Magical power
JF-Expert Member
- Sep 27, 2022
- 2,158
- 5,626
UZI WA KIJOBLESS NA MBINU ZA KIDIGREE
(Utatu wenye utata
)
GAP YEAR......!!!
Kati ya mwaka 2017_2018, inaweza kuwa mwanzoni au mwishoni mwa miaka hio kumbukumbu zangu hazijakaa vizuri.
Nilikuwa nafanya kazi kwenye kampuni ya kusambaza vinywaji. Yaani mimi ndio nilikuwa natembea na gari kusambaza vinywaji vijijini.
Ndio Mimi nilipewa eneo la vijijini kuhakikisha vinywaji vinasambaa kila kijiji. Nilikuwa afisa mauzo wa upande wa vijijini.
Ilikuwa ni pombe, nilisambaza ile pombe mpaka vijana wa vijijini wakaacha kulima, wakawa walevi waliokubuhu. Hapo kuna kukubuhu na kupindukia sasa wale vijana walikubuhu.
Ile pombe ilikuwa inatengenezwa mkoa mmoja tu, na huo ambao uliwekwa kuwa wa majaribio kabla haijaanza Tanzania nzima.
Kiufupi ile pombe ilifungiwa, sijui sababu hasa ni nini lakini ikafungiwa kiwanda kikafa. Hapo ndio tunapata hio GAP YEAR.
GAP YEAR ni kipindi ambacho unakaa unakuwa huna kazi ya kufanya, huna shughuli yoyote kiufupi kichwa chako kinakuwa karakana ya shetani.
Baada ya kampuni kufungwa, mimi nilikuwa nimepanga mjini, nyumba kubwa tu. Basi kwenye ile nyumba tulikuwa tunakaa watu wanne. Mimi, Familia mbili na Mdada mmoja alikuwa hajaolewa.
Huyo Mdada tumuite Kamsi. Kipindi nakaa kwenye nyumba hio nilikuwa nakaa na mpenzi wangu yeye tumuite Uche.
Hata hivyo mimi nilikuwa sio mtu wa kushinda nyumbani sana kwa mwezi naweza kushinda mara mbili au moja.
Kipindi kampuni inafungwa Uche alikuwa amepata kazi mkoa mwingine hivyo katika hio GAP YEAR nilibahatika kuweka mazoea na Kamsi.
Kamsi alikuwa mpole, hakuwa kama wadada wa mjini wale wengine. Lakini Kamsi alikuwa analala ndani na analipa kodi anavaa na anakula nyie Dunia inamaajabu.
Tuachane na maajabu ya Kamsi. Basi Kule alikokuwa anafanya kazi Uche ile kampuni ilikuwa inatoa rikizo kwa mwaka mara moja tu.
Hapo ni miezi mitatu toka Uche aondoke. Kama nilivyosema awali kichwa kisichokuwa na kazi ni karakana ya shetani.
Nikawa namtaka Kamsi, lakini nitampataje Kamsi na anamfahamu Uche. Nikaja na mpango mahususi wa kijobless zaidi.
Basi nikaanza kurusha ndoano zangu kwa Kamsi, lakini kila nikirusha zinagoma Kamsi anadai anamjua mtu wangu na hataki kuharibu mahusiano yangu.
Nikaona huu ni mwezi wa tatu na Uche kupata likizo ni mwezi wa 12, I mean nina miezi tisa ya kupiganisha hapa katikati ikabidi nimkane Uche.
Nikamwambia sikia Kamsi Uche ni moja ya wanawake washenzi sana, katoka hapa kaenda huko kupata kazi kaolewa na mfanyakazi mwenzake😭😭😭
Nikaanza kulia, hapa nilikuwa nalia baada ya kukumbuka sina kazi na kodi inakaribia kuisha weeeee weeee wee nililia na mengi.
Kamsi akawa ananibembeleza kwa kunipa pole bhana.
Kuna rafiki yangu wa kike anaitwa Joy. Siku mbili mbele nikampigia Joy nikampa mpango.
Nikamwambia Sikia joy nakupa hii namba ya Mdada anaitwa Kamsi, mpigie mwambie unaitwa Uche. Then mwambie ni kweli umeolewa uko jifanye unajutia kwa ulichonifanyia, then mwambie mimi ni husband material hivyo kama anaweza awe na mimi hakuna shida.
Basi bhana joy ni mwana sana sio kama josh, lakini wait hawa wawili majina yao yanaanza na Jo hawa me siwaaminigi mjue, joy sio josh wa kiume kweli hebu tuone.
Basi kweli siku tatu mbele Kamsi akawa ananambia kuwa kaongea na Uche, kumbe kweli kaolewa hivyo kunibembeleza kwingi like utapata mwingine.
Basi bhana Kamsi akaanza kuwa karibu na mimi. Wiki moja mbele akanambia jumapili nitakuja kukutembelea.
Nikashangaa huyu Kamsi tunakaa nae nyumba moja anasema jumapili atakuja kunitembela, weeeee hapa lazima unyama nipate.
Eeh mnasemaga sijawahi fanikiwa kupata DEMU na hapa nimefanya nini mtoto Kamsi kanasa kwenye mtego mwenyewe makofi kwa joy tafadhali.
Siku masaa yakapita, kweli bhana Jumapili hii hapa ikafika, nikaenda kununua kuku, soda, wine na nikapika pilau.
Toka asubuhi me sikumuona Kamsi bhana, mimi sikujali nikapika niliungua sana siku ile lakini kwa upendo wangu kwa Kamsi sikujali.
Vitu vikaiva bhana vinanukia kwelikweli. Basi saa tisa hivi ugeni mzito ukafika kwangu.
Guess what..... Alikuwa na JOY, KAMSI NA UCHE.
WEEEEEEEEEH WEEEEEEEEEH, wimbo wa KASONGO ulipiga kichwani wote ukaisha ndani ya sekunde, nikabaki nimesimama mlangoni.
Mnakumbuka nilisema ile nyumba kodi ilikuwa inaelekea kuisha🥹🥹
Ninachoweza kuwaambia ile ndio ilikuwa siku ya mwisho mimi kuonekana pale,. nilihama nyumba ile bila kuchukua chochote, Kiufupi SIKU ILE NILIKIMBIA KAMA SWALA 😂😂😂
nikarudi nyumbani mwenda kwao sio mtumwa 😂.
Lakini hawa wakina JO wanashida gani wakuu.
Kilichokuwa kinafanyika kumbe Kamsi na JOY. Ni marafiki, pia Kamsi na Uche ni marafiki na mimi sikuwa najua yote hayo.
Hapo ndio ilikuwa mbwa Kala mbwa.
Siku hiyo hiyo naona wameniunga kwenye group la Whatsapp bhana, wanajiita THREE WIFE ONE HUSBAND.
alafu Joy akaweka status akasema LEO NIMESHIBA KAMA MAMBA😭😭 Umeshiba kwa chakula la nani ubwa wewe.
Kule kwa group walikuwa wanasema hawaondoki mpaka mimi nirudi tuyajenge. Muyajenge na nani kwani mimi Fundi...?
Nimerudi nyumbani, huku nyumbani nikazua msala mwingine. Huu ni mkubwa zaidi ya nilio ukimbia weeeeeeeeeh ikabidi nirudi kwangu. Maana wale majamaa walikuwa serious hadi wakalipia kodi ya miezi sita wakaamia kwangu kabisa.
Narudije kule, mpango sio mpango kama huna mwana kama Nango....!
wait for part two( it's not over until it's over ).
Pichani ni mimi nikiwa kwenye kuandaa DIKO LA KAMSI👇👇👇👇