Uzi wa kufundishana maisha ya Jela na selo

Uzi wa kufundishana maisha ya Jela na selo

Jela usiwe mbabe tii sheria utaishi vizuri utapendwa na askari na wafungwa wenzio.
Ukijifanya mbabe kule ndio kuna watu primitives kuliko wewe.
Ukijifanya unajua ngumi kule kuna watu ni walimu wa ngumi utakula ngumi hadi uombe poo.
 
Pana mtu nilimsikia akisema. Jela huwa haina wafungwa wapya bali ni wale wale wanajirudia tu. Anamanisha jela ni roho yaani kama kwenye ukoo pana mtu keshawahi kaa jela possible ya kuingia jela, lakini kama Hakuna historia ya ndugu kuwepo jela ni ngumu kuingia jela.
Anaweza akawa kweli thus kwa wengi ukitoka jela uruhusiwi kuingia ndani ya mji wako au wenu bila kutakaswa kuondolewa mikosi ikiwemo vitu vyako ikiwemo nguo kuchomwa moto, kuoga na kwenda kusomewa dua au maombi. Huku unalala nje siku tatu, ndipo unakaribishwa nyumbani kwako.
 
Chanzo cha 2Pac kumdiss Chino XL

2Pac alienda Jela nyuma Chino XL akatunga ngoma inaitwa Riiiiot ndani hio ngoma anasema "siwezi kwenda Jela nisije nikabakwa km 2Pac"

Pac alipotoka Jela na kuzinguana na Biggie ambae aliiba idea ya ngoma Get Money kutoka kwa 2Pac kupitia Faith Evans ambae alivujisha ujio wa hio ngoma ya 2Pac, Junior Mafia wakafanya Get Money ikatoka Pac akachukia akaita kikosi chake akafuta lyrics zote original za Hit Em Up akaandika lyrics mpya za diss track na katika hio diss track mwishoni anasema "Fack Chino XL" sababu Chino XL alimuimba kua 2Pac alipokua Jela alitatuliwa Malinda kinguvu yaani alibakwa na wazee wa Jela

Jela sio kuzuri
Yap man jela hawaangaliii jina
 
Mfungwa anakua msaidizi(kama 20 hivi)..
Hawawezi kuwaacha mpike mnaweza kuweka FORODANI...

Ila kama unajua kukanda maandazi/kuchoma chapati ndo afadhali yako
Mkuu, sehem nyingi kwenye wafungwa hua naona manyapara wanavonyanyasa wafungwa. Hasahasa kwenye kazi ngumu, unakuta nyapara anatembeza mjeledi hatari kwa wafungwa.
JE hawa jamaa, hua inatokea wanashushwa vyeo na kurud kuwa wafungwa wa kawaida, au ukiwa KIHEREHERE n kazi ya kudumu?
Na if wanashushwa vyeo, he wakirudi chini maisha yao yanakuwaje?
 
Ukiweza ishi jela za bongo huwezi shindwa ishi jehanamu
"Na sema: hii ni haki itokayo kwa mola wenu, basi anayetaka aamini na anayetaka na akufuru, hakika sisi tumewaandalia madhalimu moto ambao zimewazunguka wao kuta zake {wamefungiwa}, na wakiomba msaada watasaidiwa kwa kupewa maji kama shaba iliyoyeyushwa, yatakayowababua nyuso zao, kinywaji hicho ni kiovu mno! na matandiko maovu mno ya kupumzikia ni hayo!."

Qur'an 18:29

Mkuu usifananishe jahannam na vitu vya ajabu, lau ungeijua maana ya jahannam ungelia umri wako wote wala usipate furaha katu.

Nb: sijaja kuharibu uzi nimetia neno tu.
 
Pana mtu nilimsikia akisema. Jela huwa haina wafungwa wapya bali ni wale wale wanajirudia tu. Anamanisha jela ni roho yaani kama kwenye ukoo pana mtu keshawahi kaa jela possible ya kuingia jela, lakini kama Hakuna historia ya ndugu kuwepo jela ni ngumu kuingia jela.
Anaweza akawa kweli thus kwa wengi ukitoka jela uruhusiwi kuingia ndani ya mji wako au wenu bila kutakaswa kuondolewa mikosi ikiwemo vitu vyako ikiwemo nguo kuchomwa moto, kuoga na kwenda kusomewa dua au maombi. Huku unalala nje siku tatu, ndipo unakaribishwa nyumbani kwako.
Niliishia maabusu, mule ndani nilimkuta mzee mmoja ana kesi ya kumpiga mkewe, cha ajabu mkewe huyo huyo aliempiga ndie aliemletea chakula usiku...

Mimi sikukaa sana nilitolewa nikarudi home issue ni kwamba kuna mtu nilimpiga nusura nimuue akaja central akaombwa na polisi tukamalizane nyumban maana kesi ikienda mbele sichomoki ndio akakubari yaishe nikachangia matibabu tukayaongea tukasameheana yakaisha nikarudi home nikamwacha yule mzee kule maabusu, kwanza mule ndani maabusu hakufai je huko jela ndani kuna hali gani?
 
"Na sema: hii ni haki itokayo kwa mola wenu, basi anayetaka aamini na anayetaka na akufuru, hakika sisi tumewaandalia madhalimu moto ambao zimewazunguka wao kuta zake {wamefungiwa}, na wakiomba msaada watasaidiwa kwa kupewa maji kama shaba iliyoyeyushwa, yatakayowababua nyuso zao, kinywaji hicho ni kiovu mno! na matandiko maovu mno ya kupumzikia ni hayo!."

Qur'an 18:29

Mkuu usifananishe jahannam na vitu vya ajabu, lau ungeijua maana ya jahannam ungelia umri wako wote wala usipate furaha katu.

Nb: sijaja kuharibu uzi nimetia neno tu.
[emoji419][emoji419]
 
Back
Top Bottom