Uzi wa kupeana ramani za machimbo ya dhahabu yaliyolipuka/yanayolipuka na fursa zinazopatikana porini/chimboni

Mrangi natamani kujia mengi, cama hutojali njoo inbox, unijuze mengi
 
kizuri kula na wenzio na mungu atakubaiki...leo kwangu kesho kwako, utajisikiaje?
 

Kwenye jiwe ulikua umepotea, kwenye dhahabu haulali njaa, jiwe waachie akina marley dollars, na mbunge wa ulanga hisham, japo mpigo wa jiwe moja ni dhahabu kilo kadhaa, hapo saka mchongo wa kuuza dubai mwenyewe na uwe makini na wanigeria na warabu wapigaji ukiweza kufika Canada na Australia ndio ukauze huko tafuta michongo tu, dhahabu ndio pesa ya dunia hongera mzee kubadili uelekeo
 
Mtoa mada umefanya vzr sana,uwekezaji kwenye biashara ya dhahabu unatija sana lkn,changamoto ni kwamba wachimbaji wengi siyo waaminifu,kuna mambo ya kulogana,kuzungukana (kwa mfano kuna jamaa yangu aliwahi kubadilishiwa carbon akiwa plant na mwana-share mwenzake)

Vilevile changamoto nyingine ni mitaji ila,tuendelee kupambana bila kukata tamaa.Kwa tahadhari kama una mtaji usikimbilie kwenye machimbo mapya...kwa mtu mwenye mtaji mdogo hata mtaji mkubwa nenda kwenye sehemu ambayo watu wengi wanaikimbia huko dhahabu za vikole hazipatikani lkn,kwenye senga unatoboa vzr sana jambo la msingi ni kuhakikisha unalipima senga lako kwenye kila hatua!
 
kila kitu kinachangamoto kikubwa kuwa na elimu ama ujuzi wa kile unachotafuta.
 
Machimbo yako mengi na yana dhahabu yenye ubora mzuri tu.... Tuendelee kupiga pesa taratibu.
 
Huwa natamani kufanya ngumu za nguvu kama hizi ila siiamini sana afya yangu na wala sina nguvu kivile. Naweza beba vifusi siku nzima, nikalala siku mbili kwa uchovu
Unajidanganya mkuu, kwenye tasnia ya dhahabu hata mtu anaeumwa presha, kisukari na mengine anaweza kufanya as long as anaweza tu kutembea, kuongea na kulala mazingira fulani ya guest za mabati (kama huma uwezo wa kulala pazuri).

Kule **** mgawanyo wa majukumu na sio kubeba vifusi kama unavyodhani.

[emoji1428]Wachimbaji na Wachorongaji (hawa ndo wanahitaji nguvu sasa), kwakua wanazama kwenye mashimo kutindua na kulipua mikanda ya dhahabu.

[emoji1428]Wamiliki wa crusher na mialo hawa hawahitaji kuwa na nguvu yoyote ile, kazi yao ni kusagisha mawe yanayosadikika kuwa na dhahabu ili kupata unga ambao utaoshwa ili kuichambua dhabu hapo mwaloni.

[emoji1428]Makota hawa nao hawahitaji nguvu yoyote ile maana kazi yao ni kununu dhahabu kutoka kwa wachimbaji kisha wanaenda kuiuza jikoni.

[emoji1428]Deallers Uwe na pesa ya maaana tu (nimesema Pesa kweli).

[emoji1428]Kimiliki Plant.
 
Mwamba nipe connection japo pm
 
Mine the miners..

#MaendeleoHayanaChama
 
Lindi, Ruangwa, Nanganga, Mbecha etc
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…