Uzi wa kutoa Maoni Juu ya Taasisi Zilizoshindwa kusimamia Misingi ya kuundwa kwake hivo unatamani zifutwe.

Uzi wa kutoa Maoni Juu ya Taasisi Zilizoshindwa kusimamia Misingi ya kuundwa kwake hivo unatamani zifutwe.

Habari wana bodi.

Kutokana na Anachoendelea kukifanya Trump huko USA, Nimepata tafakuri ya hapa kwetu Tz.

Tuko na baadhi ya taasisi zilizo shindwa kabisa wazi wazi kutekeleza matakwa ya kuanzishwa kwake hivyo ni sawa na hakuna.

Uzi huu ni wa kupendekeza hizo taasisi, Na kupendekeza zifutwe au ziundwe upya pindi uongozi unapo badilika.

Mimi naanza na TAKUKURU, Taasisi hii ilianzishwa kwa mlengo wa kuzuia na kupambana na Rushwa nchini, lakini kadri siku zinavozidi kwenda ndio hali inazidi kua mbaya, Rushwa imetamalaki wazi wazi lakini jamaa wapo tu hata kuwasikia hakuna, wamebaki tu kuonea vidagaa sijui waalimu na madaktari lakini wahusika wa kuu wa rushwa hata hawabuguziwi.

Sasa unabaki kujiuliza kuna manufaa gani ya kua na hii taasisi, hatuoni kama ni matumizi mabaya ya kodi zetu, niwakati sasa hii taasisi ifutwe au iundwe upya.

Taasisi ya pili TBS, Jawa jamaa ni wadhibiti ubora wa bidhaa zinazo uzwa katika soko la Tanzania, Wamepewa jukumu lakujakikisha bidhaa zinazo ingia sokoni zina kiwango stahiki, lakini huko masokoni hali ni mbaya bidhaa feki zimetapakaa kila kona hakuna wanacho fanya, Wito wangu hii taasisi ifanyiwe maboresho, ikiwezekana iwe funded vya kutosha ili iweze kutimiza matakwa ya kuanzishwa kwake.
Tubadili mfumo wa utawala.

Tbs kama iwemeza kufungua ofs za kanda pekee kama imefanikiwa.

Nini kifanyike.

Ni madaraka mikoani/kanda.

Tubadili mfumo wa utawala kutoka mfumo wa serikali kuu na hadi mfumo wa serikali za majimbo yenye uhuru zaidi wa kujiamulia mambo yake wenyewe. Ambapo taasisi kama hizi ulizozitaja ziwe chini halmashari/ federal gov.
 
Policcm
Bunge mbwa koko
Takukuru
Tiaraei
Jay K. Tea
Eitsielo
Ewura
Tanesco
Hizi bodi za mikopo, sukari, nyama, maziwa na ushenzi mwingine wa aina hiyo.
Wizara ya Elimu
Wizara ya Sayansi na Teknolojia.
Braza la mitihani.

zipo nyingi sana
 
taasisi ya kwanza ilipaswa kuwa ccm.
sidhani walio anzisha TAA kisha ikawa TANU na sasa CCM walikua na dhamira ya kuwa taasisi itakayo kuwa ya kifisadi na kimafia namna hii.
 
Tubadili mfumo wa utawala.

Tbs kama iwemeza kufungua ofs za kanda pekee kama imefanikiwa.

Nini kifanyike.

Ni madaraka mikoani/kanda.

Tubadili mfumo wa utawala kutoka mfumo wa serikali kuu na hadi mfumo wa serikali za majimbo yenye uhuru zaidi wa kujiamulia mambo yake wenyewe. Ambapo taasisi kama hizi ulizozitaja ziwe chini halmashari/ federal gov.
Hata mimi naamini hivi.

Kwa sababu hata Muungano utakua stable, as Zanzibar kama zanzibar litakua jimbo lenye serikali yake na kuamua mambo yake
 
Policcm
Bunge mbwa koko
Takukuru
Tiaraei
Jay K. Tea
Eitsielo
Ewura
Tanesco
Hizi bodi za mikopo, sukari, nyama, maziwa na ushenzi mwingine wa aina hiyo.
Wizara ya Elimu
Wizara ya Sayansi na Teknolojia.
Braza la mitihani.

zipo nyingi sana
😃

Tutabaki na TISS tu sasa
 
Back
Top Bottom