Uzi wa kuelezea matukio ya kutisha uliyowahi kukumbana nayo maishani, either ya kichawi,anything scary

Dah pole sana hukupata tena maruwe ya namna hiyo baada ya kufukuzwa? Na pete uliirudisha?
 
Duh ganja gal asee kiboko na ule mdomo wake ungekuwa kama soseji kwake [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Jozay joo tupe zilipendwa hiyo ulipata msala gani? Inawezekana Pete ilisababisha? Uliirudisha kwa .mwenyewe.
Mkuu Pete niliirudisha kimya kimya kwenye kitanda nilipoikuta hata sikumwambia mtu, mida ya saa 5 asubuhi ndio nikafukuzwa shule moja kwa moja kwa kosa la kutokufanya usafi! ila barua ilisema nina kosa la utovu wa nidhamu lakini niliomba nipewe adhabu lakini walimu walipinga vikali.
 

Ulichukua mkoba wa mtu mkuu.
 
[emoji15] [emoji15] [emoji15] pole sana mkuu
 
Ikawaje sasa na ile pete. Ulisepa nayo?
 
Mkuu ulikuwwa shule gan?
 
Hata Mimi nawaza hivyo ! iLa jamaa mwenye ile Pete ni kichwa kweli darasani ndio alikua anategemewa, jamaa alikua fundi wa kupiga kinanda ile mbaya, na alikua kiongozi(mwenye kiti) wa kikundi cha (TYCS)

Wengine wanapewa ulinzi kwao, nakumbuka nilipokuwa o' level bwenini Mara ticha anatukana asubuhi asubuhi nyie wanafunzi washenzi sana nakwambia hamniwezi sisi tukabaki kutoa macho. Mwisho tukamuuliza Ticha tumekufanya nini? Au wameiba sefuria ya wali akasema ............ Alikuwa kuniwangia nimemuona anamchezea mtoto wangu.Ntammaliza asinichezee.
Ilikuwa mbaya sana aiseee na watu wengine walilalamika.
 
Aisee nimeisoma asubuhii hii,, alikua amevaa ni i huyo mtu? Ni mvulana su msichana?
[emoji2] [emoji2] kwa jinsi muonekano wake ulivyokuwa, ni mwanaume na alikuwa kifua wazi na kwa chini ni kama kajifunga msuli maana weupe wa kuanzia kiunoni ulikuwa mkali kuliko wa kifuani. Yaani alikuwa kama kapaka poda.
Lakini baada ya siku nyingi kupita maza alikuja kutueleza kuwa mtu aliyefanya ule uhuni ni Mzee mmoja alikuwa anakaa nyuma ya nyumba tuliyohamia. Alimegewa hiyo stori na wenyeji wa mtaani kuwa huyo Mzee mlozi balaa, na zile kelele zilifika mbali. Kwahiyo watu walijua kilichoendelea. Lakini cha ajabu, huyo Mzee aliyeshutumiwa kuwa ni mlozi, ndiye aliyekuwa wa kwanza kuja hom asubuhi kumuuliza bi mkubwa kuhusu kelele za watoto usiku.[emoji2] [emoji14] [emoji23]
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]dah wachawi bnh , ila hata mimi ninapoishi kuna vitu vya ajabu sana mfano usiku nasikia sauti za mtu kutembea, mara taa zitazimika, pia nasikia milango inajifunga ilhali hakuna nafasi ya upepo kuingia kwani madirisha yamefungwa, ila tukaambiwa ni mzimu wa fundi fulani aliyekufa wakati nyumba inajengwa ila siamini hizo story ,pia kuna muda utaweka kitu sehemu flani badae unakuta kimekua placed sehemu tofauti ilhali upo mwrnyewe ndani...
 
Ningekuwa me na huu uoga Wangu haki ningekufa asee
 
Walozi sio watu wazuri kabisa. Kuna mkasa mwingine nilikutana nao miaka hii ya 2000s. Mimi huwa napenda sana kurudi home usiku au hata nikisafiri nifike sehemu usiku ili asubuhi watu washtukie niko mtaani.
Sasa siku moja nimetoka mizunguuko yangu ya kawaida ilikuwa Moro hiyo. Mida ya saa tano usiku narudi home huku nawaza ntawaambia wazee sababu gani ya kuchelewa. Maana walikuwa sheria saa tatu nisiwe nje ya nyumba.
Sasa nikawa nakaribia nyumbani, na kwa macho napaona ila hakuna njia ya mkato ya kupita bali kuna kauchochoro kakuzunguuka ndio utokee njia kubwa ndio uingie ndani.
Nikawa nakiwaza hicho kichochoro maana kina simulizi mbovu kweli, nikapiga Moyo konde ila nikaamua kuongeza spidi ili nivuke ilo eneo haraka.
Basi nikachanganya mwendo balaa huku nywele na mwili wote unanisisimka. Ile nimefika katikati ya kile kichochoro, hamad! Nikakutana na kitu ambacho hadi leo sijakielewa, kwamba kilimaanisha nini? siku itabidi nimuulize Mshana Jr.
Nilikuta bonge la kinu cha kutwangia kimewekwa katikati ya ile njia. Ni Mungu tu alinilinda, maana kwa ile spidi ningekivaa tu!! Niliogopa sana, ila akili ilifanya kazi haraka, nikapita kwa pembeni. Hiyo spidi niliyotoka nayo hapo, hata bombadier isingefua dafu. Sikuwasimulia nyumbani hadi nilipokuwa nimeanza maisha yangu, maana ningekula hamsa vilevile na uhenga wangu.[emoji28]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…