Mkuu , ukitaka kujua uhalisia wa hili , wewe fuatilia SIRI nyingi muhimu hutazikuta ONLINE.
Wengi walioko online wanapuyanga tu huku wakiishi kwa "Guess work".
Kuna lundo la watu wanafanya Kazi TANESCO, TBA, TBS, TMDA, TAKUKURU, NGORONGORO, KADCO, TISS, JWTZ lakini Kuna taarifa ukizitafuta, nyingine hata siyo Siri kiviile Kama vile mishahara na nafasi za kazi huwezi kuzipata.
Lakini hayo mashirika Yana Watumishi wengi mnooona wapo online.
Mimi Kuna kipindi, nilienda kwenye shirika fulani nikakuta wanalipana vizuri sana na walikuwa wanaajiri hata watu wasio na elimu kabisa.
Lakini Mambo Kama hayo huwezi kuyakuta online.