Uzi maalumu wa picha za nukuu na misemo mbalimbali ya kiislamu

adriz

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2017
Posts
12,207
Reaction score
26,521
Assalam'aleikum...

Karibuni wote katika sehemu rasmi hapa Jf ya kuelimishana na kuzinduana na kupata maarifa kupitia picha za nukuu na picha zinazohusisha dini ya kiislamu . Baada ya pilipilika mabalimbali ni vyema kupata kitu hata kidogo kitachoongeza kitu katika siku yako na pengine jambo kitu kidogo kinaweza kuwa na manufaa makubwa kwa mtu..

Moja jambo ambalo ningependa kuhusia ni tukumbuke kutubia na kuomba msamaha kwa Allah mara kwa mara ,kwani tumepewa fursa kubwa ya kurekebisha mambo yetu kwa kutubia na kuomba msamaha ila wengi tunaghafilika kwa kudhani muda tunao wa kutosha hatimaye mauti huja ghafla bila ya kutubia toba ya kweli na kusimama katika hali ya sawa na hii ni hasara kubwa kabisa.



 
UJUMBE WA USIKU:-
~~~~~~~~~~~~~~~~~~~
LEO KATIKA UJUMBE WA USIKU


Katika mambo ambayo inamlazimu muislamu kudumu nayo na iwe kwake ni mafikio ya kila siku ni dhikri zilizo ainishwa na mtume ﷺ na usomaji wa Qur-ani.

Kwani ktk usomaji wa dhikri na Quran:

1) Utapata malipo na kuzidishiwa hasanaat.
2) Utafutiwa madhambi na makosa.
3) Utapandishwa darja.
4) Utapata radhi za ALLAH.
5) Utamdhoofisha shetwani na matamanio.
6) Utaikinga nafsi yako kutokana na shari na husda na shari za wenye kupuliza.
7) Utaitakasa nafsi yako na utainyanyua ili iwe ni miongoni mwa nafsi Mt-mainnah.
8) Utakuwa maarufu mbele ya Malaika mbinguni.
9) Utapata mwisho mwema wakati wa mauti.
10) Litakuwa kaburi lako ni bustani za peponi.
11) Utafufuliwa ukiwa na amani siku ya mkusanyiko kwenye kiwanja.
12) Utapandishwa kwenye pepo ya hali ya juu.
13) Utakirimiwa kumuona na kuwa jirani naye sayyidinaa Muhammad ﷺ.

ALLAH atujaaliwe tuwe miongoni mwa watu wenye kumdhukuru yeye na kumshukuru.
___________
🌿DARSA YA FIQHI🌿
 
Mashaallah
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…