Step_Rocker
Senior Member
- Aug 31, 2021
- 197
- 323
Subscribed....
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ni jumapili njema kwa watu wa Mungu! Poleni sana na misiba watanzania wenzangu!!
Kama tunavyofahamu kuwa,miili yetu hujengwa na chakula tulacho.Chakula cha asili kikitumiwa ipasavyo kinaweza kabisa kuwa suluhisho na tiba kwa magonjwa mbalimbali.
Magonjwa mengi yanayowasumbua wanadamu leo yanatokana na kula,pamoja na kunywa vibaya kama ilivyokuwa zamani kabla ya Garika.MATHAYO 24:28,watu walikuwa wakila na kunywa vibaya! na ndivyo wanavyoishi watu wa siku hizi,hatujali kabisa juu ya kunywa na kula ili kuendelea kuhifadhi vyema afya zetu.
Tukumbuke kuwa,kadri tunavyokula aina mbalimbali ya vyakula ndivyo tunavyojitibu na kuweka kinga imara dhidi ya magonjwa katika miili yetu.
Kumbuka kuwa duniani kote,hakuna tiba na kinga ya uhakika ya mwili wako kuzidi chakula bora.
Kila mara,watu wengi hula chakula aina moja na kuona wameshiba wakati huo,huku baadhi ya viungo vingine vya mwili vikilia na kuomboleza kwa kuwa havikupata stahiki yake,maana yake vimelala njaa.
Kipo chakula cha mifupa,moyo,macho,ngozi,afya ya uzazi n.k.Unapokula mchanganyiko wa aina mbalimbali za vyakula hasa nafaka utajitibu magonjwa mengi na utashangaa uponyaji mkuu wa Mungu ulio katika mimea ya asili.
Kuna nguvu kubwa ya uponyaji wa Mungu katika Ngano,shayiri,kunde,dengu,mtama na kusemethi.Ukisoma Ezekiel 4:9 utaelewa vyema.
Mungu anamwagiza nabii Ezekiel achukue Ngano,shayiri,kunde,dengu,mtama na kusemethi atengeneze mkate kwa kutumia mchanganyiko wa nafaka hizo aina sita(6).Mkate huo ungempa afya na kumlinda kwa siku 390 ambazo Mungu alikusudia awe ishara kwa waisrael juu ya jambo alilokusudia kulitenda juu yao,maana mkate huo ulikuwa na kila aina ya virutubisho na Ezekiel angestahimili bila tatizo juu ya mwili wake mda wote wa siku 390 au mwaka na siku 25.
Je nafaka hizi husaidiaje kutibu magonjwa...!??
1.Ngano isiyokobolewa ina virutubisho asilimia 100 kama ikitumiwa ipasavyo, ina uwezo mkubwa wa kutibu magonjwa sugu kama moyo,kisukari na mifupa.
2.Ndivyo ilivyo kwa shayiri,husaidia kwa wagonjwa wa figo,ini na pia husaidia kutengenezwa kwa kichocheo cha insulini kwenye kongosho na hivyo hutiba na kukinga sukari kwa uhakika.
3.Kunde ndicho chakula na tiba ya uhakika katika mwili wa binadamu kama umepungukiwa na damu,kula kunde kwa muda wa wiki mbili tu utakuwa na damu ya kutosha.Majani ya kunde ni tiba ya uhakika kwa wagonjwa wanaoishiwa nguvu mwilini,chemusha majani ya kunde upate supu na weka chumvi kidogo,kunywa glass 2 mara tatu kwa siku ikiwa ya vuguvugu kwa siku tatu mfululizo.Hata kama uko kitandani utainuka utembee mwenyewe.Kumbuka kuwa kunde ndiyo mfalme wa nafaka zote.
4.Kusemethi pia ni kundi la nafaka,huliwa zaidi mashariki ya kati kulingana na upatikanaji wake,nchi kama Israel,Palestina,Jordan na hata Asia.Ni lishe ya ubongo hasa kwa wanafunzi, madaktari,wafanyakazi wa maofisini na wengine wanaotumia akili nyingi katika kazi zao.Unaweza kutengeneza chakula cha ubongo( Brain Activator) kwa mchanganyiko wa ngano,dengu,ufuta na shayiri.Uji wa nafaka hizi ni tiba ya akili,neva na mifupa.
5.Mtama ni chakula kisichopendwa na wengi sana,na hapo ndipo shetani ametupiga upofu.Sifa kubwa ya mtama ni kustahimili ukame.Katika Biblia ukame huwakilisha matatizo,ama shida.Kuna aina mbili za nafaka ambazo hustahimili ukame yaani shida nazo ni mtama na dengu.Watu wanaotumia zaidi chakula cha mtama,hustahimili zaidi juu ya magonjwa katika miili yao zaidi ya mtu anayetumia sembe.Wazee wengi tunaowaona leo wengi wao wamekuzwa na mtama na miili yao imestahimili magonjwa ya kila aina.
Unaweza kula mtama kwa ugali,uji au pika mtama kama unavyopika wali,ni chakula kizuri kwa nguvu za mwili,mifupa na misuli.Vijana wengi leo wana upungufu wa nguvu za kiume kwa sababu ya ulaji mbaya,kijana umeoa lakini unashindia chips unategemea nini??
Daniel 1:12-15,Daniel na vijana wenzake walikula chakula cha mfalme kinachotoa unajisi katika miili yao,waliomba tu mtama na baada ya siku 10 walikuwa Baba kuliko vijana wengine.
6.Dengu ni nafaka inayostahimili ukame wa aina yoyote,kumbuka dengu hulimwa wakati wa kiangazi na huivishwa na umande tu.Katika biblia umande huelezwa kuwa ni baraka ya Mungu(Mika 5:7,Torati 33:13),ni nafaka pekee inayovuta baraka za Mungu kwa ajili ya kukomaza mazao yake na sisi tunazipokea baraka hizo kwa kushiriki chakula hicho cha pekee.Dengu ina vitamini A kwa ajili ya macho,watu wengi wanasumbuliwa na macho na dawa ipo imejaa kila mahali.Dengu pia ina madini ya zink kwa ajili ya afya ya uzazi kwa wanaume.Dengu huimarisha seli za mwili na ni kinga ya magonjwa ya moyo.
Leo vyakula vya nafaka vipo kila mahali,lakini watu hawavitumii.Watu wanaendelea kula chips,sembe na maandazi ya viwandani.Hebu tafakri kwa kina kuwa ni kwa kiasi gani unatumia vyakula hivi?? Yawezekana changamoto zako za mwili ni kwa sababu hii.Ndugu zangu tuendelee kula na kunywa kiasili bila kusahau kujitibu kiasili kwa dawa zetu za mimea ya mitishamba inayotuzunguka.
TUREJEE EDENI.
Nafaka zimejaa kila mahali katika masoko yetu.Ni maamuzi tu!Asante sana mkuu nimekuelewa ila changamoto ni upatikanaji wa vyakula vya asili.
Hongera kwa kutambua hilomtama ndo ugali wangu kila wakati
Grisi tu ndio dawa hawatarudi tenaa.... utatuna 20k ya asanteWajumbe habar za Jumapili.
Naomba mnisaidie Dawa ya kufukuza popo. Wamevamia kwenye kastoo kangu ka kuhifadhia bidhaaa yaaani ni kero. Ni wengi mnoooooooo. Nimejaribu ugoro, Oil chafu, Grease na dawa za Dukan za Fumigation lkn hawakomi. Naomba msaada wenu
Nipo navikusanya wakati wengine wa wkiendelea kuvitumaNikajua utaanza wewe kushusha kama vitano hivi
Mrejesho vioi asee Jambo KubwaShukrani sana, naanza dozi mara moja
Achana na hao wafanya biashara.Badilisha mfumo wa kula... mfatilie dr boaz mkumbo youtube na insta na fb... unafundishwa kuacha vyakula vya sukari na uwanga kabisaaa na kula vyakula mbadala ambavyo vinavyotokana na wanyama na mboga za majani tu kwa muda wa miezi mitatu.... ukiweza kufanya hivyo utapona maradhi mengi sana ambayo hapo zamani hukuzani km ni maradhi... ikiwemo na kupunguza kitambi na uzito mkubwa
Mkuu ni ipi dawa ya mtu asiye hisi harufu kabisa toka utotoniUte
Tumia kusugulia Ute wa alovera kwa dk15 ad 20 Kisha osha kwa maji vugu vugu alafu pakaa mafuta halisi ya nyonyo fanya ivyo 1X2 ad utakapo ona nywele zimerejea.
Nikutakie mafanikio mema[emoji1431]
Kununua chakula chako mwenyewe sokoni ukapika mwenyeo na ukala mwenyeo kuna biashara gani hapo. Muombe mungu yasikukute... uendelee kuyasikia tu kwa wengine.Achana na hao wafanya biashara.
Hakunaga chakula kibaya hapa duniani maadamu sio sumu
Picha ya mmea iko wapi?Habari za usiku huu, naomba nishare nanyi dawa Moja itokanayo na mmea uitwao leaf of life, sijui kwa kiswahili unaitwaje.
Hili Jani nililifahamu kabla lakini sikuwahi kulitumia, Juzi wife alipata tatizo la kifua alikuwa anakohoa Sana, na pumzi zinabana Sana na akipumua ni Kama mtu mwenye pumu, kumbukumbu ikanijia kuwa huu mmea unasaidia kwa matatizo ya upumuaji na bahati ninao mmea wenyewe, nilichuma Jani Moja akalitafuna na kufyonza maji yake, basi baada ya Kama dakika Tano tu akawa Safi kabisa kifua kimefunguka na akapata usingizi Safi kabisa.
Tuutumie huu mmea nasikia umejaaliwa kuwa sababu ya kuponya maradhi mengi tu.
Tafadhali Kama Kuna anayejua matumizi zaidi ya LEAF OF LIFE ni vyema ayaweke ubaoni hapa ili sote tuelimike.
Sent from my itel L5007 using JamiiForums mobile app
Akina boaz wanafanya biashara tuKununua chakula chako mwenyewe sokoni ukapika mwenyeo na ukala mwenyeo kuna biashara gani hapo. Muombe mungu yasikukute... uendelee kuyasikia tu kwa wengine.
Vyakula asili sio sumu ila watu wanachakachua sana... utalishwa tu sumu bila ya kujua