Uzi wa kuelezea matukio ya kutisha uliyowahi kukumbana nayo maishani, either ya kichawi,anything scary

binafsi nina matukio matatu moja nikilishuhudia mengine ni yakusikia.

miaka ya 95 nikiwa mdogo lakini nikiwa na ufahamu jumamosi fulani saa 12 kasoro asubuhi hali ya hewa ikiwa mawangu nadhani ilikua ni kipindi mvua za masika zikikaribia kuisha, kwa wale wenyeji wa moshi nadhan hali hii munaifahamu. kunakua na mawingu yametanda kiasi cha mtu alie mbele yako mita 5 huwezi kumuona.
siku hio nilikua nikienda jumuia kwa wakaliki haswa wa kule moshi mnajua jumuia livyokua ni muhimu kuhudhuri na mimi nilingwa kwenye msingi huo nikiwa toka mdogo, na tulikua tunasali nyumba kwa nyumba.

sasa nilivyokaribia hio nyumba iliokua na zamu ya kusali na hali mawingu yakiwa yametanda niliona watu kama watoto hivi wakiwa wameungana mwili isipokua kichwa. yaani mwili ni ni mmoja na vichwa viwili.
sasa yale mawingu yalizuia tusionane mmapena hamaki tukakaribiana, waliponiona walismama kidogo kama vile walistuka nikaona wanaywea kushuka chini yaani kama mshumaa unavyoisha, lakini kwa kasi mara wakaisha wakawa kama jiwe na mwishowe sikuona kitu.
sikuogopa sana nilienda kusali zangu lakini liletukio sikulisahau mpaka leo.
 
Duh,,sio mchezo,,sema ukikutana na jini au mauzauza yyte uspostuka au kuogopa bc yanapoteza nguvu
 
la pili kule moshi wakati wakilimo watu walika wakilima mahindi mashamba ya mbali kidogo. wakati wa mavuno usafiri wa kuleta mazao nyumbani ulikua ni matrekata au malori yale ya zamani kama isuzu nk.
sasa ile nyumba tuliokua tunasali walikua wamelima kwa ushirika kati ya mzee wao na watoto wao 3 ambao wanafamilia zao na moja ya hio familia ndio tulienda kusali nikakutana na wale watoto walio yeyuka.
siku ya mavuno ilipokaribia kwao walivuna vizuri tuu na kupakia mahindi kwenye gari ambalo kiuhalisia lilikua bovu bovu, lakini lilijitahidi kubeba mzigo mpaka karibu na nyumbani wastani yalikua ni mahindi ya shamba lenye heka 8.
gari lilikwama umbali wa km kama 8 kufikisha mzigo nymbani na ilikua mida ya saa 5.
dereva akalaza gari ili kesho yake aamkie kulitengeneza .
mpaka wanaachana ilikua saa 6 alkini dereva alipokuja saa 11 kushughulikia gari alikuta mzigo mzigo umehamishwa wote na hata nyayo za watu kukatiza wakati wakihamisha hazikuonekana!
embu fikiri umbali kutoka mzigo ulipokwama ni km 8
kiasi cha mahindi si chini ya tani 15
idadi ya watu ni 3
saa walizotumia ni 5 kati ya saa 6 na 11.
halafu hakuna moviment ya watu kupita kuonyesha kulikua na kazi ya kusombelea mahindi
na pia hakuna hata jani lililo anguka chini!
katka hali ya kawaida ingewachukua wiki 3 kuhamisha mzigo ule lakini walitumia saa 5 tuu. ilisemekena huyo mzee alikua amefuga majini na ndio yaliobeba mzigo ule na ndio nilio kutana nao wakti ule yakirudi nyumbani kutoka kwenye mizunguko yao.
 
binafsi nina matukio matatu moja nikilishuhudia mengine ni yakusikia.

miaka ya 95 nikiwa mdogo lakini nikiwa na ufahamu jumamosi fulani saa 12 kasoro asubuhi hali ya hewa ikiwa mawangu nadhani ilikua ni kipindi mvua za masika zikikaribia kuisha, kwa wale wenyeji wa moshi nadhan hali hii munaifahamu. kunakua na mawingu yametanda kiasi cha mtu alie mbele yako mita 5 huwezi kumuona.
siku hio nilikua nikienda jumuia kwa wakaliki haswa wa kule moshi mnajua jumuia livyokua ni muhimu kuhudhuri na mimi nilingwa kwenye msingi huo nikiwa toka mdogo, na tulikua tunasali nyumba kwa nyumba.

sasa nilivyokaribia hio nyumba iliokua na zamu ya kusali na hali mawingu yakiwa yametanda niliona watu kama watoto hivi wakiwa wameungana mwili isipokua kichwa. yaani mwili ni ni mmoja na vichwa viwili.
sasa yale mawingu yalizuia tusionane mmapena hamaki tukakaribiana, waliponiona walismama kidogo kama vile walistuka nikaona wanaywea kushuka chini yaani kama mshumaa unavyoisha, lakini kwa kasi mara wakaisha wakawa kama jiwe na mwishowe sikuona kitu.
sikuogopa sana nilienda kusali zangu lakini liletukio sikulisahau mpaka leo.
Bado ya kusikia mzebaba
 
nyingine kwenye familia hio hio.
baada ya watu kuona mauza uza kwenye kijiji chetu walibidi wamtenge yule mzee..
kule kwetu watu wote ni wakatoliki na ni kama ndugu. sasa wanakijiji walipochezeshwa kanyabazonga na majini ya kununua ya yule mzee walishindwa kumstahimili.
bahati ilio njema kukatokea mtaalamu wa kutoa majini nae ni pro maji marefu, kipindi hicho alikua akivuma mno.

watu wakachanga wakamuagizia akaja na pikipiki kubwa lile.
ile kufika tuu njia ya kuingia kwenye nyumba ya huyo mzee alirushwa umbali wa km moja hivi yeye na pikipiki yake na msaidizi wake!
pikipiki ilipokaa sawa pro hakurudi nyuma alipitiliza huko huko na kurudisha majeshi akiahidi atarudi tena anaenda kujipanga upya.
alikuja kurudi baada wiki 3.
alichima mapembe kwenye ile nyumba shimo la futi 6 na akalikosa, akaishia zake hadi leo hakurudi japo aliahidi.

lakini hali ilikuja kutulia pale kijijini mpaka leo hii, ila watu hawna imani na yule mzee na familia yake japo alijitetea kwamba mke wake ndio anahusika sio yeye.
 
Siku moja enzi hizo tuliharibikiwa na gari maeneo fluni panaitwa makuyuni tukiwa tunatoka Dodoma tunaelekea Moshi kwa Bus enzi hizo ni ua kampuni ya Ralway hakuna mabasi mengine nilikuwa nipo darasa la saba

Kipindi hicho barabara ni mbovu sana gari inachukuwa siku mbili kufika moshi.

Ikabidi konda na abiria mmoja wafuate spear Dodoma nayo ilichuwa siku mbili.

Ilibidi tujiongeze tutafute nyumba za jirani ili angalau tupate huduma kama chakula, kuoga na kadhalika wazee na familia zingine walifanya hivyo.

Kutola hapo kwenye bus mpaka kwenye nyumba ni umbali wa kama kilometa tano hivi tukakuta nyumba mbili tu lakini tunashukuru nyumba tuliofika tukawaeleza shida zetu walituelewa ambapo alikuwa anaishi watu wawili tu kijana mmoja na mke wake ambaye alikuwa mrembo kweli wengi tulishangaa kwanini waliamua kuishi porini ili hali kwa muonekano walikuwa ni watu wastaarabu sana.

Basi baada ya wazazi wetu kupokelewa wakaanza mandalizi ya kupika na mambo mengine sisi watoto tulikuwa mimi na mdogo wangu na watoto wawili wa familia moja kama kawa hao tukaenda eneo fulani kama shamba hivi lakini kulikuwa na mteremko unaelekea kwenye mto pembeni ya uo mto kulikuwa na ndizi mbivu basi tukazikimbilia tukazichuma tukaanza kula.

Kwakuwa ule mto haukuwa na maji tukavuka hao upande wapili tunaona matunda ambayo siyakumbuki na mapera basi tuliendelea kuchuma na kula ilikuwa kama saa 12 jioni.

Baadaye tukaona kijumba kidogo tukaenda mpa kwenye hicho kijumba tukamkuya bibi mzee sana anachuma mboga kribu na nyumba yake tukasalimia tukamweleza sikumbuki nini lakini akatuletea mziwa tukanywa.
Mara kukawa na wingu zito sana na radi dakika kumi nyingi mvua ilinyesha tukaanza kukimbia nimemshika mdogo wangu ambaye alikuwa analia sana na mdogo wake na yule mwenzetu naye alikuwa analia basi yule bibi alituzuia eti mvua itakatika na pale mtoni hamuwezi pita tulichanganyikwa lakini mimi nilgoma nikaondoka na mdogo wangu nikawacha wale wenzetu kufika pale kwenye mto mto unapitisha maji ila sio mengi cha ajabu ngambo ya pili tulimuona yule Bibi na fimbo yake amekunja uso daa tulitetemeka sana anatunyooshea ile fimbo turudi.
Nyuma ya yule bibi tukaona kwa mbali mwanga wa tochi na sauti za watu kama wanaongea ndiyo hauweni kumbe mzee na wenzake wanatutafuta.
Yule bibi kuona watu akaja upande wetu huku akivuka mto tukampisha tukanza kumuita mzee huku tunatetemeka dogo analia tumeloa chakari mzee alivyotuona yeye mwenyewe alitetemeka kwa hofu.
Tukawaambia wenzetu wapo kwa bibi mmoja kule juu basi mjomba wao na mwenyeji waliwafuata kwa yule bibi huku mwenyeji akisema huyu bibi ni mchawi sana asije wazuru watoto wakakimbia kufika pale wakawakuta wapo ndani kwa yule bibi wanaota moto lakini wamejikunyata wamelegea sana hawajiwezi huku huyo bibi akiwa amejilaza kwenye kitanda chake anatamka sijui maneno gani.

Yule mwenyeji nasikia akamkoromea akamwambia lolote litakalo walata hawa watoto tunakumaliza ndiyo ikiwa salama yao.
Kufika pale kwa mwenyeji hapo ni usiku sasa kama saa 2:30 kunagiza tunawahadithia kilichotokea mh..wazazi waliogopa sana tukagombezwa sana...

Hayo ndiyo nakumbula lakini ilikuwa siku mbaya sana na sitaisahau maishani.
 
Kama kawa hizi stori sizisomi usiku huu[emoji1][emoji1] , nitazipitia kesho kwa kweli unajua bora movie ata iwe ya kutisha utaangalia usiku ila hutoogopa cause sio kweli but haya matukio humu ni ya ukweli so kuogopa ni lazma aise
 
[emoji23] [emoji28] [emoji28] [emoji28] [emoji28]
 
ni juzi tu nilikuwa nimelala na changu la kimanyema tanga,
nikiwa usingizini kwa kuwa ni changu silali kabisa kabisa sasa kuna muda niliona dude kama robot la chuma likitudondokea ghalfa lilipotua tu ule upande wa mmanyema ulirudishwa mbio kama short ya umeme ila mimi nililaliwa na huo mzigo wa chuma kizito.
Akili ikanijia nimguse mmanyema nikajigongesha kidogo tu kwa mmanyema lile zigo la robot likarudishwa juu kama short ya umeme na lilitoweka.
ni hali y kweli kwani sikuwa nimelala bali kujilaza ili pakuche.
 
Duh hukuumia livoanguka
 
Siku moja enzi hizo tuliharibikiwa na gari maeneo fluni panaitwa makuyuni tukiwa tunatoka Dodoma tunaelekea Moshi kwa Bus enzi hizo ni ua kampuni ya Ralway hakuna mabasi mengine nilikuwa nipo darasa la saba

Kipindi hicho barabara ni mbovu sana gari inachukuwa siku mbili kufika moshi.

Ikabidi konda na abiria mmoja wafuate spear Dodoma nayo ilichuwa siku mbili.

Ilibidi tujiongeze tutafute nyumba za jirani ili angalau tupate huduma kama chakula, kuoga na kadhalika wazee na familia zingine walifanya hivyo.

Kutola hapo kwenye bus mpaka kwenye nyumba ni umbali wa kama kilometa tano hivi tukakuta nyumba mbili tu lakini tunashukuru nyumba tuliofika tukawaeleza shida zetu walituelewa ambapo alikuwa anaishi watu wawili tu kijana mmoja na mke wake ambaye alikuwa mrembo kweli wengi tulishangaa kwanini waliamua kuishi porini ili hali kwa muonekano walikuwa ni watu wastaarabu sana.

Basi baada ya wazazi wetu kupokelewa wakaanza mandalizi ya kupika na mambo mengine sisi watoto tulikuwa mimi na mdogo wangu na watoto wawili wa familia moja kama kawa hao tukaenda eneo fulani kama shamba hivi lakini kulikuwa na mteremko unaelekea kwenye mto pembeni ya uo mto kulikuwa na ndizi mbivu basi tukazikimbilia tukazichuma tukaanza kula.

Kwakuwa ule mto haukuwa na maji tukavuka hao upande wapili tunaona matunda ambayo siyakumbuki na mapera basi tuliendelea kuchuma na kula ilikuwa kama saa 12 jioni.

Baadaye tukaona kijumba kidogo tukaenda mpa kwenye hicho kijumba tukamkuya bibi mzee sana anachuma mboga kribu na nyumba yake tukasalimia tukamweleza sikumbuki nini lakini akatuletea mziwa tukanywa.
Mara kukawa na wingu zito sana na radi dakika kumi nyingi mvua ilinyesha tukaanza kukimbia nimemshika mdogo wangu ambaye alikuwa analia sana na mdogo wake na yule mwenzetu naye alikuwa analia basi yule bibi alituzuia eti mvua itakatika na pale mtoni hamuwezi pita tulichanganyikwa lakini mimi nilgoma nikaondoka na mdogo wangu nikawacha wale wenzetu kufika pale kwenye mto mto unapitisha maji ila sio mengi cha ajabu ngambo ya pili tulimuona yule Bibi na fimbo yake amekunja uso daa tulitetemeka sana anatunyooshea ile fimbo turudi.
Nyuma ya yule bibi tukaona kwa mbali mwanga wa tochi na sauti za watu kama wanaongea ndiyo hauweni kumbe mzee na wenzake wanatutafuta.
Yule bibi kuona watu akaja upande wetu huku akivuka mto tukampisha tukanza kumuita mzee huku tunatetemeka dogo analia tumeloa chakari mzee alivyotuona yeye mwenyewe alitetemeka kwa hofu.
Tukawaambia wenzetu wapo kwa bibi mmoja kule juu basi mjomba wao na mwenyeji waliwafuata kwa yule bibi huku mwenyeji akisema huyu bibi ni mchawi sana asije wazuru watoto wakakimbia kufika pale wakawakuta wapo ndani kwa yule bibi wanaota moto lakini wamejikunyata wamelegea sana hawajiwezi huku huyo bibi akiwa amejilaza kwenye kitanda chake anatamka sijui maneno gani.

Yule mwenyeji nasikia akamkoromea akamwambia lolote litakalo walata hawa watoto tunakumaliza ndiyo ikiwa salama yao.
Kufika pale kwa mwenyeji hapo ni usiku sasa kama saa 2:30 kunagiza tunawahadithia kilichotokea mh..wazazi waliogopa sana tukagombezwa sana...

Hayo ndiyo nakumbula lakini ilikuwa siku mbaya sana na sitaisahau maishani.
Kuna mtu alipata madhara yyte? Na wale vijana wenyeji waliwaambiaje kuhusiana na hilo tukio?
 
Walozi sio watu wazuri kabisa. Kuna mkasa mwingine nilikutana nao miaka hii ya 2000s. Mimi huwa napenda sana kurudi home usiku au hata nikisafiri nifike sehemu usiku ili asubuhi watu washtukie niko mtaani.
Sasa siku moja nimetoka mizunguuko yangu ya kawaida ilikuwa Moro hiyo. Mida ya saa tano usiku narudi home huku nawaza ntawaambia wazee sababu gani ya kuchelewa. Maana walikuwa sheria saa tatu nisiwe nje ya nyumba.
Sasa nikawa nakaribia nyumbani, na kwa macho napaona ila hakuna njia ya mkato ya kupita bali kuna kauchochoro kakuzunguuka ndio utokee njia kubwa ndio uingie ndani.
Nikawa nakiwaza hicho kichochoro maana kina simulizi mbovu kweli, nikapiga Moyo konde ila nikaamua kuongeza spidi ili nivuke ilo eneo haraka.
Basi nikachanganya mwendo balaa huku nywele na mwili wote unanisisimka. Ile nimefika katikati ya kile kichochoro, hamad! Nikakutana na kitu ambacho hadi leo sijakielewa, kwamba kilimaanisha nini? siku itabidi nimuulize Mshana Jr.
Nilikuta bonge la kinu cha kutwangia kimewekwa katikati ya ile njia. Ni Mungu tu alinilinda, maana kwa ile spidi ningekivaa tu!! Niliogopa sana, ila akili ilifanya kazi haraka, nikapita kwa pembeni. Hiyo spidi niliyotoka nayo hapo, hata bombadier isingefua dafu. Sikuwasimulia nyumbani hadi nilipokuwa nimeanza maisha yangu, maana ningekula hamsa vilevile na uhenga wangu.[emoji28]
aisee haya mambo kumbe yapo kweli eeh...mimi mwezi ulioisha tu natoka home mida ya saa 5 na robo hivi usiku naenda kwa rafiki nilikua na shida binafsi...na ni nyumba tatu mbele kutoka home...huezi amini njiani NILIKUTANA NA UNGO MPYAA...yan MPYAA kabisa...niliupita nikaenda kwa rafiki ila sikupita tena njia iyo wakati wa kurudi.
 
Kipindi niko form one nilizidisha usumbufu mtaani mzee akaona hili dogo halitamaliza shule hapa town akanipeleka kusoma kwa babu kijijini kwetu alipozaliwa mzee.

Nilipofika pale kijijini kulikuwa kuna mti mmoja mkubwa nilikuwa nasikia story huwa kuna mauzauza.Siku moja nimeenda kucheki game ya UEFA ya Arsenal na FC Portal kwenye Banda la video pale kijijini.Nikawa nimekaa siti ya nyuma kabisa peke yangu kumbe nikapitiwa na usingizi nikaja kushituka game imeisha halafu niko peke angu.kuangalia saa ilikuwa saa nane usiku asee niliogopa sana.

kulikuwa na njia mbili moja ya barabara nyingine ya mkato.Ile ya mkato ndo inapita kwenye ule mti.niliona uvivu kunyoosha barabara nikasema nipite tu ya mkato.Ile nafika kwenye ule mti pembeni ya barabara nikakuta mwanamke amevaa nguo nyeusi amechuchumaa.Nikataka kujifanya sijaona mara Yule mwanamke akaniongelesha kwa kisukuma "Wewe, unatoka wapi" sikujibu.Akaniuliza tena "unaenda kwa nani" mimi kimya.Akaongea kwa ukali "mtoto mdogo usiku huu unatafuta nini hebu potea hapa haraka" niliondoka pale sikimbii ila nilipoenda mbele kidogo nilitimuka nadhani nilivunja ata record ya Bolt.

Nilipotokeza barabarani nilipishana na gari ambayo nilikua nasikia tu mlio tu ila gari yenyewe siioni.Nilikuja kuumwa balaa mpaka baba akaniombea uhamisho.

Ni issue serious iliyonitokea kijiji flani kipindi hicho ilikuwa wilaya ya Magu mkoa wa Mwanza ila kwa sasa nadhani ni mkoa wa simiyu.
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]dah wachawi bnh , ila hata mimi ninapoishi kuna vitu vya ajabu sana mfano usiku nasikia sauti za mtu kutembea, mara taa zitazimika, pia nasikia milango inajifunga ilhali hakuna nafasi ya upepo kuingia kwani madirisha yamefungwa, ila tukaambiwa ni mzimu wa fundi fulani aliyekufa wakati nyumba inajengwa ila siamini hizo story ,pia kuna muda utaweka kitu sehemu flani badae unakuta kimekua placed sehemu tofauti ilhali upo mwrnyewe ndani...

kwanini usihame? hapana kwa kweli
 
Back
Top Bottom