TAECOLTD
JF-Expert Member
- Mar 2, 2013
- 1,051
- 1,836
1) Miaka hiyo ya 1993 nikiwa kijijini Mengwe Rombo Kilimanjaro tulikua tunapenda sana kuwinda ndege kwa manati na kuwatega na mitego...
Mimi ndio nilikua kama kubwa la maadui, tukaenda kuwinda kwenye mapango ilikua mida ya jioni hivi, ila kwa mbali ndani tukaona macho yanawaka kama taa nyekundu hivi, mara mngurumo wa hatari tukausikia hapo, hizo mbio zake sikumbuki nikifika je nyumbani ila kuna mtoto mmoja alithurika ikajulikana walikua fisi, yule mtoto hakukaa sana akafariki...
Kijijini nimepita misuko suko mingi sana ambapo ningeshakufa muda tu
2) Tulikua na kawaida ya kwenda kuiba matunda na mazao kama mahindi kwenye mashamba ya watu kisha tunakutana sehemu tunayachoma tunakula weee, hiyo tabia ikawa inachukiwa sana na wana Kijiji, siku moja mzee mmoja alitufukuza na mishale ikawa inapita tu pyuuuuu kama muvi sie tunakimbia mashambani, ila bahati mbaya mshale mmoja ulimpata mwenzenu mguuni ila hatukukamatwa...
Hadi naletwa Dar mwaka 1995 nilishafanya visa vingi tu, miaka ikaenda nikapewa habari wale watoto tuliokua tunaiba wote mahindi walilogewa mahindi wakavimba matumbo wakafa wote walikua wanne, means namie ningekumbwa huko ningekufa pia
Maisha haya acha tu