Uzi wa kupeana ramani za machimbo ya dhahabu yaliyolipuka/yanayolipuka na fursa zinazopatikana porini/chimboni

Uzi wa kupeana ramani za machimbo ya dhahabu yaliyolipuka/yanayolipuka na fursa zinazopatikana porini/chimboni

Naomba taarifa kamili
Mwanzoni dhahabu ya kule ilikuwa ya shikole, hivyo kwa sasa hadi kuna karasha mnasaga fero?

au bado mnapiga hio sesa ya shikole?

na kama mnasaga wastani kwa mfuko mmoja mnatoa gm ngap?
Ni sesa za vikole man,Ila kuna muda palisimama kimtindo kutokana kuna ajali ilitokea watu wakafa ila sahivi ni kawaida wanachimba
 
Nimefanya sana ila haikuwa na faida, uwekezaji mkubwa ila mmmmh
 
Nmeingia rasmi kwenye hii biashara ya dhahabu,jiwe nmeliweka pembeni nna miezi 4 sahv huku,sema mleta uzi utanisamehe chimbo langu.

Kwa sasa sitoliweka wazi maana,sitaki kuwaamsha waliyolala

Ila dhahabu nayoigumia huku purity yake inagonga 98%


Ova
Mi najua soko lake ambao utauza bei nzuri sana mpaka useme basi tena nikikuungisha hutonisahau maishani
 
Nitajieni chimbo lenye amsha za kutosha niwaletee pombe huko na spirit
 
Uzi mzuri sana huu hongera, ila mtoa mada Msalala sio Wilaya ni Halmashauri na jimbo la uchaguzi tu.
Wilaya ni Kahama.
 
Habari za wakati waponchaji na madigala na watu wengine, tumain langu mnaendelea vyema na kijiti cha utafutaji na bwana anaendelea kubariki kazi ya mikono yenu.

kama uzi unavyosema ni mahususi kutaja maeneo ambayo wachimbaji wadogo dhahabu inapatikana kwa wingi kwamba yeyote atakaye thubutu kwenda uhakika wa kupata riziki uwepo.

Wengi hatuwezi kua na mawaasiliano ya moja kwa moja na watu walio porini kwa maana porini wakati mwingine mitandao hua haikamati vizuri. Hivyo kupitia uzi huu uwe msaada kwa wahitaji, wataffutaji wa dhahabu maana najua maisha ya kutafuta dhahabu ni kama ndege wakisikia sehemu imehila mda huohuo watu wanasafiri.

Naanza mimi mkoa wa shinyanga wilaya ya msalala kata ya nyamishiga machimbo ni nyamishiga yamelipuka miez kama 6 iliyopita lakin uzalishaji bado ni mkubwa sana na watu bado wanahila nimeshuhudia kwa macho watu walisaga mfuko mmoja wa mawe wakakamua 72gm.

Hivyo nawakaribisheni kutujuza mliyonayo.
 
Nawaiteni wawekezaji wazawa , karibuni tujadili. July 2023
 
Back
Top Bottom