Na mimi ngoja nichangie Uzi kama ilivyo tokea katika familia yetu japo wahusika niliowapa ramani walikuwa hawaamini haya mambo lakini badae walikuja kuamini
Mwaka 2021nikiwa mkoa wa kigoma, wilaya ya kibondo nikipiga michakato kwenye shirika x la wakimbizi, nilipata taarifa ya msiba wa uncle wangu tumbo Moja na mama. Nilijiandaa kulejea Kanda ya ziwa ambako ndio ndio nyumbani.
Tukio linaanza kama hivi, maleemu ambae ni uncle wangu aliwaikuwa na mgogoro na jamaa flani ambae walikuwa wakipiga mishe zao pamoja, lakini inaoneka, uncle uncle alikopa ela za jamaa na akawa ameweka Hati ya nyuma Kwa jamaa. Basi jamaa akawa anadai pesa yake lakini uncle hakuweza kumlipa, walivutana sana maana uncle nae alikuwa yuko fiti Kwa waganga. Basi siku zimeenda yule jamaa akaenda kufungua kesi mahaakamani Kwa vile alikuwa na pesa uyo jamaa alionga mahaakamani, mahakama ikatoa kibali Cha nyumba kuuzwa.
Ni story ndefu sana siwezi elezea yote, ni kwamba baada ya uncle kuwa ameugua na kufaliki kesi ilikuwa Bado Iko mahaakamani na nyumba ilikuwa lazima iuzwe, Kumbuka nyumba ipo mwanza town sio Kijiji. Sasa baada ya maziko kikao Cha familia kilikaaa, kumbuka kwenye uko wetu wengi wao ni watu wa dini sana Hadi watoto wake, sema Kuna dogo mmoja kwenye familia ni mwanaharakati na ninamkubali. Kikao kilitoa mapendekezo ya kutafta mwanasheria asimamie Ile kesi, lakini Mimi niliona iyo kesi ilikuwa ni nzito na lazima nyumba ingeuzwa. Baada ya kikao kumalizika Mimi niliwachukua vijana wa malehemu nikawaweka chemba nikawauliza, hivi Ili jambo mnalichukuliaje na hapa mkicheza nyumba inaenda.
Mkubwa akunielewa maana nae ametanguliza usomi sana na anakaa uko Dsm, mdogo alinielewa ni Teacher akaniambia brother Mimi nimekuelewa sasa tunafanyaje? Nilimwambia nyie ndo vijana wakubwa lakni mbona amuelewi kwaiyo nyumba ikiuzwa mtakaa wapi?
Kumbuka kipindi hicho maombolezo Bado yanaendelea, Mimi ilinibidi nirudi kigoma nikamwambia dogo ngoja niende tutawasiliana nitakwambia jambo, basi nilivofika kule Kuna Mzee mmoja wa kiha alikuwa na kijiwe Cha kahawa, siunajua tena mkishatoka mtingoni ni kwenda kuchuli kwenye kahawa. Sasa bandugu baada ya kumuelezea Mzee mkasa mzima wa marehemu mjomba na Hadi kesi ilipofikia nyumba kuuzwa, Mzee aliskitika sana na akasema kwaiyo nyie kama familia mmekubali nyumba kuuzwa?
Nikamwambia ndo maana nimekueleza unipe Mawazo tufanyeje, Mzee akuniambia Kuna mtu nitakuelekeza uende, uyo ni mtaalamu wa mambo ya kesi, napiga hata kama unataka jirani Yako kuhama na kuuzia eneo lake ni kazi raisi Kwa uyo mzee. Ilibidi anielekeze, Kwa menyeji wa Kibondo ukiwa kibondo mjini, ni kilo mita chache tu unafka kwenye icho kijijini Barabara ya kwenda kasuku. Ndugu zangu sikuamini baada ya kufika pale, Yani nilikuta watu wakubwa na matajiri ya kisukuma kutoka uko bariadi, Kahama NK.
Kwa siku iyo sikufanikiwa kuonana nae kwani alikuwa na kazi nyingi ilibidi nilale Hadi kesho yake saa saba mchana nikafanikiwa kuingia chumba Cha kazi.
Baada ya kuingia nilijitambulisha na ndipo aliset radar na kuanza kuangalia, kile alicho kusema ni kweli na alisema hata kifo Cha mjomba wako si chakawaida uyo jamaa amemzidi nguvu, kwaiyo anacho pambana sasa nikuchukua nyumba na kati ya watoto wa marehemu atakae jitokeza kufatilia iyo kesi nae ataenda na maji.
Kwaiyo nilimuuliza tunafanyaje sasa Mzee, aliniambia kazi inawezekana lakini anatakiwa kati ya mtoto wa wa marehemu Kuna zindiko anatakiwa kulifanya Kwa niaba, maana hapo nikiangalia nyumba uyo jamaa amezika vitu vizito tayari kuteka iyo nyumba, hivvo ni lazima tambiko la kusafisha mji lazima lifanyike na kuzika dawa Kingo zote za mipaka na katikati ya mji na dawa za kuoga mhusika atakae simama kama familia na maelekezo mengine. Alisema Kwa vile ni mbali itabidi umlipie kuja wangu nauli ataenda kufanya iyo kazi lakni Kuna vitu mnatakiwa mkanunue huko, aliniambia vitu vya kununua na nilimpigia simu bwana mdogo nikwambia aviandae na sisi tungekuja siku inayofuata.
Siku iyo tulifika rock City mnamo majira ya saa kumi lakini kazi yenyewe ilitakiwa ifanyike saa tisa usiku bila kukosea time, ilibidi tufikie lodge kwanza maana kazi Ile hakutakiwa mtu mwingine kujua. Ilibidi nimuite dogo aje lodge akapewa maelekezo ya kufanya, dogo akaenda kuandaa mazingira na vitu vilivyoitajika katika zoezi, kumbuka kazi iyo inafanyika mhusika lazima Kuna dawa anaoga nje akiwa uchi na akifanya manuizi.hatari.
Kukatisha story ni kwamba nyumba Hadi Leo ipo na kesi mahakama ilifuta na aliekuwa ana dai hajulukani alipo, sijui alikufa au vipi.Dogo anashukuru Hadi Leo japo wanafamilia hawajui, ninaejua iyo issue ni Mimi na madogo hao wa kiume tu, ingawa yule msomi wa Dar alikuwa anapinga lakni sasa ivi anakubali na mambo yake sometime ananishirikisha Nampa Mawazo. Hata na Mimi ni muumini lakini sometimes unaangalia na upepo.
Kigoma uchawi upo na yule Mzee ninamkubali kinoma, Wenyeji wa Kibondo uyo mzee mtakuwa mnamjua, Barabara ya kwenda kasulu, kijijini Cha kwanza kabisa ndo alipo. Ova.