Uzi wa ma-lastborn tu

Uzi wa ma-lastborn tu

Nilishawahi kuchezeshwa kichapo Cha mbwa koko na bro kisa sijaosha vyombo😂😂
Siku nyengine sijui nilifanyaje akanikurupua usiku ati anitwike mimboko ila limboko lenyewe lile halikuwa fimbo lilikuwa ni likuni nikaona ngoja nitumie nafasi yangu ya uziwanda imtese usiku huohuo nikakimbia kusikojulikana!! Kwani palilalika ni kunitafuta bi maza alimtukana kila tusi halafu wanaenda mpk mbali kunitafuta wkt mhuni nimejibanza jirani nawasikia tu😂😂

Mziwanda Mimi nilikuwa mmwaga kojo hatari siku moja sista akanifungia kazi asubuhi tu nishachafua mashuka wacha anitimue nikiwa uchi mi nachekelea najiuliza huyu sister leo mbona kanigeukia halafu anambio utafikiri Hussein bolt!! Kanikamata kafura kunipiga hata hajanipiga wala nini moja kwa moja mpk bafuni ati nifue mashuka!

Ndo kwanza nilikuwa natabasam maana kufua nilikuwa sijui wkt huo njemba nyengine zipo mlangoni zinashangaa tu akaja bi maza zote zikapisha akaingia akafua😂😂 na kojo liliendelea kama kawa haswa ninywe ile mi juisi kola ulikuwa unanukia mkojo wa kishenzi ule! Halafu hata waniwekee makaratisi ati kojo lisifike kwenye godoro wapi kojo lile lilikuwa na ufahamu litapata upenyo tu😂😂

Uziwanda una tabu zake na raha zake
 
Last born Wote Was*ng* tuu
Njooni Mnipige Nipo Nyumbani
.
.
.
.[emoji38][emoji38][emoji38][emoji13][emoji13][emoji13]
 
Tunatumwa Sana
Mimi nadhani Ni housegirl wa dada zangu..ikafika muda nikawa mkali maana nilikuwa naendeshwa Kama gari bovu.

Unakuta unaagizwa kitu dukani,unajrudi Mara unaambiwa tulisahau hiki nenda Tena...Mimi nilikuwa nawaambia ukiona umenituma kitu ukasahau kngine Basi uende mwenyewe.

Sent using Jamii Forums mobile app
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Mie nilikuwa nalia.
 
Nakumbuka siku moja nalala chumba kimoja na bro kitanda double decker bro akaniweka chini kisa feni haifiki Kwa hiyo kuna hiyo, alikuja kuangushwa huko juu na mm nikapandishwa kwenye feni nikaanza kumcheka mzee alivyoondoka aliishia kusema nikipanga hutokaaa na mm
View attachment 1384357
Lastborn wana raha utasikia mwacheni mtoto
Hata akiwa mkate mzima wengine mkose hata hafokewi sasa kula wewe ambae wa pili kuzaliwa utaona cha mkutema kuni [emoji2][emoji2]


Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
pumzika kwa amani mdogo wangu ....jana tuu nilikukumbuka , wakati nasikiliza wimbo wa Maroon 5-Memories , nawish ungekuwepo na mimi ningekuwa ninavimba kuwa na kabeauty sibling ,
Mama , kaka zako na dada yako Tumekumiss sana unaishi mioyoni mwetu Forever
Pole sana mkuu.
 
Hii ilishawahi nikuta Mie, Madada wote wapo boarding na wengine waliolewa.

Aisee hakuna kazi ambayo sikufanya:Kupika,Kuosha vyombo,nashukuru ilinijenga...

Japo walivyokuwa likizo nilikuwa nawalipa kila kazi wafanye wao mie nageuka mhindi tu..!!(Kula na kulala)
Usiombe ukutane na last born wa familia yetu. Ni wa kiume na anajua hadi kupika chapati.
Unaleta mchezo nini, umezaliwa dada zako wako boarding school na wengine tumeolewa. Na vile wazazi wameamua asome day kwa sababu ni katoto ka mwisho msoto wake si wa kitoto.

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom