesomea lazima awe amaefaulu vizuri mtihani wa kidato cha sita.

Miaka ya hivi karibuni watu wengi hapa nchini tanzania na duniani kwa ujumla wamegeukia dawa hizi na kupenda kuzitumia kuliko zile za hospitali ambazo nyingi hutengenezwa kiwandani.

Dawa hizi zimekua zikipingwa sana na madaktari waliosomea elimu ya kisasa, yaani madaktari wa kawaida japokua dawa zao nyingi zimetoka kwenye mimea kama nilivyosema hapo mwanzo..mfano kwinini za malaria, digoxin za kutibu moyo na na dawa za aspirini za maumivu ni dawa zinazotokana na magome ya miti.

Leo ninaandika faida na hasara za dawa hizi ili mtumiaji atumie akijua kabisa anapata nini kutoka huko na nitaanza na faida zake kama ifuatavyo;

1.Dawa hizi hazina madhara madogo madogo wakati wa matumizi; mara nyingi dawa za viwandani zikitumika hua na madhara fulani fulani wakati wa matumizi kama kizunguzungu, kichefuchefu, kutapika na kadhalika lakini mitishamba watu wengi wameonyesha kuivumilia.

Ni mbadala wa dawa za hospitalini; baadhi ya magonjwa ambayo wataalamu hua wanashindwa kuyapatia ufumbuzi wa moja kwa moja kuna baadhi ya mitishamba imeweza kuyatuliza ama kuyatibu kabisa kama kuna dawa mbadala za presha, kisukari, pumu, kifafa na magonjwa mbalimbali yasiyotibika.

2. Zinapatikana kwa wingi sana; dawa hizi ziko sehemu nyingi sana hasa bara la afrika na asia, na kwa mtu anayefahamu anaweza kupanda hata miche kadhaa nyumbani kwake au shambani na kuzitumia pale anapopata tatizo, mfano kijijini unapata tatizo la jipu mzee anaangaza majani pembeni ya nyumba yameota yanapondwa pondwa unapakwa na jipu linapona kabisa hata bila kupasuka.

3. Bei yake ni ya chini; tofauti na dawa za hospitali ambazo ni gharama sana kwa baadhi ya matibabu ya magonjwa makubwa,dawa za mitishamba zinaweza kupatikana kwa gharama ya chini na mtu akatibiwa tatizo lake la kudumu.

4. Hutibu na kurudisha/kuweka kinga ya uhakika dhidi ya vimelea vya magonjwa.Tofauti na dawa za Antibiotics nyingi za viwandani ambazo zikitumika kwa muda mrefu hulizoea tatizo na kushindwa kutibu kwa uhakika linapojirudia.

Mfano magonjwa ya PID, fangasi sugu, UTI na magonjwa ya zinaa mara nyingi yanawatesa watu bila kupona kwa sababu wanaamini katika antibiotics za hospitalini kuliko mitishamba inayomaliza kabisa matatizo hayo bila kujirudia.

5. Chemikali zake hazina madhara makubwa katika uchujwaji wakati wa matumizi maana nyingi ni lishe kwa maana ya mizizi,magome na majani. Tofauti na antibiotics nyingi ambazo hubakiza sumu nyingi mwilini baada ya matumizi.

Pamoja na faida lukuki, kuna hasara za matumizi ya dawa hizi za mitishamba;

1. Hazifai kutumika kwa baadhi ya matibabu; kuna magonjwa mengi sana ya hatari ambayo dawa hizi haziwezi kutibu, magonjwa haya yanahitaji vipimo vya kisasa na matibabu ya kisasa ili kumpatia mgonjwa nafuu.

Kwa mfano mama aliyeshindwa kuzaa kwa kawaida lazima apasuliwe tu, mtaalamu wa mitishamba hawezi kufanya upasuaji wa aina yeyote, huwezi kuongeza damu wala kuongeza maji mwilini.

2. Dawa hizi hazina dozi inayo eleweka; kuna hatari kubwa sana ya mtu kutumia zaidi ya inavyotakiwa kwani waganga wengi wa kienyeji kila mtu ana dozi yake tofauti na hospitali ambapo kuna viwango vya aina moja dunia nzima.

Mfano watu huchemsha na kunywa mwarobaini lakini hawajui ni kiasi gani cha kunywa...wao wanajali kunywa tu. watu wengi hawajui kwamba dawa hizi pia zina kemikali pia kama dawa za hospitali na kemikali zile haziko viwandani ila ziko kwenye mti wenyewe unaotibu, gome la mti wa kwinini ni kemikali hatari sana.

3. Huingiliana na dawa za hospitali; ni vizuri kuacha mitishamba pale unapoamua kwenda hospitali au kuacha dawa za hospitali pale unapoamua kwenda kutibiwa na mganga wa miti shamba kwani dawa hizi huweza kuingiliana na kutengeneza sumu inayoweza kuua.

4. Kuuziwa vitu ambavyo si vyenyewe; tafiti nyingi zilizofanyika zilikuta chupa ya dawa ya mitishamba inayoandikwa kwamba ina dawa fulani ndani yake zilikutwa na dawa tofauti kabisa au unga ambao sio wenyewe. Mfano hapa kwetu unakuta mtu anakwambia ana dawa ya nguvu za kiume kumbe kachanganya na viagra jambo ambalo linaweza kuendelea kukuua kabisa nguvu zako.

5. Vifo vya kuepukika; waganga wengi wa kienyeji wanaotumia dawa hizi za kienyeji hasa hapa kwetu sio waaminifu na wakweli. Ukienda kwake na kansa inayoanza ambayo kimsingi ukiwahi hospitali inatibika atakuweka mpaka ufikie hali mbaya ndio akuache uende kufia hospitali.

Pamoja na mambo hayo yote bado mitishamba imeendelea kuonyesha suluhisho katika matatizo mengi ambayo kwa njia za kisasa yameweza kushindikana kabisa, mfano matatizo ya Nguvu za kiume, kuna matatizo ya tezi dume na nawasiri ambayo hosp mpaka ufanyiwe upasuaji lakini kwa mitishamba inaweza kutibiwa na ikaisha bila kadhia hiyo.

Matatizo ya uzazi kwa wanawake na mengine mengi. Jambo mhimu ni kuhakikisha kuwa unapoamua kutumia tiba ya mitishamba, hakikisha mtaalam wako ana uelewa wa kutosha juu ya taaluma hiyo na dawa zinaandaliwa katika mazingira bora kabisa.
 
Dawa kutoka kwa machikongwe 👴🏼 wa milima ya urugulu.

Kwa watu wa biashara chukua karafuu maua majani ya kitunguu swaum. Udi karaha maua ya uwaridi changanya pamoja. Choma kwenye biashara Yako Kwa mvuto.

. chukua karafuu maua mdalasini na chumvi mawe weka kwenye maji kaoge. Kwa ajili ya kufungua mwili wako na kuondoa mikosi

Kunywa karafuu maua na pilipili manga
Kwa kurudisha hamu ya tendo.
Tunapatikana morogoro mjinj
 

Attachments

  • FB_IMG_16738463592152190.jpg
    FB_IMG_16738463592152190.jpg
    41.6 KB · Views: 86
KUONDOA VIFUNGO MWILINI, AU MAMBO YAKIWA HAYAENDI, HATA KAMA UMEFUNGWA NA WACHAWI USIZAE, KUACHIKA BILA SABABU, USIOLEWE, USIPATE KAZI, USIPATE HELA, BIASHARA KUTOENDA VIZURI, UCHUKIWE HII INASAIDIA SANA.

CHUKUA MAJANI YA TEMBELE KAMA KWENYE PICHA, HATA YA KUNUNUA AU KUCHUMA MWENYEWE YANAFAA, WEKA NA MAJI YA KUTOSHA KWENYE SUFURIA, BANDIKA JIKONI. CHEMSHA MPAKA MAJI YAWE YA KIJANI, WEKA KWENYE CHUPA MENGINE UTUMIE SIKU 7 KAMA HUNA MUDA WA KUCHEMSHA KILA SIKU. CHUJA HAYO MAJI YA TEMBELE TU, NDO YANAHITAJIKA, NDO DAWA.
BAADA YA KUOGA NA SABUNI NA MAJI KAMA KAWAIDA, UNAWEKA HAYO MAJI YA TEMBELE KWENYE NDOO UNANUIA MAMBO YAKO KUFUNGUKA NA KUJIFUNGUA VIFUNGO ALAFU UNAJIMWAGIA.
FANYA SIKU SABA (7) MUDA WOWOTE. MLETE MREJESHO, MTAONA MAMBO YATAKAVYOANZA KUWA MAZURI.
Kalibuni morogoro mjini.
 

Attachments

  • FB_IMG_16738458388129894.jpg
    FB_IMG_16738458388129894.jpg
    61.1 KB · Views: 74
KUONDOA VIFUNGO MWILINI, AU MAMBO YAKIWA HAYAENDI, HATA KAMA UMEFUNGWA NA WACHAWI USIZAE, KUACHIKA BILA SABABU, USIOLEWE, USIPATE KAZI, USIPATE HELA, BIASHARA KUTOENDA VIZURI, UCHUKIWE HII INASAIDIA SANA.

CHUKUA MAJANI YA TEMBELE KAMA KWENYE PICHA, HATA YA KUNUNUA AU KUCHUMA MWENYEWE YANAFAA, WEKA NA MAJI YA KUTOSHA KWENYE SUFURIA, BANDIKA JIKONI. CHEMSHA MPAKA MAJI YAWE YA KIJANI, WEKA KWENYE CHUPA MENGINE UTUMIE SIKU 7 KAMA HUNA MUDA WA KUCHEMSHA KILA SIKU. CHUJA HAYO MAJI YA TEMBELE TU, NDO YANAHITAJIKA, NDO DAWA.
BAADA YA KUOGA NA SABUNI NA MAJI KAMA KAWAIDA, UNAWEKA HAYO MAJI YA TEMBELE KWENYE NDOO UNANUIA MAMBO YAKO KUFUNGUKA NA KUJIFUNGUA VIFUNGO ALAFU UNAJIMWAGIA.
FANYA SIKU SABA (7) MUDA WOWOTE. MLETE MREJESHO, MTAONA MAMBO YATAKAVYOANZA KUWA MAZURI.
Kalibuni morogoro mjini.
Tembele kwamba mambo yanateleza tu yenyewe...
 
Bitter melon majani
Hutumika kufukiza majini
Tumia kumuogeshea mtoto asipatwe na nguvu za Giza
Yaweke kwenye maji..pigia deki kwenye nyumba au eneo la biashara kuondoa Giza lolote lile.
Tumia kuongea kusafisha mwili wako
Unaweza weka majani Kona za nyumba kuepusha ubaya wa nguvu za Giza
Weka Jani chini ya mto kukomesha wanga na majini wanaoattack usiku.

Matunda yake husaidia kueka level ya sukari kua sawa


View attachment 2447446

Asante!
 
Kama kuna mwenye kujua dawa za asili za kufunga kizazi (mwanamke asishike ujauzito) atusaidie.

Haya madawa ya hospital sio rafiki kwa afya za wake zetu
Zina masharti mkuu ipo sio ya kunywa unafunga tuu kiunoni mpigi zake ila hakikisha zisidondoke zenyewe, inabidi uzifungue wewe kama wewe zikijidondokea hutazaa milele
 
Bitter melon majani
Hutumika kufukiza majini
Tumia kumuogeshea mtoto asipatwe na nguvu za Giza
Yaweke kwenye maji..pigia deki kwenye nyumba au eneo la biashara kuondoa Giza lolote lile.
Tumia kuongea kusafisha mwili wako
Unaweza weka majani Kona za nyumba kuepusha ubaya wa nguvu za Giza
Weka Jani chini ya mto kukomesha wanga na majini wanaoattack usiku.

Matunda yake husaidia kueka level ya sukari kua sawa


View attachment 2447446
Kumbe ni dawa mimi niliyakuta kwangu yameota mpaka juu ya bati nikayafeka yote aisee ujinga mzigo

Sent from my CPH1823 using JamiiForums mobile app
 
Niko na mtoto hapa wa rafiki yangu,kwa ninavyomuona ana daliki zote za kifafa.Katika familia yao upande wa baba kuna huougonjwa kwani hata baba yake mzazi na babake mdogo walisumbuliwa sana na kifafa.


Huyu mtoto ana miaka minne kasoro, kuna muda anakuwa kama kaduwaa kwa sekunde kama kumi na kumfanya apoteze umakini kwa jambo analolifanya,sasa mama yake akawa anahisi ni kiburi au kususa susa kwa watoto.Hali hii ni kama redio inayopoteza frequence kwa sekunde kisha kurejea tena.
Frequence zinaporejea mtoto anapata hali ya kustuka na kuacha kule kuzubaa na ni kama hajui nini kilitokea hapo awali. Naombeni msaada kama kuna shida yoyote ama dawa yoyote ya huu ugonjwa ili udhibitiwe mapema. Ahsanteni sana.
 
Back
Top Bottom