Uzi maalumu wa Mimea Tiba inayotuzunguka majumbani

Uzi maalumu wa Mimea Tiba inayotuzunguka majumbani

anaejua dawa ya mtishamba/kienyeji ya kuua au kufukuza popo ndani ya nyumba asaidie hapa[emoji1672]
 
Kama kuna mtu ana afya ya kusuasua, mwili uliokondeana, chukua matunda ya muegeya yakaushe kisha saga na tumie kama lishe kila siku kijiko kimoja cha chakula kwenye uji halafu njoo na majibu yetu hapa mkuu.

Huo mmea ukoje,msaada kwapicha kuna dogo hata ale vipi haongezeki uzito.
 
Ninamshukuru Mungu kwa kuendelea kunitunuku pumzi ya uhai ambayo hakika ni kwa neema tu. Kwa sababu hiyo ninafurahi pia kushirikiana nanyi wanajukwaa kubadilishana maarifa bure kabisa, maana nimejaliwa bure nami ninatoa bure.

Wale wenye tabia ya kupuuza maandiko kama haya ninawaomba kuzingatia sana maana bila afya hata kusoma maandiko mengine itashindikana kabisa. Tujitahidi sana kuzingatia na kuitumia mimea yetu tuliyonayo kupitia wataalam mbalimbali kutatua changamoto zetu za kiafya. MIMEA NI HAZINA KUBWA YA MUNGU.

TIBA ASILI YA MAGONJWA YA MOYO
Kabla ya mambo mengine yahusianayo na tatizo la moyo, ninaomba kukufundisha tiba hii asili ya matatizo ya moyo ambayo unaweza kujitengenezea wewe binafsi hata ukiwa nyumbani kwako.

1. Andaa American garden vinegar lita moja(Hii inauzwa kwenye supermarket zetu)
2. Andaa limao iliyokaushwa kiasi cha robo kilo
3. Andaa maji safi na salama kiasi cha nusu lita.

Changanya lita moja ya American garden na kiasi cha robo kilo ya limao iliyokaushwa, ongeza kiasi cha nusu lita ya maji safi na salama na kisha koroga vizuri kabisa na uhakikishe mchanganyo wako umekaa vyema. Baada ya hapo, mchanganyo wako uko tayari kwa matumizi.

MATUMIZI
Tumia vijiko viwili asubuhi,mchana na jioni. Au Tumia vijiko vinne mara tatu kwa siku(asubuhi, mchana na jioni) katika maji ya moto.

Mchanganyo huu ni salama kwa afya yako na unaendelea kutumika na kuponya watu mbalimbali. Mchanganyo wote huo ni virutubisho.

Mchanganyo huu utakusaidia mambo yafuatayo ambayo huwa ni matokeo ya magonjwa ya moyo

1. Miguu kuvimba, kufa ganzi na kuwaka moto.
2. Maumivu ya kifua na mgongo
3. Maumivu sehemu za mbavu
4. Maumivu ya viungo
5. Maumivu ya shingo.
6. Nguvu za kiume(zitarejea automatically)
7. Kifua kubana wakati wa usiku
8. Kupumua kwa shida n.k

CHANZO CHA MAGONJWA YA MOYO
Magonjwa ya moyo hutokea pale ambapo moyo huathiriwa na kuharibiwa kwa vitenda kazi vyake. Kuna mitindo ya maisha inayoweza kukuweka hatarini kupata magonjwa ya moyo nayo ni pamoja na;

1. Kuwa na lehemu (Cholesterol) na Shinikizo la damu (B.P), Kuvuta sigala
2. Uzito kupita kiasi na unene uliozidi
3. Kisukari
Kukaa sehemu kwa mda mrefu bila kuufanyisha kazi mwili
4. Umri
5. Ulaji holela wa vyakula vyenye mafuta mengi na sukari nyingi
6. Utumiaji wa vinywaji vinavyobadili hali ya mwili
7. Historia magonjwa yanayoambatana na moyo katika familia

AINA ZA MAGONJWA YA MOYO
Zipo aina mbalimbali za magonjwa ya moyo hutofautiana japo yote huathiri moyo, nayo ni;

[emoji2389]Ugonjwa wa moyo unaotokana na kuathirika kwa mishipa ya damu (Coronary artery disease)

Hili ni tatizo linalowakuta watu wengi, mishipa ya damu hupasuka na kuharibika hii hutokana na mishipa ya damu kuwa na uchafu na mafuta mengi na kufanya damu isipite vizuri

Mapigo ya moyo kwenda tofauti (Heart Arrhythmias)
Hii hutokea pale mapigo ya moyo kwenda taratibu isivyo kawaida au kwenda haraka isivyo kawaisda, pia mapigo ya moyo kwenda ovyo. Hii ni hatari sana na huua sana

Moyo kushindwa kufanya kazi (Heart Failure)
Hii ni hali moyo hushindwa kufanya kazi yake kama kupampu na kusambaza damu, kusambaza oxygen. Hii inaweza kutokea kwa mtu mwenye magonjwa kama ugonjwa wa moyo wa misipa kuathirika, Shinikizo la damu, na magonjwa mengine

Magonjwa ya moyo ya kuzaliwa (Congenital heart disease)
Haya ni magonjwa ambayo wengi huzaliwa nayo, yanaweza kuwa ni baadhi ya kasoro katika mwili kama baadhi ya chemba za moyo kuziba au kupasuka, oxygen kupita kwa shida na vinginevyo.
[emoji2393]Ugonjwa wa valvu na misuli ya moyo (Heart Valve Disease & Cardiomyopathy (Heart Muscle Disease))

Katika moyo kuna chema nne nazo zinapitisha damu na oxygen kutoka kwenye mapafu, valvu hufunguka na kufunga. Valvu na misuli ikiwa imepasuka na kuharibika husababisha tatizo la moyo.

Moyo kutanuka
Hii hutokea pale damu ikiingia ndani ya moyo harafu mishipa ya kutoa damu ikiwa na tatizo ikashindwa kutoa damu nje ya moyo moyo utaanza kutanuka siku hadi siku. Kutanuka kwa moyo kunatokea usipotibu baadhi ya matatizo kama shinikizo la damu, moyo kwenda mbio, valvu na misuli ya moyo n.k.

[emoji2395]Shinikizo la damu (B.P) ni shinikizo la damu yako kwenye kuta za mishipa yako kwani moyo wako unasukuma karibu na mwili wako. Unaweza kuwa na shinikizo la damu (shinikizo la damu) kwa miaka bila dalili yoyote.

Mshtuko/ Shambulio la moyo (Heart Attack)
Ni kifo cha sehemu ya misuli ya moyo inayosababishwa na kuzuiwa wa usambazaji wa damu. Amana zilizo na mafuta huunda kwa wakati, na kutengeneza alama katika mishipa ya moyo wakoIkiwa baadhi ya misuli ya moyo inakufa, mtu hupata maumivu ya kifua na kukosekana kwa umeme kwa tishu za misuli ya moyo.

Chembe ya Moyo
Hii ni maumivu ya upande wa moyo maeneo ya kifua hutokea wakati unafanya kazi au hata kama umekaa kama ni yenye kukubuhu. Maumivu haya huambatana na kutokwa jasho na kukosa hewa. Hutokana na moyo kukosa damu ya kutosha.

Endapo utahitaji ushauri wowote juu ya magonjwa mbalimbali na tiba za mimea,mitishamba na lishe unaweza kuweka comment yako hapa hadharani tukaendelea kujifunza zaidi.

MCHANA MWEMA.
 
Msaada

Nina dada yangu ana vimba shingo ana anakuwa na vitezi tezi nyuma ya masikio.

Naombeni tiba yake
 
Salama wakuu, Mwenye kujua dawa ya kutibu tatizo la miguu kufa ganzi kwa mwanamke aliyejifungua tafadhali.
 
Back
Top Bottom