Uzi wa maswali kwa Rais wa TFF, Bw. Jamal Malinzi


Serikali ndiyo nguzo muhimu kwenye Youth development,TAMISEMI hususani ndo wanatakiwa wawe vinara wa ajenda hii kama wasimamizi wa shule za msingi.Youth football development plan tunayoiandaa itawasilishwa serikalini ili kwa pamoja tuifanyie kazi.In my opinion bila mpango endelevu wa kulea na kukuza vipaji tusahau world cup.Alliance Mwanza nawashukuru hawana masikhara, they walk the talk,siku ukifika Mwanza tembelea pale.
 
Ndigu Malinzi, kwanza nakupongeza kwa kushinda kiti cha Urais wa TFF,
Nina swali langu dogo tu kuhusu wachezaji wa kigeni, je utaratibu tuliotangaziwa kuwa wachezaji hao wataruhusiwa watatu tu kwa klabu, uongozi wako unauafiki?
na nini athari za kuwa na wachezaji wa kigeni kwa wingi?
 
Ndugu na jamaa yangu Jamal Malinzi, we ni shuhuda wanawake angalau wanatutoa kimasomaso kwenye match za kimataifa, japokuwa hatuna ligi wala timu zenye hadhi. Mpango ukoje kuhakikisha soka la wanawake linakua?
 
Last edited by a moderator:

Ngolombwe this is a two edged sword,upande mmoja unataka wachezaji wa kigeni wawe wachache ili wa kwako wapatw fursa ya kucheza na kukuza kipaji,upande wa pili ligi lazima ichangamke na ivutie public,sponsors na advertisers,wachezaji wa kigeni wanaongeza hii ladha na kupandisha hadhi na ushindani wa vilabu kwenye ligi.Inabidi kupata uwiano (balance).Sasa je hiyo balance ni wachezaji wangapi wa kigeni kwenye ligi?
 
Last edited by a moderator:
Ndugu na jamaa yangu Jamal Malinzi, we ni shuhuda wanawake angalau wanatutoa kimasomaso kwenye match za kimataifa, japokuwa hatuna ligi wala timu zenye hadhi. Mpango ukoje kuhakikisha soka la wanawake linakua?

Ndugu yangu Asprin mambo matatu makubwa tunayahangaikia kuhusu women football na ninaamini tutafanikiwa punde:
1.kuanzisha ligi ya vilabu vya wanawake
2.kuanzisha taifa cup ya wanawake
3.kuingiza watoto wa kike kwenye youth programmes nao wafundishwe mpira wakiwa wadogo.
TFF tumeamua pamoja na ufinyu wa bajeti kila mashindano ya kimataifa ya wanawake tutaingiza timu ili tupate uzoefu,leo tumejisajili All africa games Congo brazaville 2015 tunaingiza timu ya wanawake na CAF tumewafahamisha rasmi.
 
Last edited by a moderator:

Kwa hili ntawatakieni kila la kheri, kama ambavyo unajua mie na wanawake tuko damdam. Ushauri ningeomba timu za ligi kuu zingekuwa na timu za wanawake, afu ikawepo hata ligi ya mtoano kupunguza gharama. Natamani siku moja nishuhudie warembo wa Simba wakitafuna nyama ya manungayembe ya Yanga. (samahani kama nimekukwaza)
 
Last edited by a moderator:

Wazo zuri la vilabu vya premier kuwa na timu za wanawake,ngoja tulifanyie kazi.
 
Mkuu Malinz Nina Maswal Mawl 1. Vip Kuhusu Rufaa Ya Mpwapwa Staz. Kwan Tunaskia Katbu Wa Dorefa Anae Dai Kuwa Ww N Baba Yake Ameifuta Rufaa Na Kaja Tff Kuchukua Barua Ya Kuwataka Mpwapwa Wacheze Ligi. Hii Ipoje 2. Mnampango Gan Na Kuanzisha Mashndan Ya FA??
 
Electronic ticketing tumeanza ila kwa kweli kwa yaliyotokea leo mkwakwani Tanga itabidi kesho tuchukue hatua za dharura kulinda usalama wa watazamaji wa mpira.Taarifa nilizoletewa leo kutoka Tanga si nzuri.
Thanks for your prompt response.
Ila mkuu ujue yaliotokea siku ile ya mechi kati ya Taifa Stars na Ivory Coast June last year pale Taifa ni aibu tupu, na ni hatari sana kwa walioingia uwanjani na tunaomba isitokee tena. Nimeapa sitohudhuria mechi yoyote tena pale uwanja mpya hadi marekebisho yatakapofanyika, na siku peke yangu tuko wengi sana.
Tickets zikikatwa based on seat numbers, na ikawa enforced itakuwa ni permanent solution ya tatizo hili
 
Kwanza nikupongeze ndugu Jamal Malinzi kwa kuchaguliwa kuongoza shirikisho la mpira wa miguu Tanzania na nikupongeze pia kujitokeza kujibu maswali hapa JF.

Swali langu linahusu mgawanyo wa mapato yanayotokana na viingilio kwenye mechi mbali mbali. vilabu vya Tanzania ndo vinavyomiliki wachezaji na ndo vinavyohangaika kuhakikisha wachezaji wao wapo katika hali nzuri kimwili pamoja na kiakili, kuyafanya yote hayo vilabu vinaingia gharama kubwa sana ambayo ni pamoja na kuwalipa mishahara, posho, kuwatibu wanapougua au kuumia, kuwasafirisha pamoja na gharama ya kambi.
Mashabiki wanaingia uwanjani kwa ajili ya kwenda kuona soka linalochezwa na hawa wachezaji wanaomilikiwa, kutunzwa na kuhudumiwa na vilabu lakini linapokuja suala la mgawanyo wa mapato vilabu vilivyoshiriki kwenye mechi husika vinapata mgawo ambao ni chini ya asilimia hamsini ya mapato yote kitu ambacho mimi nadhani si haki, je TFF ikiwa chini yako, mna mpango wowote wa kupunguza haya makato ya kinyonyaji?

Nitachukua mechi kati ya Yanga na Ashanti pamoja na ile ya Simba na Rhino zilizochezwa wiki iliyopita kama rejea kwenye swali hili.

Mechi ya Yanga na Ashanti iliingiza ≈TZS86.04M, na kila klabu iliingiza kiasi cha ≈TZS 20.65M, ukichukua timu zote mbili zilipata 48.001% ya mapato yote.

Mechi ya Simba na Rhino iliingiza ≈TZS53.82M, na kila klabu ilipata mgawo wa ≈TZS12.60M, jumla timu zote mbili zilipata 46.823% ya mapato yote
.

Kutokana na rejea hapo juu pamoja na maelezo niliyotoa, hivi TFF hamuoni kama vilabu hivi mnaviumiza ukizingatia zenyewe ndo zinaingia gharama kubwa lakini kuna wengine wanapata mgawo bila kutoa jasho lolote? Kwa nini msiweke angalau vilabu husika vipate japo 55%-60% ya mapato yote halafu wale wengine kama malipo ya Uwanja, gharama za mechi, Bodi ya Ligi, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF), Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) wakapunguziwa mgawo wao?
 

Mimi nadhani ili kukuza soka letu na kuifanya ligi yetu iwe bora kabisa katika ukanda wetu huu, vilabu viruhusiwe kuwa na idadi yeyote ile ya wachezaji wa kigeni, ila kuwe na masharti ya hao wageni, kwanza wawe na sifa ya kuwa kwenye timu zao za taifa iwe za vijana au za wakubwa, pili vilabu vyote vya ligi kuu viwe na academies ambazo zitakuwa maalumu za kukuza vijana tena wawe na mpango unaoeleweka wa kitaalamu namna ya kiwakuza vijana hao, na iwepo kurugenzi rasmi ndani ya FA itakayoshughulia maendeleo ya academies hizi chini ya wataalamu wa soka la vijana.
 
Last edited by a moderator:
1.Ni kweli tumewaagiza Dorefa wawambie Mpwapwa stars watches eligible ya mkoa kwa mujibu wa taratibu za Dorefa.Muda wa kutosha ulitolewa Walter vielelezo vya madai Yao mpaya Leo hatujaviona.
2. Kobe la FA linakuja,litaitwa Federation cup.
 
Nakubaliana na wewe asilimia Mia SHERRIF ARPAIO tuna Kazi kubwa ya kufanya katika kukabiliana na changamoto za uingiaji,ukaaji na usalama wa watazamaji uwanja wa taifa na viwanja vingine.
 
Last edited by a moderator:
Lini mtabadilisha jina la timu ya taifa? Hili jina la Taifa Stars halina mvuto na limepitwa na wakati, na pengine lina nuksi ama gundu na huenda ndio maana timu yetu imekwama toka iliporudi Lagos in 1980.
I think it's time now we switch to something else for instance Kilimanjaro or Serengeti ambayo yataitangaza Tanzania kwenye mambo mengi hasa utalii. Just my thought!
Angalia hata Nigeria na Zambia wameshabadili.
 

Nakubaliana na wewe suala la mgao ni tatizo.Kwanza katika hiyo asilimia 52% inayokatwa Serikali inachukua VAT 18%.TFF royalty inayopata (mrahaba) ni sifuri 0% hiyo FDF kwa mujibu wa sheria ni kwa ajili ya miradi ya vijana,maana yake ligi yetu haichangii TFF hata hela ya kununua LUKU.Yote haya yanajadilika ili tutafute formula nzuri ya kumsaidia kila mhusika vikiwemo vilabu.
 
Upatikanaji wa tickets za world cup kule Brazil kupitia TFF kwa watanzania huu ukoje? Ni taratibu gani inabidi nifuate ili niweze kupata tickets ambazo TFF imekuwa-allocated na FIFA?
 

Uko sahihi kabisa ,hilo nasi tumeliona.Kwa sasa tunashughulikia software ili watanzania wote tushiriki kupata jina jipya kupitia mobile networks.Muhimu jina sio tu lihamasishe lakini pia liuze vivutio vya utalii wetu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…