Uzi wa kufundishana maisha ya Jela na selo

Uzi wa kufundishana maisha ya Jela na selo

Maisha ya Jela sio mchezo hata kidogo!.

Sitosahau siku napelekwa kwa mara ya kwanza Gerezani kukaa siku 14,kiukweli mwanzo unaweza kuona ni kama utani vile ila baada ya siku 3 ndiyo unaanza kuamini kweli nipo Gerezani.

Nashukuru Mungu ni sehemu ya maisha ila nilipata Funzo.
 
Ole wako..utapigwa chuma ya kisogo...ingawa wapo watu wanatoroka....ishatokea jamaa alitoroka jela kwakua alikua ameaminiwa sababu alikua amebakizA mda mdogo kutoka..sasa mfungwa akitoroka askari anashushwa cheo kimoja..sasa uyo askari akaenda kwa mganga wa vitabu..jamaa alivutwa kishirikina akaenda adi mji wenye gereza akashikwa kama kuku😬😬😂😂...mmoja yeye alitoroka mchana wakati wa kula kama vumbi...hii ni jela moja kanda ya kati..huyu hakuwahi kushikwa maana mganga aliemsaidia ni hatari
Waganga wa vitabu ndo wakoje na huwa maeneo yapi mkuu kama hautajalj
 
Makamarade nimeona nianzishe huu Uzi ili kupeana uzoefu wa maisha ya Jela. Sisi wote ni wafungwa watarajiwa alijisemeaga magufuli.

Sasa hebu tupeane mbinu maisha misamiati tamaduni taratibu za Jela ili siku ukienda kule unakuwa Mwenyeji. Pia tuambiane mabosi wanakaa maeneo gani kule Jela? Wanavyumba vyao?

Majitu yaliyouwa je Kila mtu anachumba chake? Au yamelundikwa? Je chumba gani ni hatari zaidi kule Jela na mfungwa gani ni hatari zaidi? Je kuna mfungwa yupo Jela toka mwaka 1977 ccm inazaliwa mpaka leo hajatoka?

Je wafungwa wanapata msongo gani wa mawazo akijua fika mke wake lazima agegedwe wakati yeye yupo Jela? Je wafungwa wakike Wana life la kibabe? La kindava kama wakiume?

Je, wafungwa wakike wanapashanaje joto kimapenzi? Nk
Duuh
 
Maisha ya Jela sio mchezo hata kidogo!.

Sitosahau siku napelekwa kwa mara ya kwanza Gerezani kukaa siku 14,kiukweli mwanzo unaweza kuona ni kama utani vile ila baada ya siku 3 ndiyo unaanza kuamini kweli nipo Gerezani.

Nashukuru Mungu ni sehemu ya maisha ila nilipata Funzo.
Tupe experience mkuu
 
Kazi ngumu bro,
Nakumbuka siku moja kuna gogo tulienda kubeba kuleta jikoni,umbali kama mt 50 tu, tulikua 15 tukashindwa kuliweka begani.

Nyapara tuliekua nae akaenda kwa mkuu akamwambia "niongezee nguvu wale jamaa wameshindwa"
Alitandikwa vibao, halafu akaja yeye na wenzie kama wa3 hivi.

Mkuu hukuwepo ila niamini tulibeba gogo likakaa begani na akaanza kupunguza mmoja mmoja mpaka tukabaki 8.

Hapa siongelei magereza yenu ya town(kazi kubwa kumwagilia maua na kufyeka majani). NGWALA,SONGWE,KISONGO,MAWENI,MPECHI na ISISI usiombe ukaingia hizi ngome....

ROHO YAKO MWILI WAKWETU
Na wanautumia kweli
Duuh
 
Picha linaanzia tuko site tunavuta bangi msituni huko, miongoni mwa wavuta bangi walikuepo maaskari tulikua tunanyonga nao.

Sasa yule pusha ilikua lazima awape kodi ya meza ili wamlinde wasimchome, naona alizingua aise lilitimba pila Hilo tulichukuliwa tukashuka central😬

Sasa ishu ikawa mtu wa kumcheki Kwa ishu kama io ya kisenge ya kuvuta bangi😀😀 nikasema nitakaa hapa adi mnitoe wenyewe mimi Sina ndugu yoyote hapa mjini🤣

Na kweli nimekaa mahabusu siku 3 wale jamaa kumbe target Yao ilikua pesa tu mwisho waliamua kuniachia tu
Yaani sikukuu imenikutia mahabusu. Nilacha bangi tangu hapo😬😂

Mahabusu kubaya sana sipati picha huko jela Kuna jamaa alikua analia tu aliletewa chakula Hali watu ambao hatuna ndugu tunabonda tu. Mahabusu unaweza kua huna ndugu ukala ukashiba Kuna watu wako so frustrated aise
Hahaha
 
Kama hilo wanaita NGWALA lipo milima ya chunya kama unaenda tabora(hii ni shortcut) gereza lipo katikati ya mbuga hata hamlindwi kama utaweza kimbia....
Naskia unavopelekwa gerezani njiani ni mafuvu tu...

Na kila baada ya mwezi wanachukuliwa wafungwa kadhaa wanapelekwa kuongeza nguvu(escoter)....
Ili ubaki inatakiwa uhonge 100k kila inapokuja escoter..,asikwambie mtu huwa wanalia watu(hawataki kwenda na hela ya kuhonga hawana) kama watoto muulize mtu anaepasikia ngwala akwambie..

NB:LILIJENGWA NA WAKOLONI KAMA MAXMUM SECURITY KIPINDI HIKO...kwa wafungwa wasumbufu..
Mmh
 
Chanzo cha 2Pac kumdiss Chino XL

2Pac alienda Jela nyuma Chino XL akatunga ngoma inaitwa Riiiiot ndani hio ngoma anasema "siwezi kwenda Jela nisije nikabakwa km 2Pac"

Pac alipotoka Jela na kuzinguana na Biggie ambae aliiba idea ya ngoma Get Money kutoka kwa 2Pac kupitia Faith Evans ambae alivujisha ujio wa hio ngoma ya 2Pac, Junior Mafia wakafanya Get Money ikatoka Pac akachukia akaita kikosi chake akafuta lyrics zote original za Hit Em Up akaandika lyrics mpya za diss track na katika hio diss track mwishoni anasema "Fack Chino XL" sababu Chino XL alimuimba kua 2Pac alipokua Jela alitatuliwa Malinda kinguvu yaani alibakwa na wazee wa Jela

Jela sio kuzuri
Ile ni best diss track in my whole life ni motoooo
 
Umenikumbusha jamaa yangu alipelekwa escoter Gereza la MAWENI(MUUWENI),,alikua anaitwa john me nlipenda kumuita FIDEL CASTRO...Alinunua redio(hatukujua kaitoa wapi wala betri ananunuaga muda gani)..

kesi zetu zilikua zinafanana japo yeye alitenda kweli,,

analalia magodoro ma3,halafu sio nyapara kila ikifika saa 8 usiku,ananipigapiga begani halafu ananiambia "JAMBAZI MIMI NAWASHA REDIO" Halafu anawasha tena sauti mpaka mwisho...

alikua anapigwa muda wote na anashinda na minyororo,wakampeleka MAWENI(Tanga)...atakua alikufa na kama mzima haji kuwa na familia sio kwa vipigo vile...
Duuh
 
Nakumbuka 2019,nilikua mahabusu pale ISISI gerezani,sasa wakati tunasubiri kupewa jezi(zile za orange) na kukaguliwa,TV ilikua imewashwa tunaangali kuna jamaa alikuja dirishani akasema.

"rasta rasta huo umeme wa magufuli rasta haaya,mtaulipia rastaa"
aliongea kwa uchungu na tuliulipia kweli dadeki..
Toka lini mahabusu wakapewa jezi?!
 
Back
Top Bottom