Uzi wa kushuhudia mazuri ya kwenye ndoa, Tuyaweke pembeni yale mabaya yanayowatia hofu watu wasioe au kuolewa

Raha ya kuwa na mwanamke wa pekee yako na anayehishimu ndoa ni pale unapotafuta pesa, ukiwaza kwenda kuzitumbua halafu ukakumbuka mkeo yupo nyumbani na anakutegemea wewe, unajikuta tu unakwenda nyumbani na kuketi nae mpange maswala yenu ya maendeleo pesa haipotei.

Ukiwa na mke wako, usiku unajua yupo pembeni yako, sometimes, ile moment umegeuka usiku unamuona kalala pembeni yako... Dah ile feeling asikwambie mtu.

Pia kuna ile moment umerudi kutoka kwenye mihangaiko, unafika home unakuta chumba kisafi, harufu nzuri ya chumba, kitandani mashuka uliyoacha hayapo, kuna shuka mpya safi zimetandikwa, halafu mkeo yupo jikoni anamalizia kukuandalia chakula ili mle. Dah hivi naanzaje kupata nguvu ya kutoka nje tena na nipo na my best friend hapo ndani?!

Kitu kingine kuhusu ndoa, mwanamke ukipatia wa kuwa nae anaekusikiliza, huwa kuna raha sana kuketi nae na kuzungumza maisha pamoja. Unaona upo na mtu ambaye hana pa kwenda ameweka maisha yake kwako sasa anakusikiliza maagizo, amri, ushauri na maelekezo yako sababu wewe ndie amiri jeshi mkuu wake. Huyu mwanamke wa hivi, ukitoka nae out, especially kwenye mgahawa wa hadhi ya juu na utulivu , mkiwa m'metulia utaona raha yake unapokuwa nae hilo eneo, kuna ile moment anakupa attention na wewe umempa attention. Mnatazamana mnaongea mambo yenu.

Aiseeeeeee hebu acheni uhuni mbwa nyie oweni na nyie wengine mnaodanga muache huo upuuzi tulieni na mtu wa kueleweka mtakuja kusema hapa siku. Mahusiano ya ndoa yana raha yake. Mwanamke utavaa mavazi yote ya bei ila la gharama na la hadhi ya juu kuliko yote ni vazi liitwalo MKE WA MTU. Hili vazi aisee hili vazi....acha tu..... Wanaolivaa wanajua thamani yake.

Imagine wewe mke wa mtu, wakati wenzio wanahangaika kipindi cha mvua, kuita uber, kugombania daladala, wewe mumeo anakwambia nisubirie tu hapo mlangoni, anakuja na gari hata kama ya kuazima, anafika na mwavuli anakuchukua hao mnakwenda nyumbani. Acha banaaaaa acha kabisaaaaa ndoa especially kipindi cha ujana ima raha sana....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Imagine umekwama pesa. Ukigeuka ukamwambia mume wako unashida ya 50,000 fasta amekupatia. Bila kuitwa gest ukagongwe wala kutumika kimwili kokote kule....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Halafu kuna mambo mengine yaani mpaka upate ruhusa ya hubby, au mpaka ushauriane na hubby, kwa hiyo hata mashost hawawezi kukulazimisha wanajua kwamba you are under someone, kuna raha yale bana
True. Mume au mke ni watch dog wako. Unaweza kutaka kutoka ukafanye upuuzi ila mke au mume ni malaika wako wa ulinzi, utaona tu amekataa usiende....

Maana anajua baya lolote likikukuta basi na yeye atadhurika...... Dah jamani raha sana kuwa katika ndoa...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ila wanaume jamani! Hivi jiulize mlivokua mnaishi kabla ya ndoa ma sasaiv ni sawa? Unakuta mwanamke ana watoto shughuli zot3 za nyumbani toka asubuhi hadi jioni zinamtazama yeye wewe ukiombwa hata kusaidia kuogesha mtoto unanyanyua mabega kama roboti [emoji35] alafu jioni nimechoka zangu hoi uanze kunishika shika nakupiga ndosi hadi utoke damu puani, Mapenzi ni pamoja na kuhurumiana na kusaidiana tena mwingine unakuta wote mnafanya kazi na ukirud nyumbani unafanya majukumu ya home yeye amekaa miguu juu kashikilia rimoti akila hata sahani yake hasogezi, hizo genye nazipata saa ngapi...kwakweli kama mnaona solution ni kutafuta michepuko tafuteni na muhamie huko milele [emoji57]

Sent from my SM-A205F using JamiiForums mobile app
 
😺😺😺😺😺 sasa kumbe mnajua pekeenu hamtuwezi ila tukigonga nje mnakasirika..Hebu acheni mambo ya kitoto basi
 
Ona sasa umeshaanza malalamiko ya kuleta gundu kwenye ndoa. Mada inasema tuongee mazuri.... Wewe umekosa mazuri... Khaaaaaaaaaaah

Sent using Jamii Forums mobile app
 
True
 
Hahaha daah kweli ninecheka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…