Uzi wa maswali kwa Rais wa TFF, Bw. Jamal Malinzi

1. Je, TFF ina fikiria kwa namna yoyote ile ligi kuu ya vodacom kuwa na timu zaidi ya zilizopo sasa?

2. Kwa sasa viwanja vya michezo hasa vinavyotumika kwa soka na hasa kwa vijana wadogo mitaani vinabadilishwa matumizi kila kukicha na hivyo kuwakatisha vijana tamaa. Je. TFF wana mbinu gani katika kuhakikisha kuwa viwanja hivi vinaendelea kuwapa hamasa vijana.

3. Katika miaka ya hivi karibuni yamejitokeza matatizo ya mechi kubwa kuwa na waamuzi ambao hushindwa kuzimudu. Hata ikitokea maamuzi kutakiwa kuchukuliwa nje ya uwanja huwa yanajitokeza matatizo na malumbano makubwa. Ili kupunguza ama kuondoa tatizo hili, TFF imejipangaje?

The Listener
Ex Detective
 
Nimefurahishwa sana na Mh. Jamal Malinzi, yuko very interactive katika kujibu maswali ya wadau. All the best, timizeni ahadi zenu na kuboresha soka la Tz!!!!
 
Last edited by a moderator:
Ndugu zangu kwa nia njema kabisa ya kujenga nimeamua kutumia muda kujibu maswali na kupokea ushauri.Ninaomba tuulize maswali na kutoa ushauri wa kujenga.Ninaomba tusiongelee watu tuongelee issues,tuangalie ni kwa jinsi gani tutakabiliana na changamoto mbali mbali.
Kuhusu ligi kuwa na timu zaidi ya 14 ni kweli tumeliona na tutashauriana na mshirika wetu vodacom ili tuone tutafanya nini.
 

Jamal Malinzi naomba kujua baada ya mpango mkakati mzuri ambao umeuanza kwa ajili ya kuiandaa timu ya vija na kuweka makao makuu mwanza Alliance Academy,umejipanga vipi katika kuwatumia watu wa mpira wakiwemo waandishi wa habari katika kuitengeneza pia timu hiyo,ukiachilia wataalam ambao umesema watapelekwa mwanza kwa ajili ya kushughulika katika kitikankiyuo hivho?!
 

1 LISTERner la idadi ya timu kwenye ligi nimeliongelea hapo juu.
2.uvamizi wa maeneo ya wazi ni gonjwa sugu nchini mwetu,wanamichezo inabidi tuwe wanaharakati kulinda maeneo ya wazi.Vyama vya mikoa vimeshauriwa vinunue maeneo mapya yanayopimwa na TFF tutachangia kama tulivyochangia Tanga,Mwanza nao wako mbioni kupata.
3.Refereeing ni kwwli ni tatizo lakini na upande wa pili wa shilingi timu nazo zikipoteza mchezo zisikimbilie kulaumu refa.Tunazo program mbili za kulea marefa watoto moja iko Gen Twalipo barracks na nyingine Alliance academy mwanza.
 
Last edited by a moderator:
Tarehe 13 feb nitakutana na wahariri,ulilolisema tutalijadili siku hiyo.
 

Uongozi una changamoto nyingi na wakati mwingine maamuzi yanatolewa kwa faida ya wengi,hiyo ipo dunia nzima.Hakuna atakayepindisha sheria kiholela tu au kwa nia mbaya.
 
Mh. Jamal Malinzi unasemaje kuhusu TFF kujazwa na watu kutoka mkoani kagera hali inayoelezwa kwamba italeta suala la ubaguzi katika TFF kuhudumia mikoa yote ya tanzania na visiwani.

asante mh rais
 
Last edited by a moderator:
Nani mwenye jukumu la kufanya matangozo ya matimizi ya hizi teketi za electronic ni tff au crdb? Manake hakuna matangazo yoyote rasmi zaidi ya watangazaji wa vipindi mbalimbali vya michezo vya radio kutangaza kwenye vipindi vyao
Makampuni mbali mbali au taasisi wakianzisha jambo lao utalisikia likitangazwa kwenye tv, radio, na magazeti kila saa kila siku ili watumiaji waelewe kwa nn nyie hamfanyi au hamkua na bajeti ya matangazo
 
Sijui kama lilishaulizwa hili swali, hivi kwanini TFF msilazimishe au kuweka sheria ya kila kilabu cha ligi kuu kuwa na kiwanja chake cha kisasa?? Maana Kuna baadhi ya timu mfano Yanga wanawezaje kwenda Uturuki na kulipa mapesa kibao ilihali ikija bongo kiwanja hata cha mazoezi hakuna?? Huoni hii itasaidia PIA kuwa na viwanja vingi ambavyo vitatumika kwa ajili ya mashindano mbalimbali ikiwemo CHAN, CAF na hata ya FIFA???
 
Mimi sina swali ina napenda kukupongeza sana hatua yako hii ya kujitokeza na verified account na kuja kujibu maswali ya wadau wa soka kupitia JF.Hatua hii ni ya kupigiwa mfano na viongozi wengine wanaooa dhamana ya uongozi ni kujitenga na watu waliokuchagua.Bravo kwa hili Brother Jamal
 

Unajua kuna vitu vingine vinakera, sasa yeye ana maana gani kunyamaza kimya baada ya kuulizwa haya maswali? Kuna watu takribani wanne wameuliza lakini yeye amewanyamazia kimya, ni bora akatoa neno lolote lile ili tujue amesema nini kuliko kukaa kimya. Samahani kama umeboreka.
 
Jamal Malinzi
Nakupongeza kwa hiyo kazi yako ya sasa;

Jitahidi sana na kwa moyo wako wote kuwatumikia Watanzania kwa kuwa walikuamini
wakakuweka hapo.

Angalia sana usilewe madaraka;
 
Last edited by a moderator:
Eng Jamal Malinzi,
Mimi naomba nikurudishe kwenye swala la Okwi, nimesoma ufafanuzi wako ila naomba kuuliza, Je ina maana TFF hamna imani na njia inayotolewa ICT?

Kuhusu Kapombe bado sijaelewa vizuri hivi tatizo la mafanikio ya mpira wa Tanzania ni kukosa wachezaji wanaocheza nchi za nje? Mbona Egypt imekuwa na mafanikio makubwa na wakati ina wachezaji wachache saana wanaocheza nje? Naomba ufafanuzi wako, kwani inaonekana wewe sasa unatafuta au ajenda yako ni kupeleka wachezaji nje, na wala si kujenga vilabu imara ambavyo vitakuwa chachu na ushindani kwa timu zetu, na ambayo ndo itafanya tuwe na timu imara.

Hakuna nchi ambayo imefanikiwa kuwa na timu ya Taifa imara, bila ya kuwa na vilabu imara vyenye mafanikio.

Naomba ufafanuzi, hili nimekuuliza baada ya kauri uliyosema umempa bila kumung'unya maneno Kapombe.

Hili kwangu halina tofauti na anayedhani bila watu kuja kutoka nje sisi wenyewe wazawa hatutafanya kitu.

Naomba niishie hapo kwanza nisubiri majibu yako Mh Rais wa TFF
 

uko sahihi kabisa,mfano mzuri ni promo iliyopigwa na Tanesco walipoanzisha huduma ya LUKU.Tutafanya vikao na wahusika maana mkataba nimeukuta ushasainiwa kitambo.
 

hili ni suala la reinforcement tu,kanuni za FIFA za club licencing zinaelekeza hivyo.
 

ahsante
 

Yombayomba unaweza kuwa na timu ya taifa imara bila vilabu imara,mfano ni Zambia mabingwa wastaafu wa afrika.Lakini pia unaweza kuwa na vilabu imara (Orlando Pirates) usiwe na timu ya taifa imara (bafana bafana).Uimara wa timu ya taifa ya Cape verde ni vijana wao wengi kukulia ureno (hata Nani wa manU asili yake cape verde).
TFF linapokuja suala la maendeleo na uongozi wa vilabu ina mipaka yake tena mikubwa tu,yako mambo vilabu huwrzi kuviingilia.
 
Last edited by a moderator:

Mh Jamali Malinzi,

Nashukuru kwa majibu yako, ila bado nina maswali haya kutokana na majibu yako.
1) Kwanza kwa faida ya kadamnasi nilikuwa naomba nikukumbushe tu kwanza , hujajibu swali kuhusu OKWI, je ni kuwa TFF haina imani na ICT, au kuna ICT za kughushi? Au hamuamini huo mtindo nyinyi uongozi mpya. Nasema hivi ili watanzania wote uweze kutuelewesha, ili kuondoa hoja inayoendelea mtaani kuwa mnafanya kazi kwa kupitia habari zinazoandikwa magazetini.

2) Nikirudi kuhusu kuwa na Timu ya Taifa yenye mafanikio, wewe ni engineer, ingawa ulihitimu siku nyingi, lakini nina imani mpaka leo bado unakumbuka Statistics, na umuhimu wake katika utafiti ili kupata majibu yaliyo sahihi.

Sasa takwimu za nchi ulizonipa hivi kweli wewe zinakupa majibu kuwa hilo ndo jibu la matatizo ya kukosa timu imara Tanzania yenye mafanikio?

Ok, chukulia Zambia as a case study, je umefuatilia kwa undani ni jinsi gani walianza kujenga timu hiyo?

Naomba niishie hapa wakati nasubiri majibu, na niwie radhi kukuchosha kwa maswali.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…