Uzi wa kuelezea matukio ya kutisha uliyowahi kukumbana nayo maishani, either ya kichawi,anything scary

Nakumbuka nilikuwa darasa la tano mkoani mwanza wilaya ya misungwi shule maalufu sana pale wilayani, nikiwa na rafiki angu kipenzi yeye alikuwa mdogo kwangu.

Jioni kanipitia nyumbani twende tukaluke sarakasi nikamfundishe wakati huo ukijua kuluka salakasi ya nyuma wewe mjanja sana, basi bwana tukafika sehemu kuna tank kama tatu za maji nikamwambia tupite pale kwenye tank tukachukue asali, yani lile tank lina ngazi na bomba moja limeshuka mpaka chini sasa juu lilipo pita bomba kuelekea ndani ya tank kuna uwazi hivi hapo kuna bonge ya mzinga wa nyuki ukitikisa bomba inagusa ule mziga kwahiyo,

Nikamwambia best tutikise kwa nguvu ili nyuki wasambae tupande tuchukue asali, tulifanya lile zoezi kwa muda kama dakika tano nyuki walizagaa kwenye aga sehemu tulipo na ile milio yao iliongezeka kwa kasi ya ajabu mwenzangu akaanza kuogopa na kudai tuondoke huku nyuki wametanda anga zima nilimzuia asiondoke hakunisikia gafla akatoka mbio kuelekea maeneo ya nyumbani kwetu haikuwa mbali na maeneo yalipo matank ya maji.

Alikuwa akilia akitaja jina la mama angu, mama Fulani nakufa nisaidie mama alikuwa anafua uani akamsaidia kumvua tshit nyuki zikamuuma na mama ikabidi wakimbilie nyumba jiran ya mwalimu kuomba msaada kufika wakaingia ndani nyuki wakajaa tena ndani ikabidi wakimbilie nyumban kwa mwalimu mwingine yule rafiki angu kuona vile ikabidi akimbie mpka kwao huku nyuki wakimuuma.

Tuludi kwangu sasa baada ya kusikia kelele za rafiki angu na nyuki walishaanza kuniuma nilikuwa pale kwenye tank nimeganda nimejilinganisha kwenye ukuta nikaingiwa na huruma nikamuokoe jamaa ile natoka naanza kukimbia uelekeo aliokuwepo kundi la nyuki likanifuata niliumwa na nyuki kila sehemu ya mwili sipigi kelele nisije gundulika nilikuwa nimevaa kaoshi wasukuma wataelewa hapa yaani kama singland

Inavitundu vidogovidogo kama neti nyuki walikwama kwenye nguo wakawa wananiuma wameng'ang'ania kwenye nguo, nikageuza kuelekea uwanja wa mpira nilipita katkati ya shule yani parade nyuki walinizidi kwa maumivu nikaanguka macho yamevimba yote sioni vizuri mbele nikavua ile singland kuzuia nyuki kuendelea kuniuma nikaiacha hapo hapo parade

Kisha nikaendelea kutafuta msaada huku nakimbia ovyo, Sikuona mtu hata mmja mtaa mzima wamejifungia ndani nikaenda kwa rafiki angu mwingine nyumbani kwao ili anisaidie nilikuwa nishachoka kukimbia na nyuki bado wananiuma mwili mzima nanukia harufu ya nyuki kama ulishawahi kuua nyuki huwa anaharufu Fulani hiv, nilipofika kwa rafiki baba ake alikuwa ni mwl asieona akamwambia mwanae sitaki nimuone huyo kwangu mwambie aondoke, nikaondoka nikaenda kaa kwenye Shamba la shule nisubili usiku uingie niludi nyumbani cha ajabu nyuki wananifuata tu ikabidi niende kwao na jamaa angu tuliofanya tukio wote nikamkuta amelala kapewa Huduma na mama ake kampaka mafuta ya taa kisha akaenda kwenye kikao cha kujadili waponda nyuki ambao ni sisi, nashukuru rafiki angu akanihudia vzuri lkn kichwa kinaunguruma kama mashine kinauma balaa, masikio yanapiga kelele ziiii, akanipaka mafuta ya taa tukapumnzika wakt huo sina Niko kifua wazi nyuki wameniuma mpka wamejisifu

Mara mama wa rafiki angu kaludi kutoka kwenye kikao kaja chumbani katukuta tumelala mama anafuka huyo anamtukana mwanae,nikaamka kumsalimia mama alipigwa butwaa kama dkk nzima akaongea kilugha yy ni mjita alinihurumia nilivyovimba macho hayaonekani masikio yamekuwa makubwa kiufupi sura haieleweki tumboni Nina nundu na mgongoni, mama wa watu akaogopa nitamletea shida na kwa jinsi nilivyokuwa pia akasema kesho wamesema muende shule wote ili tukachapwe, nikaomdoka kwenda nyumbani, mama alikuwa mkali kuliko maelezo nilijua Leo sijui ila kwakuwa nilikuwa najisikia kuumwa sina namna mama kuniona akaanza kufoka kashika fimbo nilipomsogelea kalibu mama alishindwa kuongea ukali ukamuisha nilisikia sauti ya mama kama anataka kulia hivi nikaingia ndani akaja akanipa panadol nakumbuka nikapanda kulala, akaanza kusema wamesema wazazi tulipe fidia kwani nyuki wameua bata wawili na mwanafunzi mmja wa kike asiyeona kalazwa niliumia sana sikuwa na jinsi, niishie hapo story ni ndefu kuanzia siku hiyo namuogopa nyuki kama nini nikisikia tu mlio wa nyuki huwa nakumbuka kisa kile

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pole

Sent using Jamii Forums mobile app
 
[Hii noma QUOTE="ngebo, post: 24094314, member: 453062"]
Hahaha kaka yangu pole sana hivi visa aise nafurahia apa masimulizi ila usiku inakua patashika nguo kuchanika[emoji1], but ninavosikia ni kwamba kama hutoamini hayo mambo then inakua vigumu sana kudhurika ila mpaka uwe na imani kali kweli
[/QUOTE]
 

Mm ningekuwa nishahama zaman sana
 
Aisee kwa maelezo haya nimekujua vizuri...... KAMA NI IKE AJALI BASI NIMEKUJUA.
 
Eeeh mtu mrefu....mim navojijua ningezima kwanza
 
Nmecheka sana....pole lkn
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Ulikosea kumshika mtu shati mfe woote,weee ungetimua kuvyako
 
Pole aiseh
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…